Balozi wa Marekani Burkina Faso, Joann Lockard, ameomba kuonana na Captn. Traore, ila Captn akamjibu ana shughuli nyingi na akamtuma Waziri wake wa Mambo ya nje,mwezi huu.
Utakumbuka nimeripoti hapa kuwa baada ya Trump kuwapiga marufuku raia wa Mali, Niger na Burkina Faso (sawa na wetu wa Tanzania), kwa dharau na ujeuri tu; waume hawakukawia. Siku ifuatayo nchi hizo zikawapiga marufuku raia wa Marekani kuingia nchini mwao, katika kile kinachojulikana katika itifaki za kidiplomasia kama 'mutual reciprocity'- ukinitenda nakutenda!
Kwa kirefu zaidi, uhusiano wa Marekani na Burkina Faso ulianza kuzorota tangu kuja kwa Capt. madarakani Octoka 2022 na kubadilisha uhusiano wa kitumwa na Wazungu. Akaanza kwa kuwatimua Wanajeshi wa Kifaransa, kisha akafuatia na kununua migodi iliyokuwa katika mikono ya hawa. Hapo hapo akaifanya mali ya taifa, akanunua zana kubwa za kuchimbia akawapa wananchi wachimbe, kisha akajenga mtambo wa kusafisha dhahabu. Hii leo dhahahabu inachimbwa, inasafishwa na kuuzwa na Waburkina, kwa bei ya Soko la Kimataifa.
Lakini chuki zaidi ya Marekani ilipanda baada ya kijana kuwakaribisha Warusi wamsaidie kupambana na makundi yaliyoundwa na Wazungu ili kuiweka Burkina Faso katika matatizo huku wao wakisomba dhahabu!
Capt. aliwaudhi zaidi kwa kuichagua Iran, na si Wazungu, kwa kujenga mji wake mkuu mpya, na pia kwa kuifundisha maarifa ya kuunda drones. Hayo ni makosa yasiosamehewa na Mabeberu.
Michael Langley, aliyekuwa Mkuu wa majeshi ya Marekani Afrika, naye akamwudhi Capt. kwa kumsingizia kuwa ni mla rushwa na mtoroshaki wa dhahabu, kwa chuki tu iliyojengeka kwa niliyoyasema. Hii ni dhambi ambayo Traore haisamehi. Huyu ni mwanamapinduzi ambaye tangu kushika cheo hakukubali kupandishiwa mshahara, na hadi sasa anakula mshahara wa cheo chake cha Capteni- hata cheo hakujipandisha!
Kisa cha leo ni kuwa Balozi huyo wa Marekani nchini humo hatimaye amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso, kwa maombi yake. Moja ya yaliyozungumziwa ni hilo la kuondoa marufuku kwa raia wa Burkina Faso kuzuru Marekani! Waona? Haya, mfikishieni 'Who are you?'