Yamenikuta kwa huyu msichana, naomba ushauri wenu

Tafuta wa dhehebu lako tu

Kweli,ili kuondoa usumbufu afanye hivyo, kama sivyo afuate dini ya mchumba wake na aipende pia la sivyo kama kampenda binti na dini akaona isiwe shida ngoja aende tu, watakuja kutofautiana huko mbele.
 
Fact.
Wee Jamaaa unakaa na mwanamke kujadili kumuoaa???? Mle kimasihara kwanzaa ufalaa uo... Alafu wote wakristo anaanza kukuletea siasaa... Akupendi aiseee unapoteza muda apoo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani kama kweli unampenda kuokoka sio kubadili dini we okoka utakuwa umepiga hatua mbele kuliko yeye kuukataa wokovu atakuwa karudi nyuma,,
Ni ushauri tu
 
Nafikiri kuna maelekezo flani huwa wanapewa kutoka kanisani ili kuongeza wateja wao na pia mhusika anaogopa kutengwa na kanisa ,hii Wenda inaweza kuwa sababu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeanza vizuri ila mwishoni umehalibu ,hakuna tatizo lolote zaidi ya yeye kukomaa na dini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mwanamke pia ana heshima yake ,na sio rahisi kama unavyochukulia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri mzuri mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani Karne hii una bembeleza manzi wakati hata papuchi ujaiona acha udwanzi wewe
 
sjui ni kwa nini hua naonaga mwanaume akibadili dini kumfata mwanamke namuona huyo mwanaume dhaifu sana

Ki-imani, alichosema mdada ni sahihi,ki-imani hairuhusiwi kuoana na MTU wa imani tofauti hata biblia imefundisha hivyo

Ila sasa naona kama mdada hampendi mtoa mada, so anatumia kigezo hicho cha dini kumkataa mtoa mada, na huyo mdada ana mwanaume wake anaempenda, sema huyo mwanaume Pasua kichwa

Ewe mtoa Mada, ukiona unatumia nguvu nyingi kumpata mwanamke kimapenzi, ujue huna chako hapo Madame S proxy
 
sjui ni kwa nini hua naonaga mwanaume akibadili dini kumfata mwanamke namuona huyo mwanaume dhaifu sana
Umesema kweli. Mwanaume kubadiki dini kwa ajili ya mwanamke ni udhaifu. Umchague, umtongoze, umtunze bado nifate dini au dhehebu lake? Over ma.dead body

Bazazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri mzuri mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi ningekua ni wewe, ningeachana na huyo mwanamke. Sababu kuu za kuachana nae ni hizi:

1. Huyo dada anaonekana ana kiburi, jeuri na hana shukrani. Kitendo cha kumpa zawadi kisha anaanza kuhoji, tayari hiyo inaonyesha huyo ni mtu wa aina gani. Hebu fikiria ndio mpo ndani utaishije na mtu kama huyo? Najua wengi hua tunadhani kwamba mtu akiwa mlokole basi anakua "malaika" ila sio kweli, ulokole hauondoi hulka halisi za mtu.

2. Hana mapenzi ya kweli, mapenzi yake ni "conditional". Yaani ili akupende, ni mpaka utimize anachotaka yeye na sio unachotaka wewe. Huyu atakusumbua sana huko mbele amini usiamini.

3. Hana msimamo! Mara aseme ana mtu, mara hana mtu, mara akikuona anachanganyikiwa, mara hakutaki..!! Huyu hajielewi mkuu mi ningekaa nae mbali sana.

4. Ikitokea ukalazimisha mpaka mkaoana, changamoto za kuishi na mwanamke mlokole ni nyingi kuliko unavyofikiri. Maisha yenu yote yataongozwa na mchungaji wake. Atakachosema mchungaji, ndio kitafanyika haijalishi wewe kama mume unataka nini. Ndio maana hata sasa anakusumbua kwani mchungaji wao alishawaambia wasikubali kuolewa na mtu ambae hasali hapo kwao. Hata ungekua mlokole, lakini ukawa unasali kwa mchungaji mwingine, bado kuna uwezekano ungekataliwa!

Mwisho: Wanasema mapenzi ni upofu. Inawezekana wewe umeshampenda/tamani huyo dada kutokana na sababu zako unazoona wewe. Hiyo imekufanya usisikie wala kuona madhaifu yoyote mengine ya huyo dada. Sisi hata tupige kelele kiasi gani, bado uamuzi ni wako.
 

Nilipomweleza kwamba nampenda akatoa kigezo cha kuwa anamtu wake na tukazungushana sana kama miezi 3 hivi ,ila juzi amenieleza kwamba mzunguko wote ule ni kwa ajili ya imani ,pia kuhusu zawadi nilimnunulia seti ya chupi ndio maana akahoji kwa sababu aliona kama ni zawadi ya kumpenda kingono ndio maana alihoji, lakini pia kuhusu kubwa na mtu nimefatilia sana kwa watu anaofanyanao kazi, pia aliokaanao mwanzoni wanasema hawajawshi sikia huyu manzi anamwanaume na hawajaona aliwa na mwanaume yeyote, pia hapo anapokaa wamepanga na mdada ambaye pia ni mfanyakazi na nikiwa naenda pale kwao ananiona na naongea naye vizuri na tunafaamiana, nilijaribu kumuuliza kulikoni kwa huyu msichana Je anamtu kaniambia hajawahi ona na wameishi zaidi ya miaka 2 sasa, hajaona mtu anakuja pale wala kuona anamishe za namna hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sawa mkuu. Ndio maana nilianza kwa kusema "mimi ningekua ni wewe...." bahati nzuri mimi sio wewe, we endelea tu mkuu. Kila la kheri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…