Yamenikuta, maji yapo shingoni, naomba ushauri wapendwa plse!

huyo dada kabila gani?? na wewe ni kabila dani dini zenu ni zipi then tunaweza changia zaidi haya mambo yanaendana na udini na ukabila vile vile!
 
mmmh,ndoa ndoana.inashangaza,baada ya ndoa mke kubadilika.kwa kifupi huyo mke hana mapenzi tena na wewe,ila juu ya yote lazima kuna sababu,muulize,ukishindwa mchunguze bila ya yeye kujua ndio utaujua ukweli.hilo suala la mtoto apelekwe kijijini hiyo ni roho mbaya.kwani mtoto ni mtoto.na mtoto hana makosa,huyo mtoto hata ukimuachia hatomlea vizuri
 

Dah!!Pole yako!

Well kwanza mkalishe chini umuulize nini sababu ya mabadiliko yake.Kwanini sasa hivi ndo aone ndugu zako pamoja na mwanao ni wabaya??Asipokupa majibu ya kueleweka ni bora muachane tu.Inawezekana amepata mtu huko wa kumpa kiburi....usiruhusu mali zikufunge kwenye kifungo cha mateso.Kama ulivyozipata hizo utapata na nyingine.
 

Sitaki kuwa kwenye hukumu ya kushauri watu kuachana,ila mimi mke kama hawapendi ndugu zangu au wazazi wangu basi hanipendi!
Hey,kwani unadhani una tofauti na ndugu zako?...no,nyie ni damu moja,na hiyo damu haipendi!
Kwanini kuendelea kung'ang'ana nae?

Sasa napata akili kwanini mamangu alinambia nisikimbilie kuoa,...natamani ningekuwa karibu nikupe kalamu uanze kuchana mistari ya talaka fastaaaa!

Unajua ni kiasi gani wazazi wako wanaumia kwa kutokuwa huru kuja kwako lakini eh?
Unafurahia maumivu hayo?

Kama haonekani kupatanishwa achana nae,tupa kule
 
Kama walivyosema wengine hapo juu kwa nini abadilike ghafla inawezekana nduguzo wanamsimanga ukiwa haupo, cha msingi chunguza ujue chanzo ni nini na ukiona ye ndio mwenye makosa mpe muda ajirekebishe kwanza usikurupuke kumuacha na kama hataki kujirekebisha basi chapa lapa kwani mali kitu gani my dear mali zinatafutwa utapata nyingine pengine zaidi ya hizo.

Kama ukiridhishwa yeye ana makosa halafu hataki kujirekebisha ni pm nikupe mbinu zitakazofanya msigawane mali za uhakika labda kijiko na vigoda tu
 
achana nae huyo m/mke najua unaweza ukawa unampenda sana huyo mchumba wako lakini kwa nn aanze kukuonyesha red light mapema kiasi hiki wakati hata bado hakujapambazuka? Nina mfano wa ndg yangu mmoja alikuwa na kesi kama yako na walipoishia ni jamaa kuacha kila kitu kwa mkewe na akaenda kuanza moja, Bora wewe bado hata hamjafunga ndoa huyo ndg yangu yy alikuwa ameoa ila mkewe alikuja kumfukuza mama mkwe wake wakati jamaa yuko safarini.

Suala la mali sio issue kwanza hamjaoana mtagawana vp mali? nani ana ushahidi kuwa mliishi pamoja, timua huyo mapema au kama vp uza hivyo vitu mtimue halafu nunua vipya. Nakushangaa unashindwa kumtimua kwa kuofia mtagawana mali wakati sio mke wako?

Amka huyo si mke nakwambia na kama ukimuoa utapata laana ya ndugu, marafiki, wazazi na wafanyakazi wenzio hicho ni kimeo MUNGU amekuonyesa tu mapema
 
Mkuu umepotea sana
 
L.o.l Maty leo utafanya mkoloni wangu anipe notice kwa ajili ya kucheka
 


Hizo red zimefanya nikwambie hivi:
1. Huyo mwanamke kukujibu kuwa hakulazimishi kuishi na wewe ni dalili mbaya sana eidha amekuchoka au kama kuna mtu hapa kasema angalia wasije wakawa wameshamchakachua na kumfundisha ujinga ili aachane na wewe ili mgawane hizo mali.
2. Hiyo ya kugawana mali umenishangaza sana wewe kama umemchoka na humtaki unaogopa nini kumuacha mali zinatafutwa lakini amani haitafutwi kama mali so amua tena ningekuwa mimi sigawani nae chochote namwuachia kila kitu.

Nawasilisha
 
Usikurupuke Bro kumuacha mkeo.

Fanya uchunguzi inawezekana ni hao ndugu zako ndio wana maneno. Ndugu hasa kama tegemezi au hawana cha kufanya kijijini, lazima watajaribu kuingilia ndoa yako ukiwachekea wanahania mjini kabisa na kujaza nyumba milele.

Isitoshe imeandikwa kila mmoja atamuacha baba na mama yake na kuambatana na mkewe, hao wawili watakuwa mwili mmoja. Kama nyie mnaelewana ndugu ndio wawaachanishe?? Labda hilo la mtoto wako kutokuishi na nyie ndio la msingi.

Ndoa changa haipendezi ndugu kuja kuishi na nyie manake mnakosa faragha.
 
Kama walivyosema wachangiaji wengine jua chanzo cha mabadiliko hayo, usipende kusikiliza maneno kutoka kwa ndugu zako inawezekana yanaukweli au uongo
ukishajua ukweli yeye ndio chanzo cha matatizo ni bora kumwacha
 
Dah dunia hii bwana kweli tu wasafiri. Hebu mshirikishe Mungu kwa nia moja hilo tatizo, hebu jaribu kuongea naye kwa lugha ya upendo, mweleze muulize ujue kwa nini anafanya hivo. Hebu tulia ili upate kujua kiini cha matatizo hayo nini? Haiwezekani awachukie wazazi na ndugu zako bila sababu. Na sababa inaweza kutokana na yy mwenyewe, mf. uchoyo nk nk, au ikatokana na hao wazazi/ndugu. Pengine ndugu hao wanamuona kauzibe kwa yale unayo/uliyokuwa unawafanyia na sasa hufanyi au unafanya kidogo.
 
Mkuu pole sana kwa kisa hiki....kifupi ni kwamba huyu sio mtu mwenye upendo na wewe na sio wewe tuu kwa ujumla hana hata chembe ya upendo na familia yako...bora kwa ndugu lakin hata kwa wazazi?...sidhan kama atarekebika huyu...kama hawapendi wazazi wako unadhan hata wewe anakupenda kweli? huyu nadhan yuko na wewe kwa sababu ni mtafutaji na pia hana future nzuri na wewe..mwanamke asietaka ushirikiano familia ya mume ni hatari sana. iko siku atakulazimisha ujikute huna uhusiano mzuri na wazazi na ndugu..watch out bro..mali na nyumba zisikufanye ujutie mashine mwako...zinatafutwa kirahisi ila uhusiano wa ndugu na wazazi ni kovu ambalo halifutiki kirahisi..huna mtoto nae na kuzaa bado ni issue halafu anakuwa na nyodo hivyo..nadhan fikiria kwa undani..usiogope mali kupotea.
 
Hapo hakuna kitu Mangi,ishi kwa amani.wasiwasi wako ni mali.mimi wa kwangu nimemuachia kila kitu,nilitoka na nguo zangu na vitabu tu.mali utatafuta tu man.

hahahahaha nimecheka mpaka mbavu zinauma lol, we kweli ulimchoka
 


Aisee kuna ndugu wana midomo na wanataka maamuzi yote muhimu kati ya wanandoa wahusishwe. Pia kuna wakwe ukiwachekea kutwa wanashinda hapo kwenu ilhali watu ndio kwanza mmeoana mnataka privacy.

Mara nyingi ndugu wa upande wa mume wanachangia sana ndoa za watoto wao kuvunjika. Wanaume tuamke na kukataa kutawaliwa na wazazi wetu hata kama wametuzaa. Familia yako ya zamani (wazazi) na ndoa yako ni vitu viwili tofauti, ukijaribu kuvichanganya una haribu. Haiwezekani mkeo awachukie ndugu zako bila sababu. Huyu bibie lazima hawa ndugu wa mume walisha mletea za kuleta ndo maana kawadelete.
 
Mkuu, kwa maelezo yako unaonesha kuangalia consequences za kuachana ...

the fact kwamba unafikiria ivo ni kwamba tayari ameshakutoka, hili la kusema bado unampenda siliamini sana maana hata mimi ningempendaje mtu hapendi ndugu zangu, hapendi mtoto wangu nk? Huenda ana act ivo sababu anajua anaweza asipate mtoto maishani but she could do better

kama yeye anaona pia kuachana na wewe sio issue, manake pia hakupendi kivile.....sasa angalia maisha yako yanaenda pande gani kama vipi tafuta mpango wa kando utulie zako kimyaaaa....:A S-key:
 
L.o.l Maty leo utafanya mkoloni wangu anipe notice kwa ajili ya kucheka

Mbona hicho kitu kidogo tu kama analeta jeuri, mnagawana na yule mliezaa nae for the sake of your child/children au yule ambae wewe baba umeamua kumuacha bila sababu so umempotezea muda wake. Lakini ambae analeta dharau, unamuomba abadilike hataki dawa yake ndogo sana

Kaka yangu yoyote humu akipata tatizo kama hili usisite kunitafuta utafurahi na roho yako, tena free of charge, ila uwe na uhakika wewe huna makosa hata chembe maana nikizungumza tu na wewe tajua kama u mkweli au unaleta usanii
 

Ndio inabidi kabla ya kuchukua maamuzi achunguze kwa umakini kabisa nini chanzo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…