Yamenikuta naombeni ushauri, biashara yangu haiendi vizuri

Yamenikuta naombeni ushauri, biashara yangu haiendi vizuri

Usikate tamaa Jaribu kuchanganya na vitu ambavyo vinamzunguko mzuri
 
Biashara kwa sasa ina changamoto Sana. Kama uko sehemu yenye mchanganyiko wa watu changanya biashara unaweza ukatundika vitenge, kanga na viatu vya watoto au kuna zile ndala kama yeboyebo za wakubwa na watoto.
Kwel mkuu hapo umenena ni kujiongeza tu kwa sasa
 
Kwa uelewa wangu mdogo wa biashara, biashara ya stationery na nyumba ya kupanga ukiviweka karibu na university upatapa tu wateja. Fanya urafiki na maofisa wa serikalini kama unaweza kupata tenda ya kupeleka stationery ya vikao vya ofisi.
Daaah, hyo ya maofisini ni pasua kichwa kupita kiasi. HAWALIPI. Kuna hela naidai halmashauri fulani huu ni mwaka wa 4 sasa. Kila ukiuliza unapewa story za ajabu ajabu, kama fungu halijatoka na story kma izo. Na sasa hv hawachukui stationary hovyo hovyo kma zamani.
 
Na wanaweza wakachukua, ila ukubali kukopwa. Kwahyo kma mtaji wako ni mdogo inakuwa imekula kwako kwa sababu wakichukua sio wa kulipa leo au kesho.
 
Mkuu sijakuelewa wewe ni mjasiriamali au mfanyabiashara?
 
Habari wana JF wenzangu,

Mimi ni mjasiriamali takribani miaka kadhaa sasa, nafanya biashara ya stationaries na biashara zingine zinazolingana na hiyo hapo juu.

Lengo la kuandika Uzi huu ni kuomba ushauri kwa takribani miaka 3 hii ya karibuni biashara haifanyi vizuri mpaka imefikia point pesa za kulipa pango natoa kutoka vyanzo vingine vya pesa.

Kwa sasa nina mfanyakazi mmoja ila bado mambo yanazidi kuwa magumu siku hadi siku, kinachopatikana baada ya kutoa gharama kama vile umeme, mshahara wa mfanyakazi, pango, ulinzi ni kidogo sana na Mara nyingine hata faida hamna kabisa.

Naomba ushauri wenu nini niweze kufanya ili kujinasua na hili janga maana bado ni nia ya dhani ya kuendelea na biashara.

Fanya utafiti kwa nini mwanzo biashara ilikuwa nzuri na sasa inaporomoka. Je, vipi kuhusu ubora wa bidhaa zako wakati ule na sasa? Wateja wako hasa ni akina nani? Kama wateja wako hawafiki tena, je sababu ni nini? Je, sababu ni kukua kwa teknolojia ya mawasiliano, mfano, matumizi ya IPad? Je, umekuwa ukilipia kodi muda wote? Je, hizo bidhaa ulikuwa mwanzo unazipata kwa deal? Je, umepata competitors hapo jirani? Je, umebadilisha mfanyakazi? Je, customer service na care zipo vizuri?

Waulize wateja wanaofika hapo juu ya huduma unayotoa.

Niliwahi kwenda stationery moja nikaomba huduma ya kutoa nakala ya A3 (original) kwenda A4 (photocopy), wale wasichana wakaniambia haiwezekani wakati nikiangalia hile machine naona inaweza kabisa. Waliniambia niende umbali wa kilometa nane wakati ile document haikutakiwa nje ya ofisi kwa muda mrefu halafu tulikuwa tunaitaji markings zilizoongezewa ili niwe na nakala.

Niliomba nifanye mwenyewe, wakakubali, nikafanya copy kiulaini; halafu nikawaelekeza namna ya kufanya ile copying.

Jiulize maswali mengi iwezekanavyo kuhusu biashara yako, ila yasiwe yanayoendana na imani ya dini au mazingaombwe.
 
Usijilaumu sana. ni muda wa kujifunza kutokana na makosa, na ku-cut your losses.

funga biashara ufungue nyengine. uliyojifunza kwenye hii utumie kama darasa kwenye hiyo nyengine
 
Kama una photocopy machine na unafanya typing services, binding, scanning na bado huoni faida na pia umeshakaa hapo ofcn na hukuona wateja anza utafiti wa kuihamisha hiyo biashara.
 
Back
Top Bottom