Yamoto Band: Watatu mambo yao safi; nini tatizo kwa Enock Bella?

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370


Baada ya kuvunjika kwa kundi la Yamoto band, kila msanii wa kundi hilo alianza kufanya kazi kivyake.

1. Aslay alianza kutoa nyimbo moja baada ya nyingine kila baada ya muda mchache bampa to bampa na karibia zote zikafanya poa na hadi sasa ana hit na ngoma ya Subalkheri

2. Beka flavour nae akatoa nyimbo zake nzuri tu kama Libebe, Sikinai na sasa katoa Kiben ten.. Kwa ufupi nae anafanya poa tu kwenye game.

3. Maromboso ambae sasa tunamwita mboso alikaa muda mrefu tukajua kapotea mazima ila akapata bahati ya kujiunga label maarufu nchini ya wasafi. Hii label ina nguvu imemfanya nae arudi kwenye level nzuri.

4. Enock Bella ndio bado anatupa sintofahamu juu ya kazi zake za muziki. Licha ya kutoa ngoma kama nitazoea nado hazija-hit na zinachuja fasta.

NINI HATMA YA ENOCK BELLA? JE, AFANYE NINI ARUDI KWA KISHINDO KWENYE GAME?!
 
Labda bado masikio ya watanzania hayajaelewa kile akifanyacho

Ameachia wimbo mwengine Jana
 
Mbona hata huyo Mboso sioni kama nyimbo zake zinabamba sana kama Aslay na Beka?

Hivi kweli Diamond alimuamini huyo Dogo kuliko aslay? au aliingia wasafi kwa influence ya Mkubwa fella
 
Mwisho wanakosa kitu mfukoni, lawama kwa CMG kuwa wamempa stress, then anaanza kula vumbi kama nyoka...
Btw, sijui miye ndo sijui kufananisha? Naona kama kafanana sura na Harmonize!
 
Dogo na sauti yake nzito ile anapendeza kufanya kazi na bendi vilevile kama ilivyokuwa. Akichomekea vionjo vyake vile alikuwa anaburudisha mno, ila kusimama kama solo anahitaji ubunifu wa hali ya juu sana japo ukweli unabaki kuwa ni mzuri tu.
 
Madogo cjawah kuwaelewa kbsa wanachoimba tang ya moto
Band ivunjike
 
Mbona hata huyo Mboso sioni kama nyimbo zake zinabamba sana kama Aslay na Beka?

Hivi kweli Diamond alimuamini huyo Dogo kuliko aslay? au aliingia wasafi kwa influence ya Mkubwa fella

Aslay ameshamaliza mziki wake...Wenye nafasi ya kuendelea kushain ni Beka na Mbosso..Muziki ni mipango sio ujuzi pekee. Waelewa wa muziki wananisoma nachomaanisha.
 
Aslay ameshamaliza mziki wake...Wenye nafasi ya kuendelea kushain ni Beka na Mbosso..Muziki ni mipango sio ujuzi pekee. Waelewa wa muziki wananisoma nachomaanisha.
Huyo Mbosso hakuna kitu, promo na nguvu nyingi lakini hakuna kitu !

- Wajuvi Yamoto Band ni Beka na Aslay tu !
 
Mi kwa mtazamo wangu ule wimbo alioutoa wa kwanza 'Sauda' ni mzuri kuliko nyimbo zote za Mbosso alizoachia, sema kakosa promo na watu walishamtabiria kufeli kabla hata hajatoa nyimbo[emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…