Yaliyotokea uwanja wa Soikoine yanaleta hasira na kichefu chefu

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Kilichotokea uwanja wa Sokoine Mbeya ni matusi, uonevu,kebehi,dharau,na manyanyaso kwa wapenda soka na michezo kwa ujumla.

CCM kwa makusudi huku wakijua kuwa Yanga watacheza mechi kesho tar.27/12/2019, jana wameruhusu kufanyika tamasha la mziki ndani ya uwanja huohuo ambao unasifa ya kuwa na matope km jaruba la mpunga. Tamasha lenyewe naskia lilikuwa la bure sasa kulikuwa na ulazma gani wa kufanya ndani ya uwanja?

Kwa picha nilizoziona uwanja haufai kabsa kuweza kuchezewa mechi ya hadhi ya ligi kuu kesho. Ntashangaa sn km timu zitaridhia kucheza kwenye hilo jaruba. Nitashangaa km Azam Media watakubali kuonyesha mpira kupitia television yao yenye viwango vya kimataifa.Ni aibu. Naskia hata waziri wa michezo Mwakyembe nae alikuwepo kwenye hilo tamasha. Sjui ataongea nn akisikia timu zimegoma kucheza!

Ndio maana huwa nafurahi timu ya Taifa ikifungwa,sababu ya huu usanii,upuuzi, na ubabaishaji unaoendelezwa kwa maksudi. Tukiwaambia waturudishie viwanja vyetu hawataki.

Wanaudhi sn hawa jamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo hamna la kufanya maana viwanja vingi ni vya CCM, na hata hilo tamasha walikwepo viongozi wa CCM pia,ni heri hizi timu ziwe na viwanja vyao au pia TFF iwe na kiwanja hata kimoja kila mkoa.

Watu wamefanya yao hata makopo hawajaokota asubuhi na kuna mechi,ni madharau sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Game zimeahirishwa, timu zimelekezwa zitafute viwanja mbadala [emoji1787]
 
Nimesikia bodi ya ligi umeufungia, kwahiyo mechi haitakuepo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Yaani ilikua nikukanyaga mixer tetema unafikiri kinatokea nin
 
Huu ni upuuzi wa hali ya juu anyway ,ni jitihada za awamu ya tani.Hongera Jpm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona Yanga wamezoea kucheza kwa matope? Uwanja wa KAUNDA SPORTS AREA una matope mengi kuliko huo wa Sokoine na Yangu huwa wanashinda kwa hiyo usihofu mkuu Yanga 6-Mbeya City 0

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM na Yanga Mbona lao ni moja?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…