Mkuu, pole sana na hizo changamoto.
Najua wengi wameshauri kwa kadiri ya uwezo wao, lakini kwa upande wangu ningeshauri wazo la 'KUVUNJA NDOA' ondoa kabisa.
Hebu fuata ushauri uliotelewa na wadau hawa
Ndugu Lumecha
wachunguze hao ndugu zako, watakuwa wana tatizo ndio maana mkeo anawachukia. Labda wanamsimanga na kumpiga majungu kwa vile hajapata mtoto na wewe.
Ndugu wa baadhi ya wanaume wamekuwa wakiwafanyia visa wake za ndugu zao kwa sababu nyingi ikiwapo kuwa na tofauti ya makabila, life style, kukosa watoto, mali etc.
Kama mwanaume usipotumia busara na uchunguzi usiokuwa biased, unaweza vunja ndoa yako.
Usizungumze na kila upande kivyake, usitumie mshenga, babu, bibi au mjomba. Subiri hadi utakaporudi myazungumze kwa pamoja, mke na nduguzo.
Labda uliwaringishia ndugu zako kuwa mke wangu nimemsomesha mwenyewe, ni mwema sana, atawasaidia. Ukawapa expectations za uu kuliko mkeo alivyoweza kuwatimilizia, wakaanza kumchukia na kumfanyia visa. Na yeye anajiona ni mke na anastahili heshima kutoka kwao pia. Lugha au vitendo vikagongana.
Waambie nduguzo kuwa huyo ni mkeo, ni familia yako na anastahili heshima kama wanayokupa wewe, wakimdharau wamekudharau wewe.
Mwambie mkeo hao ni nduguzo na wanastahili heshima kama anayokupa, akiwadharau kakudharau. Hivyo hivyo na kuhusu chuki.
Mwanaume lazima uwe na msimamo sio kulegalega na kukimbilia kuvunja ndoa.
USITOE SIRI ZA MKEO AU UBAYA AU UZURI WA MKEO KWA NDUGUZO, LAZIMA WATAMCHUKIA.
Dah dunia hii bwana kweli tu wasafiri. Hebu mshirikishe Mungu kwa nia moja hilo tatizo, hebu jaribu kuongea naye kwa lugha ya upendo, mweleze muulize ujue kwa nini anafanya hivo. Hebu tulia ili upate kujua kiini cha matatizo hayo nini? Haiwezekani awachukie wazazi na ndugu zako bila sababu. Na sababa inaweza kutokana na yy mwenyewe, mf. uchoyo nk nk, au ikatokana na hao wazazi/ndugu. Pengine ndugu hao wanamuona kauzibe kwa yale unayo/uliyokuwa unawafanyia na sasa hufanyi au unafanya kidogo.
Mtu ataachana na mama yake na baba yake, nao watakuwa mwili mmoja, alichokiunganisha Mungu mwanadamu akiwepo mzazi na ndugu wasitenganishe. Chonde chonde kaka angu Mama yako hata pamoja amekuzaa asikutenganishe na mke wako. Tafuta jinsi ya kuishi na mkeo kwa akili kamwe mama hawezi chukua nafasi ya mke moyoni mwako, atabki mama tu milele, fikiria kk ukimuacha huyo ukamuoa mwingine wazazi wakamchukia tena utamuacha? Dah bwana labda kuna sababu ingine, hicho cha kujibu inategemea na mazingira. Nakuja!!
Siku zote lazima tujifunze
kutatua na sio
kukimbia matatizo. Kama ndoa yako ni ya KIKRISTO, basi imekatazwa kabisa kwa wanandoa kuachana isipokuwa kwa sababu ya uzinzi.
Kwa vile tatizo lako linaweza lisihusiane na uzinzi hivyo basi, yakupasa kutatua tatizo, labda ukirudi kutoka kubeba box.
Kaa na watu wenye busara, watu wa kanisa kama wachungaji jaribu kupata ushauri wao. Pia jaribu kutafuta nafasi nzuri ya faragha kuzungumza na mwenzio. Hayo matatizo yote yanasuluhisho... Hebu weka moyo wako na uamini kuwa utayapatia ufumbuzi matatizo yako na sio kuyakimbia, kwa sababu huna hakika utakutana na mtu wa namna gani.
Kama mliweza kupanga na kufunga ndoa pamoja na changamoto zote zile huoni kuwa unaweza kupata suluhisho??
Ndoa yako ni changa sana, haina hata mwaka,hivyo nafasi ya kupata solution ni kubwa sana. Mkae chini mzungumze
Labda angalizo kwa wasomaji wengine, mojawapo ya vitu vilavyoleta matatizo katika ndoa ni
WATOTO wa nje kuletwa ndani ya ndoa. ni wanawake wachache sana wanaweza kuvumilia kwa moyo mmoja, lakini kama ikiwezekana watoto wa nje uwahudumie kivyao vyao..
Asante