Yamenikuta kwa huyu msichana, naomba ushauri wenu

proxy

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
1,481
Reaction score
1,356
Habari za muda huu wana JF,

Siku kadhaa zilizopita niliomba ushauri wa kuhitaji zawadi ya kumnunulia huyu msichana, nashukuru kwa michango yenu kwa wale wote walionichangia Hivi huyu manzi nataka kumnunulia zawadi, binafsi nilifanikiwa kumnunulia zawadi na aliipokea ingawa hakulizishwa sana kwa zawadi niliyompa; aliniuliza maswali mengi sana kwa nini namnunulia zawaidi kama ile na nilikuwa na maana gani?

Leo nimekuja na swala lingine, nahitaji mnishauri pia. Ni kwamba toka kipindi chote hicho kabla na baada ya kumpa zawadi nilikuwa naendelea kuongea naye na kumtokea kwa nguvu zote majibu yalikuwa kwamba hataki kuoana na mimi kwa sababu ana mtu wake na anampenda Yesu.

Jana nimefanikiwa kukutana naye kwa mara nyingine na kukaa naye kuanzia saa 2 mpaka 5:30 usiku tukiongea na kujadili kuhusu ishu yetu. Lakini cha ajabu jana ameweza niaeleza ukweli kwamba yupo singo na hana mwanaume yeyote ila kinachompa kigugumizi ni dini yake, yaani yeye kaokoka na anampenda Yesu na mimi ni Mroma yaani Mkatoliki, so hana sababu ya kuolewa na mimi na anahitaji mtu mwenye imani sawa na yake.

Nilijaribu kumsihi sana kwamba mimi nipo tayari kumuoa hata kama dini imekuwa tofauti lakini alisisitiza kwamba hawezi fanya hivyo kwani akifanya hivyo ni kinyume na Mungu wake. Najua hapa kuna wanazuoni wengi na watu waliopitia changamoto kama hizi mpaka wakatoboa, naombeni ushauri wenu kwa hii kitu, binti nampenda na nahitaji kuishi naye.
 
Huyo hakutaki tu. Mkatoliki na mlokole wote ni wafuasi wa Yesu. Utofauti ni namna tu ya kuabudu na kujitoa mbele za mungu Ila sioni mantiki eti ubadili dini, mmekuwa Mkristo na Muislamu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
proxy,

Ushauri wa bure achana naye oa wa dhehebu lako hawa waliookoka kumzidi Yesu wanasumbua sana katika ndoa waoane wao kwa wao
 
Yawezekana hana sehemu za siri au hakupendi. Siku hizi hakuna anayetanguliza dini
au kabila. Mapenzi hutangulia kisha mengine yote hufuata
 
Mkuu heti anadai ukimuoa wewe atamkosea mungu? Kwani wewe huko RC una muabudu Mungu yupi? na yeye huko aliko okoka ana muabudu Mungu yupi?.

Wao huko ulokoleni wanatumia kitabu kipi kwa mahubiri na wewe huko uromani mnatumia kitabu kipi kwa mahubiri?

Hilo dhehebu la kilokole nila kikiristo ama ni la Budha

Ushauri wangu huyo mwanamke wako bado hajawa na Akili za kujitegemea badala yake anashika kile anachomezeshwa na Viongozi wake. Piga chini tafta mwanamke anaejielewa.

Binafsi Sina mpango wa kuja kutafta mwanamke wa kuoa kwa kigezo Cha dini Wala dhehebu. Huu Ni ujinga wa kutukuza utamaduni uliotufikia mwishoni mwa Karne ya 18 Baada ya wazungu kuja Afrika.

​
 
Ushauri wa bure achana kabisa na viumbe wanaosemaga wameokoka utakuja kuichukia hiyo ndoa yako bure na wakati huo hapatakuwepo wa kukusaidia.hawa watu wa kushinda kanisani muda wote ni hatari sana kwa afya yako ya ubongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo hakutaki tu. Mkatoliki na mlokole wote ni wafuasi wa Yesu. Utofauti ni namna tu ya kuabudu na kujitoa mbele za mungu Ila sioni mantiki eti ubadili dini, mmekuwa mkristo na muislamu???

Sent using Jamii Forums mobile app
Na tofauti nyingine ni kwamba mlokole yuko tayari ata alale njaa ila apeleke mchango kanisani baba mch.anunue usafiri
 
Mkuu, endelea kumkazia tu atakubali, kama amekuambia ukweli kuwa yupo single tofauti na alivyokuambia mwanzo maana yake hata dini atabadilisha tu.

Ikishindikana kabisa kumshawishi na unaona unampenda kabisa hauwezi kuoa mwingine mnaweza kukubaliana. Kanisa Katoliki lina utaratibu ambao nyote mnaweza kufunga ndoa (Kanisa Katoliki au huko kwa Walokole) na kila mmoja akabaki na dini yake.

Wewe utaendelea kuwa Mkatoliki na yeye ataendelea kuwa Mlokole. Sema mtakuwa mnawachanganya watoto japo ili mruhusiwe itabidi aingie mkataba na Kanisa Katoliki kiwa watoto mtakaojaliwa watakuwa Wakatoliki.

Ongeeni mkubaliane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…