Yamenishangaza St.Hellen Junior Kimara Mpigi

CURRENT ISSUE

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2013
Posts
256
Reaction score
57
Nimeshangazwa na utaratibu wa hawa wajasiriamali wenye shule za majina ya watakatifu.Watoto wameachwa stendi leo na gari ya shule ya St.Hellen kwa kile kinachodaiwa hawajamaliza ada ya shule.Nilipoona hivyo nilimuuliza dreva wa ile gari ya watoto kuwa kwa nini anawaacha,anasema ndivyo alivyoambiwa na boss wake.Imeniuma sana kwa sababu kuwaacha watoto kituoni kwa kosa la mzazi sio sawa.Uongozi wa shule ungetoa taarifa kwa wazazi husika kuwa leo wasiwalete watoto vituoni wataachwa.Kilichoniumiza ni kuwa;1.Huu uroho wa kupenda pesa bila kuthamini maisha ya watoto sio nzuri.2.Niliongea na mzazi ambaye mwanae naye amekutwa na dhahama hiyo,mzazi huyu alimwacha mtoto wake kituoni ambapo gari ya shule inawachukua akitegemea kuwa mtoto wake atachukuliwa kama kawaida,kumweleza kuwa mwanao yupo hapa kituoni ameachwa na gari ya shule alisikitika sana.Maana anasema hajawahi kupewa taarifa zozote na uongozi wa shule hata kama kuna deni hawezi acha kulipa ilikuwa ni taariifa tu.Ila kitendo walichokifanya cha kumwacha mtoto kituoni akishangaa shangaa ni kitendo kiovu na cha kukemewa na mamlaka husika.Mzazi huyu pamoja na mimi tumeanza zoezi la kutafuta shule yenye kuwajali watoto.Wadau naombeni msaada wenu.
 
Tupe ukweli juu ya kudaiwa ama kutodaiwa.
 
Ada imelipwa vizuri,na mtoto wangu hajaakutwa na hayo.Kilichoniuma ni kuwa huyu aliyeachwa ni mtoto wa jirani yangu ambaye mimi ndie niliyemtafutia hiyo shule.Hata kama kuna deni,sio kuwaacha watoto stendi kituoni.Maisha ya mtoto hayanunuliwi kwa pesa sh. 20,000/= ambayo hajamalizia.Hii ndio hoja yangu ya msingi
 
Nimekuelewa,
uongozi wa shule umekosea kutoa maelekezo kwa wenye magari kuwaacha vituoni wanafunzi wanaodaiwa bila kujali wamekwisha andaliwa kwenda shule. ilipaswa wawaeleze wazazi wanaodaiwa wasisumbuke kuwaandaa watoto mpaka wawe wamemaliza kulipa madeni yao yote.
ili kuepuka kadhia hii wazazi tujitahidi kuwa na kumbukumbu ya kulipa kwa muda stahiki ada za shule ama angalau kuwa na mawasiliano na uongozi wa shule tunapokuwa na mkwamo wa kiuchumi.

pia si vibaya kufikiria kutafuta shule nyingine ingawa hakuna shule isiyo na changamoto.
Kila la kheri.
 
Mwenye kujua shule nzuri ya Primary tafadhali nijuze ili niweze kumshauri mzazi yule kufanya maamuzi magumu,maana toka muda ule amekuwa akinitaka nimpe listi ya shule nzuri.
 
Nimeshangazwa na utaratibu wa hawa wajasiriamali wenye shule za majina ya watakatifu.Watoto wameachwa stendi leo na gari ya shule ya St.Hellen kwa kile kinachodaiwa hawajamaliza ada ya shule.Nilipoona hivyo nilimuuliza dreva wa ile gari ya watoto kuwa kwa nini anawaacha,anasema ndivyo alivyoambiwa na boss wake.Imeniuma sana kwa sababu kuwaacha watoto kituoni kwa kosa la mzazi sio sawa.Uongozi wa shule ungetoa taarifa kwa wazazi husika kuwa leo wasiwalete watoto vituoni wataachwa.Kilichoniumiza ni kuwa;1.Huu uroho wa kupenda pesa bila kuthamini maisha ya watoto sio nzuri.2.Niliongea na mzazi ambaye mwanae naye amekutwa na dhahama hiyo,mzazi huyu alimwacha mtoto wake kituoni ambapo gari ya shule inawachukua akitegemea kuwa mtoto wake atachukuliwa kama kawaida,kumweleza kuwa mwanao yupo hapa kituoni ameachwa na gari ya shule alisikitika sana.Maana anasema hajawahi kupewa taarifa zozote na uongozi wa shule hata kama kuna deni hawezi acha kulipa ilikuwa ni taariifa tu.Ila kitendo walichokifanya cha kumwacha mtoto kituoni akishangaa shangaa ni kitendo kiovu na cha kukemewa na mamlaka husika.Mzazi huyu pamoja na mimi tumeanza zoezi la kutafuta shule yenye kuwajali watoto.Wadau naombeni msaada wenu.

Ngoja basi ........ usilalamike sana huwezi jua huenda walishaandikiwa barua ikiwa ni pamoja na kuwaita wazazi ili wafike shuleni kunegotiate namna ya kuilipa hiyo ada na wazazi hawakuonyesha ushirikiano
Huwezi jua pia kwamba wazazi waliandikiwa barua ya tarehe ya mwisho ya kuliapa ada zao na kutaarifiwa kwamba ifikapo tarehe ya mwisho kama watakuwa hawajalipa ada basi wasiwatoe watoto majumbani mwao kwenda mashuleni kwasababu hakika hawatachukuliwa na gari la shule
SWALI LANGU KWAKO je kwa mzazi wa aina hiyo unadhani ni njia ipi nyepesi na rahisi ya kumfanya alipe karo ya mwanae mapema ili aendelee na shule?

ELIMU NI GHARAMA HAKUNA CHA BURE
 
Kimara Mpigi ndio wapi? Wewe kweli ni mwenyeji maeneo hayo au?. Ninavyojua Kimara na Mpigi ni mbalimbali ingawa kote ni wilaya ya Kinondoni. Poleni kwa kuachwa watoto!
 
Nimekuelewa,
uongozi wa shule umekosea kutoa maelekezo kwa wenye magari kuwaacha vituoni wanafunzi wanaodaiwa bila kujali wamekwisha andaliwa kwenda shule. ilipaswa wawaeleze wazazi wanaodaiwa wasisumbuke kuwaandaa watoto mpaka wawe wamemaliza kulipa madeni yao yote.
ili kuepuka kadhia hii wazazi tujitahidi kuwa na kumbukumbu ya kulipa kwa muda stahiki ada za shule ama angalau kuwa na mawasiliano na uongozi wa shule tunapokuwa na mkwamo wa kiuchumi.

pia si vibaya kufikiria kutafuta shule nyingine ingawa hakuna shule isiyo na changamoto.
Kila la kheri.

Umenena vyema mkuu ila hiyo conclusion ni option nzuri zaidi especially kumpeleka mtoto kwenye shule ambayo una uwezo nayo maana siku hizi imekuwa kawaida kila mtu anataka kumpeleka mtoto wake kwa shule za daddy na mammy. Nadhani ni bora kumpeleka tu kwenye shule zetu za kizalendo ambazo mwalimu ukimrudisha mtoto shule wazazi wanaandamana kwa kuwa ni shule ya serikali na mtoto hana makosa.

Kama ukimsimamia vizuri mtoto hata hizi shule za kizalendo mtoto atachomoka tu kwani mpaka tumefika hapa wazazi wetu walikuwa wanatusimamia kwa kuangalia maendeleo ya shuleni kila siku, lakini siku hizi baadhi yetu tumewakabidhi waalimu watufanyie kila kitu kwa watoto wetu na akirudi shule ni tution hakuna hata siku moja umeshika daftari lake na kujazia jazia mawili matatu ambayo unayajua
 
Mzazi mlee mwanao na umpe elimu nzuri kama uridhi wa maisha yake....Sidhani kama wenye shule ni vichaa kuwaacha watoto wadogo stendi.... wazazi tunakera ufuatiliaji wa watoto kwenye mambo ya elimu na hata ada na inafikia mahali hata wenye shule wanaghadhifika. Najua huyo jamaa yako anataka kumhamisha mwanae ili kuficha kosa la kutokuwajibika kwake. Sio vizuri kuwahamisha watoto shule kutokana na mambo ya kipuuzi kama haya kwani unampa mtoto ugeni wa waalimu na marafiki ktk shule mpya. Mwambie apunguze hasira na akubali uzembe wa kuchelewesha mpunga wa wenye shule.... Tena mwisho wa mwaka kama hivi wazazi wengi tunahamisha watoto shule ili kukimbia madeni.
 
Issue sio deni,kwani shule mpya si unaingia gharama mara mbili vile.Ni usumbufu wa kuja kupotelewa na motto kisa mwalimu.Aliyewaacha ni dreva aliyeelekezwa na mwalimu mhusika kufanya hivyo.Nami nimeuona huo uzembe,leo hii nimewasiliana na shule moja inaitwa MARTIN LUTHER iliyopo Dodoma,naombeni kwa wenye taarifa zaidi za shule hii wanijuze.Maana huu uzembe wa staili hii ya hawa Watakatifu(ST.)umenichosha.
 
Naona una yako mkuu..... all the best ktk kumpenda mwanao.
 
Back
Top Bottom