Kwel mkuu hapo umenena ni kujiongeza tu kwa sasaBiashara kwa sasa ina changamoto Sana. Kama uko sehemu yenye mchanganyiko wa watu changanya biashara unaweza ukatundika vitenge, kanga na viatu vya watoto au kuna zile ndala kama yeboyebo za wakubwa na watoto.
Daaah, hyo ya maofisini ni pasua kichwa kupita kiasi. HAWALIPI. Kuna hela naidai halmashauri fulani huu ni mwaka wa 4 sasa. Kila ukiuliza unapewa story za ajabu ajabu, kama fungu halijatoka na story kma izo. Na sasa hv hawachukui stationary hovyo hovyo kma zamani.Kwa uelewa wangu mdogo wa biashara, biashara ya stationery na nyumba ya kupanga ukiviweka karibu na university upatapa tu wateja. Fanya urafiki na maofisa wa serikalini kama unaweza kupata tenda ya kupeleka stationery ya vikao vya ofisi.
Habari wana JF wenzangu,
Mimi ni mjasiriamali takribani miaka kadhaa sasa, nafanya biashara ya stationaries na biashara zingine zinazolingana na hiyo hapo juu.
Lengo la kuandika Uzi huu ni kuomba ushauri kwa takribani miaka 3 hii ya karibuni biashara haifanyi vizuri mpaka imefikia point pesa za kulipa pango natoa kutoka vyanzo vingine vya pesa.
Kwa sasa nina mfanyakazi mmoja ila bado mambo yanazidi kuwa magumu siku hadi siku, kinachopatikana baada ya kutoa gharama kama vile umeme, mshahara wa mfanyakazi, pango, ulinzi ni kidogo sana na Mara nyingine hata faida hamna kabisa.
Naomba ushauri wenu nini niweze kufanya ili kujinasua na hili janga maana bado ni nia ya dhani ya kuendelea na biashara.