Yamoto band mnakera sana

tamimusalim

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2014
Posts
1,822
Reaction score
498
Napenda kumwambia kamanda Kova na kikosi chake, kumwambia mmiliki wa Yamoto band "Mkubwa na wanawe" Said Fela kufunga vifaa maalum vya kuzuia sauti au kutafuta sehemu nyingine ya kufanyia mazoezi ya bendi yake hiyo.

Sababu pale anapofanyia mazoezi hayo ni katikati ya mtaa, hivyo kusababisha usumbufu wa makelele, pia inawaathiri watoto wetu kutokwenda shule kwenda kutazama mazoezi ya bendi yake iyo. Tulijaribu kumwambia na barua kumtumia, nadhani amekaidi hilo, hivyo Kova saidia hili mikelele imezidi watu hatulaliii! Mweee!
 
kamanda kova come this way!!!!
 
Nilidhani tatizo hilo linamalizwa na watendaji tu... maana liko under local governance
 
Nilidhani tatizo hilo linamalizwa na watendaji tu... maana liko under local governance

Unaweza kuta aaid dela na yamoto wanakunywa chai ikulu kila wiki na mshkaji wao. Sasa local gov ina nguvu tena hapo?
 
Wasilisha malalamiko yako serikali ya mitaa utasikilizwa bila shida
 
Muandie katika ukurasa wake wa Instagram_ mkubwa Fella, na mimi nitamuandikia. Aache uhuni
 
Unaweza kuta aaid dela na yamoto wanakunywa chai ikulu kila wiki na mshkaji wao. Sasa local gov ina nguvu tena hapo?

acha hizo wewe, wanakunywa chai kila siku?? mbona hata Ray C na liyumba walikunywa chai ikulu, wako wapi sasa

tusiwape mibichwa wale madogo

if we want them to stop, it can be done... wananchi wana mfumo wa kuwafanya waseme hapana
 
Safiii sana great thinker
 
Fuateni taratibu tu..mkiwa madhubuti ata awe nani mtashinda tu.
 
Na nyie matajiri mnasumbuliwa na kelele za uswahilini? Mi nilidhani unaishi Masaki mkuu.
 
Basi nijuavyo watoto hayo maeneo hawaendi shule, kisa na wao wanataka kuwa Kama yamoto band...kazi kwelikweli
 
Ila jamani tuongee ukweli,hawa madogo wana vipaji! Kinachotakiwa wawe chini ya uangalizi wa wazazi na jamii wasije jiingiza kwenye tabia mbaya, vinginevyo wanaweza iletea heshima nchi yetu kama diamond ...
 
Daaah ni noma aisee ni mitaa gani hiyo?nijuavyo mimi ushwahirini ndio huwa kuna huo upumbavu.
 
Njoo ukae masaki uepukane na kero za yamoto band..
 
Basi nijuavyo watoto hayo maeneo hawaendi shule, kisa na wao wanataka kuwa Kama yamoto band...kazi kwelikweli

ha ha ha ha ha ha haaaa daaaah hii nayo kali,ni kweli lakini vijana wanavyohangaika kutoka mweeeh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…