Yametimia sasa kiswahili hadi ............. Phd

stevelwa

Member
Joined
Nov 2, 2012
Posts
72
Reaction score
20
Katika hali ambayo inaleta matumaini makubwa kwa wapenzi wa lugha ya Kiswahili, taarifa wkamba Dkt. Metho Samweli amefanikiwa kuandika thesis yake ya PhD ya somo la Kiswahili kwa lugha ya Kiswahili ni za kusisimua.
Kwa mujibu wa gazeti la THE HILL OBSERVER la Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Method Samweli amekuwa mhitimu wa kwanza wa Chuo hicho kuandika Thesis ya PhD kwa lugha ya Kiswahili. The Hill Observer limeeeleza kuwa kwa muda mrefu sana wahitimu wote walikuwa wakiandika thesis zao lwa lugha ya kiingereza.
Lakini Dk Method Samweli mwenye miaka 32 ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (UDSM-DUCE) ametunukiwa PhD hivi karibuni wakati wa sherehe za 42 zilizofanyika kwenye ukumbi wa MCCC (Mlimani City Conference Center).
Mkuu wa Idaya ta fasihi, Mawasiliano na Uchapishaji katika Idara ya Kiswahili ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, Dk. Shani Omari alisema kuwa kabla ya thesis ya Dk method Samweli, hapakuwahi kutokea Thesis yoyote iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili Chuoni hapo.
Aidha, Chuo Kikuu cha Dar es salaam kinafuata nyayo za Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambacho tayari wapo wanafunzi kadhaa walioandika thesis zao lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa wahitimu wa PhD waliofanikiwa kuandika Thesis zao kwa lugha ya kiswahili, ni Mohamed Seif Khatibu ambaye ni waziri mwandamizi na kiongozi wa siku nyingi ndani ya CCM.

WASIFU WA DK. METHOD SAMWELI
Alijiunga sekondari ya Ndanda, kisha akajiunga na UDSM mwaka 2002 hadi mwaka 2006 alipomaliza masomo yake ya B.A with Education na kuwa mhadhiri msaidizi wa UDSM-DUCE. Kati ya mwaka 2006 na 2008 alimaliza masters katika masomo ya Linguistic hapo hapo UDSM.

Chanzo ni: blogu ya lundunyasa na simu toka kwa shuhuda wangu pale Udsm.
 
Afadhali hilo jambo linaweza kututoa kimasomaso kwenye hii lugha maana uzoefu unaonesha lugha ya kiingereza ni tatizo hata kwa wanafunzi wa elimu ambao hawana usuli wa shule zinazotumia lugha ya kiingereza kama ya kufundishia, binafsi ninachoamini sasa mitindo ya kukariri na kunakiri kidogo itapungua hadi kufikia uvumbuzi wa hali ya juu. hakuna taifa liliendelea kwa kutumia lugha isio ya kwao katika nyanja ya elimu. rejea china, japan, india, nk.
 
Back
Top Bottom