Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
Ni lazima tujiulize lakini pia tujipe moyo. Tuliokuwa vijana mwanzoni mwa miaka ya tisini tumepita hapa na tukaona brutality (ukatili) wa watawala walioshindwa. Kuanzia tuliokuwa tunaandamana kumuunga mkono Mrema na baadaye kina Slaa miaka ya karibuni.
Vijana wameshawahi kujitoa mhanga kuanzia Arusha, Mwanza, Morogoro, Tanga, nk. Gen X walijaribu lakini bado hakukuwa na uungwaji mkono mkubwa na wananchi wa kawaida. Maandamano ya wakati ule yalikuwa ni ya kivyama zaidi kuliko ya kirika. Wengi wetu tulikuwa tumetoka CCM.
Gen X tulikaribia kuitikisa CCM hadi mwaka ule mabadiliko yaliposalitiwa. Sasa wamekuja hawa vijana ambao wenginwamezaliwa baada ya 1992...wamezaliwa wamekuta vyama vya upinzani vipo. Hawa wamekua katika mazingira ya vyama vingi na hivyo wanaweza kuona nini hawakitaki.
Wanasaidiwa zaidi na uwepo wa mitandao ya kijamii na oganaizesheni ambayo imenishangaza sana. Kati ya vizazi hizi viwili kimoja sasa kimekaribia kweli kuitikisa nchi na kuishtua CCM madarakani.
Kazi iliyoanzishwa na Gen X ikaahirishwa mara nne sasa inaweza kuja kumalizwa na Gen Z? Au nao watawaachia Millenials?
Nawatakia kila la kheri Watanzania.