Yamenikuta leo Mama G

Yamenikuta leo Mama G

pole.. ila huu ni ushauri kwa watu wote
MLANGO UNAPASWA KUFUNGUKA KWA NJE... in case ikitokea BALAA lolote ni rahisi kuvunja.

Lab doors huwa inafunguka kwa nje.. ikitokea ajali ya moto watu wanapiga teke wanasepa nje.. tofauti ukiwa unafunguka kwa ndani.. mijitu inajazana mlangoni kila mtu anawahi kitasa avute ndani wakati nyuma yake kuna mijitu mingine inasukumana kutoka nje.. mwisho wa siku wanadedi kama kuku
Asante nimekuelewa
 
Kama kungekua na CCTV camera mule ndani inarekodi ningekua kituko cha dunia!!
Maana nilizunguka kila engo ya store!
Mwishowe nkajichokea na kulala kwenye gunia la pumba hadi asubuhi nilipopata wazo
Hahaaaahaaa!!panya walilala na wewe!
 
Dah pole mama Sabrina!! Nina mkasa unaofanana na wako kidogo,kuna siku panya walikua wanasumbua sana kwenye store ya kihifadhia pumba ya kulisha nguruwe!! Siku moja niko free nikasema ngoja niwakomeshe maana nilikua hata nikiwawekea sumu hawali,.
Nikatoa magunia yote ya pumba nikacha moja tu ambalo kwa chini nilikua na mbao ambazo wamejificha humo.
Nikachukua mpini wa jembe nikawasha na taa yenye mwanga mkali nikabamiza mlango paaaah! Ili nikitembeza rungu wasitoke!! Niuwe wote
Nikatoa lile gunia ambalo kwa chini panya wengi wamejificha kwenye zile mbao,walitoka panya wengi wakirandaranda wasione pakutokea!.
Mi nikaanza kutembeza rungu nikaua wote pamoja na vitoto(sikumbuki idadi)
Nakuja kufungua mlango niwatoe nifanye usafi mlango haufunguki!! Vuta wapi kitasa kimejiloku afu home nipo alone simu ipo chaji geto
Nakumbuka nilikaa mle store kuanzia sasa 11 jioni mpaka kesho yake saa 2 asubuhi ambapo nilipata wazo la kutoboa ceiling board nikapita daarini mpaka kutobozea kwenye korido ya geto
Wewe ulikosea ungepiga mikeleeee mpk watu waje![emoji3][emoji3][emoji16][emoji23]
 
Huko daarini kuna vumbi,mixer nyaya za umeme halafu Giza nilivyotua tu koridoni nikaenda oga ndoo kama tatu kubwa
Kesho yake nikaenda kibosho hospital kucheki afya maana nilipata homa na mshtuko
[emoji16] [emoji16] ila ulipata tabu..masaa yote hayo umekaa na panya ..uwiii sijui kama ningeweza
 
hayo maspirit yalinishindaga nilianzaga grants..nikaja JD...nikahamia jameson hadi captain morgan zote zikanishinda ...huwa nakunywa wine ila kwa habari njema kama hizi wine lazima niipumzishe kama wiki mbili

maisha yenyewe mafupi nisije nikafa huku sijanywa za buku buku
Sawa mi napenda wine na whisky zaidi,bia nakunywa tu kwakweli
 
pole.. ila huu ni ushauri kwa watu wote
MLANGO UNAPASWA KUFUNGUKA KWA NJE... in case ikitokea BALAA lolote ni rahisi kuvunja.

Lab doors huwa inafunguka kwa nje.. ikitokea ajali ya moto watu wanapiga teke wanasepa nje.. tofauti ukiwa unafunguka kwa ndani.. mijitu inajazana mlangoni kila mtu anawahi kitasa avute ndani wakati nyuma yake kuna mijitu mingine inasukumana kutoka nje.. mwisho wa siku wanadedi kama kuku
Okay sawaa...ila nyumba zetu za kibongoo haziko hvyo hapa narecall movie nilizoziona almost zote milango yafunguka kwa nje
 
Ahaaa sawa nimekupata mi hata sijui hii ni mbao ipi ,
Ya kupanga bana kujenga ni uoga wa maisha [emoji6]
Hapo huna la kufanya ila ingalikuwa yako ungebadilisha. Muulize Nyani Ngabu akueleze jinsi ilivyo lazima kwa nyumba, huko majuu kwao, mlango kufungikiwa nje baadala ya ndani kwa usalama. Aidha ukiwa na mlango wa nje ukafungukia nje, fatuma (nadhani unaelewa ile wezi wanakuja na jiwe kubwa kubamiza mlango) haiwezekani hadi mlango upasuke vipande. Kwa mlango unaofungukiwa nadani fatuma ni kama ugumu wa mkate kwa chai
 
Huko daarini kuna vumbi,mixer nyaya za umeme halafu Giza nilivyotua tu koridoni nikaenda oga ndoo kama tatu kubwa
Kesho yake nikaenda kibosho hospital kucheki afya maana nilipata homa na mshtuko
Hahahahahaha hukukutana na wadudu
 
Back
Top Bottom