Habari zenu wana JF. Nina rafiki yangu na ni jirani yangu wa karibu ambaye katika story mara nyingi alipenda kumsifia mumewe kuwa ni mwaminifu kupita kiasi hawezi kumcheat. Kumbe inaonekana jamaa alikuwa na mazoea ya kutoka nje lakini alikuwa anazingatia vigezo na masharti ya kuwa na nyumba ndogo. Jana ikatokea km bahati mbaya jirani akawa anachezea simu ya mumewe mara akaingia katika inbox na kukutana na sms za mapenzi toka kwa hawala kuwa anamshukuru kwa penzi tamu alilompa kwenda kwenye sent item akakumbana na jibu la mumewe kuwa hiyo ilikuwa cha mtoto ngoja wakutane tena. Bibie akatoka amepanic na kuja kwangu huku analia anaomba ushauri afanye nini. Nimeamua kuwashirikisha ili walau nipate mawazo yenu nijue nimshauri nini kwa sababu hajajiunga JF.