CURRENT ISSUE
JF-Expert Member
- Jun 20, 2013
- 256
- 57
Nimeshangazwa na utaratibu wa hawa wajasiriamali wenye shule za majina ya watakatifu.Watoto wameachwa stendi leo na gari ya shule ya St.Hellen kwa kile kinachodaiwa hawajamaliza ada ya shule.Nilipoona hivyo nilimuuliza dreva wa ile gari ya watoto kuwa kwa nini anawaacha,anasema ndivyo alivyoambiwa na boss wake.Imeniuma sana kwa sababu kuwaacha watoto kituoni kwa kosa la mzazi sio sawa.Uongozi wa shule ungetoa taarifa kwa wazazi husika kuwa leo wasiwalete watoto vituoni wataachwa.Kilichoniumiza ni kuwa;1.Huu uroho wa kupenda pesa bila kuthamini maisha ya watoto sio nzuri.2.Niliongea na mzazi ambaye mwanae naye amekutwa na dhahama hiyo,mzazi huyu alimwacha mtoto wake kituoni ambapo gari ya shule inawachukua akitegemea kuwa mtoto wake atachukuliwa kama kawaida,kumweleza kuwa mwanao yupo hapa kituoni ameachwa na gari ya shule alisikitika sana.Maana anasema hajawahi kupewa taarifa zozote na uongozi wa shule hata kama kuna deni hawezi acha kulipa ilikuwa ni taariifa tu.Ila kitendo walichokifanya cha kumwacha mtoto kituoni akishangaa shangaa ni kitendo kiovu na cha kukemewa na mamlaka husika.Mzazi huyu pamoja na mimi tumeanza zoezi la kutafuta shule yenye kuwajali watoto.Wadau naombeni msaada wenu.