Makonde plateu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 1,443
- 3,480
Nilimuambia kama ukiondoka na huyo mtoto basi jua kuwa sitamhudumia kwa chochote. Mwanzo nilikua naongea kama utani kwani niliamini kuwa mke wangu hawezi kuondoka. Ni kweli nilishamfanyia mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kumpa ujauzito mtoto wa mama yake mdogo. Kuna kipindi nilimp!ga mpaka akaishia kulazwa hospitalini kwa wiki mbili ila bado niliamini kuwa ni mke wangu na nina haki ya kumfanyia chochote kwa kuwa ni mke wangu.
Ukweli ni kuwa mke wangu hakuwahi kunikosea kwa chochote; changamoto ilikuwa mimi. Nilikuwa sijiamini kwa sababu kipindi nakutana naye sikuwa na kitu, sina hata shilingi mia lakini alinikubali na kunivumilia. Yeye alikuwa akifanya kazi serikalini ila nikahangaika mpaka akaacha kazi na kuwa mama wa nyumbani. Kingine ambacho kilikuwa kinaninyima amani ni kunizidi elimu; yeye alikuwa na digrii na mimi ni darasa la saba. Kila mtu alikuwa akiniambia huyo mwanamke si mwanamke wako, wasomi wenzake wanatembea naye.
Maneno ya watu yalinifanya kuwa na kisirani. Jinsi nilivyokuwa namnyanyasa, analia na kuniomba msamaha, ndipo nilihisi mimi ni mwanaume, najiona kama nina akili huku nikimfanya ajione kama taahira hana akili hawezi kuishia bila mimi. Nilifanikiwa kumtenga mbali na marafiki, ndugu zake walimchukia kwa ajili yangu, mpaka anaondoka nilijua kuwa hakuna mtu atampokea. Siku alipoondoka kwangu, nilimpigia simu mama yake, nikilia kama mtoto kuwa mke wangu kaondoka kaenda kuishi na mwanaume mwingine.
Mama yake ambaye ni mtu wa dini alinipa imani kuwa hawatampokea hata alipopiga simu kwao hakuna mtu alimsikiliza. Kipindi hicho tulikuwa na watoto wawili, mmoja mkubwa wa miaka 4 ambaye nilimchukua, na mwingine wa miezi 6, huyo nilitaka kumchukua lakini akakataa. Nikamuambia asiponipa mtoto sitamhudumia kwa chochote. Nilijua hana kazi, hivyo nilijua kuwa atarudi.
Aliondoka lakini hakurudi. Mwaka mzima mke wangu alikaa mbali, nilikuwa namfuatilia na kutuma watu kujua kama ana wanaume wengine au la, lakini haikua hivyo. Aliondoka na akaanza kupambana, akafungua duka lake la vyombo, biashara aliyokuwa akiipenda, na kweli ilianza kwenda vizuri. Sijui alipata wapi mtaji ila nahisia likua akijikusanya kwa muda mrefu ni kama alishapanga kuniacha, alishachoka manyanyaso yangu na kuamua kujipanga kuondoka! Nilituma watu dukani kwake kuona biashara inaendeleaje na kweli ilikua inakua kwa kasi. Mimi nilikuwa na magari ya mizigo, nilikuwa na fuso 7 pamoja na kenta 4.
Gari la kwanza kununua ilikua ni pesa ya mke wangu, alichukua mkopo kazini na kununua ili nisiendesha magari ya watu. Bada ya hapo ndiyo nikaanza kufanikiwa na kumlazimisha kuacha kazi kwa kumuamabia nitamfungulia biashara ila sikufanya hivyo! Nilikuwa na kila kitu na kweli biashara zilikua zinaenda vizuri ila sikuwa na amani.
Kila nilipoona mke wangu anaendelea vizuri, mambo yanamnyookea, nilikasirika. Nilichukua mwanamke mwingine kuishi naye lakini sikuwa na amani. Tulikuwa tunagombana kila siku kwa kuwa kila siku nilikuwa namzungumzia X wangu ilimkera naye akaondoka.
Mwisho niliamua kwenda kuomba msamaha kwa mke wangu. Niliomba msamaha hadi kulia lakini hakutaka kurudi. Alifanya kitu kingine, badala ya kurudi niliishia kuitwa Mahakamani kuwa kafungua kesi ya talaka. Hapo ndipo nilijua lazima kuna mwanaume anampa kiburi mke wangu. Nilishangaa kupelekwa moja kwa moja mahakamani badala ya kupitia ustawi wa jamii, na nilihisi kwamba kuna mwanaume anamshika mkono.
Nilisahau kila kitu nilichomfanyia, nikawa namtangaza kwa maneno mabaya, lakini mke wangu hata hakujali. Siku moja nilikuwa nimekaa najiuliza, ni kitu gani nitamfanyia mke wangu kitakachomuu*miza sana na kumfanya ajione mjinga. Nikafikiria mtoto wetu. Wakati huo mtoto mdogo alishafikisha miaka miwili hivyo nilijua kuwa naweza kumchukua bila shida.
Siku moja akiwa dukani kwake, nilikwenda nyumbani kwake, nikamkuta binti wa kazi na kumchukua mtoto kwa lazima, kumleta kuishi kwangu kwa kuwa kipindi hicho sikuwa na binti wa kazi wala mke wa kuishi naye. Hivyo nilimpeleka kwa dada yangu, ambako mtoto mkubwa wa miaka 6 naye alikuwa akiishi huko.
Nikamwambia mke wangu kwamba akitaka watoto wake basi arudi kwangu, la sivyo ataona mai**ti zao tu! Hilo ndilo lilikuwa kosa langu, nilimtumia SMS nikisema hivyo, yeye hata hakunijibu. Alienda moja kwa moja polisi na kudai watoto wote. Sheria ilikuwa upande wake kwa kuwa kipindi hicho alikuwa na kipato kizuri, lakini pia SMS zangu za matusi na viti*sho niliyomtumia viliwafanya wakampa watoto wote.
Ndiyo, mke wangu alichukua watoto wote. Niligoma kuwahudumia lakini alikuwa na kipato chake na wala hakunihitaji. Niliumia sana na kuona ni kama dharau, ningeweka wapi heshima yangu? Ilikuwa lazima kumkomesha mke wangu. Niliwaza ni kitu gani kinampa kiburi na nikagundua ni lile duka lake. Hivyo, nilijipanga na vijana wangu kama 3 hivi. Usiku tulienda na kumpa mlinzi hela, hivyo tukaingia kwa juu.
Hatukuiba chochote, nilichofanya ni kuvunja vyombo vyote. Unajua vyombo vya udongo, nilivunja kila kitu kisha nikaondoka na wale vijana wangu. Hatukuchukua kitu chochote, nilijua kabisa kuwa atajua ni mimi niliyefanya hivyo ila sikujali. Asubuhi alipoingia dukani na kukuta ile hali, alinipigia simu na kuniambia nashukuru kwa kila kitu, Mungu akubariki.
Kwa hasira, nilianza kumtukana na kumuambia kuwa nimefanya hivyo makusudi ili kumkomoa. Nilimuambia hata akifungua duka jingine nitakuja kuliharibu, nikamtukana sana. Nikifurahi kumkomoa kumbe ile simu ilikua ni mtego, jioni sina hili wala lile polisi walikuwa nyumbani kwangu, nikakamatwa na kuwekwa ndani, bada ya kubanwa saa si nikakubali nikiamini nitatoa pesa tu mam yaishe, naona kuwa polisi ni watu wangu, kwa biashara yangu ya fuso nilijua kuwa Polisi ni watu wangu kwani naonana nao kila siku, tena kuna rafiki yangu mmoja aliniambaia wewe kiri tu hii ni kshi ya kifamilia ukikubalia utajiandikisha kumlipa mke wako, sema utamlipa taratibu taratibu kesi ya madai hata ukikaa miaka 10 hufungwi unalipa kidogo kidogo.
Nikaingia mkengea si nikakubali nikidhani itakuwa kesi ndogo, kwamba nitalipa tu deni, kumbe nilikosea. Ilikuwa ni kesi la jinai tena ujambazi wa kutumia silaha. Sikua nasomewa nasomewa shitaka niliambiwa kuwa siwezi kupata dhamana, ikabidi kutafuta wakili naye ananiambia hukumu ilikuwa ni kuanzia miaka 30 mpaka kifungo cha maisha. Kweli nilijikojolea, nakumbuka nilivyokuwa mahakamani, nikiwa sina uhakika wa chochote!
Mke wangu aliposikia hilo aliniambia kuwa amenisamehe kama ni biashara au chochote au chochote hataki anataka kufuta kesi. Hata yeye mwanzo alijua ni kesi ya madai ila kwenye Kamera tulionekana na mapanga. Alijaribu kufuta kesi ila polisi walimwambia kuwa hii ni kesi ya jinai inaendeshwa na Jamhuri, si kesi ya madai.
Labda niishie kusema kuwa nimekaa ndani miaka mitatu, mpaka natoka mke wangu alipambana sana, naweza kusema kuwa niliuza kila kitu ili kuhakikisha natoka. Namshukuru Mungu nimetoka, ila sina hata shilingi mia.
Nimetoka nikiamini kuwa labda kwa jinsi mke wangu alivyonipambania atanirudia, namuomba msamaha nmuambie nimejifuzna naye ananiambia kuwa hata yeye amejifunza kuwa hakutakiwa kuolewa na mimi, ana amani na furaha. Kweli nilipotoka sina hata mia, ndugu niliokua nawaona wamaana hakuna hata mmoja alinihangaikia. Baada ya kuuza mali kipindi cha kesi, mtu pekee aliyebaki na mimi ni mke wangu.
Hakunitupa na kila wakati aliniambia kuwa mimi ni baba wa watoto wake na atapambana watoto wawe na baba asiye na doa, lakini amekataa kunisamehe. Kanipa mpaka mtaji wa kuanza maisha, lakini nikiwaza jinsi nilivyokua na biashara za mamilioni sasa, mimi naona biashara ya milioni 2 siwezi, na najikuta nachanganyikiwa. Natamani sana kurudi kwake na kutengeneza maisha ila sasa hataki kabisa hana mwanaume mwingine ila hanitaki, nimetoka Mahabusi na talaka ishatoka ana Maisha yake, kweli mke mzurihuja mara moja!