Yanasemwa mengi juu ya ajira za Sensa, nami niseme machache

Yanasemwa mengi juu ya ajira za Sensa, nami niseme machache

Kikitumika kigezo hiki cha hesabu, wataenguliwa wengi sana kwenye hii kitu maana wengi walikimbia na alerg na hesabu/takwimu [emoji3]
Kkkkk kweli yaani MTU ana 'F' ya hesabu halafu anaomba KAZI ya takwimu??!! Huyo hayupo serious.
 
Kuna Mambo matano mtumishi wa umma ukiyafanyia mchezo yanaathiri moja kwa moja utumishi wako na yapo kwenye sheria ambayo ni mitihani ya Taifa,Sensa,uchaguzi mkuu,mwenge na msafara wa Rais
 
Kuna wanaosema ajira hizi za sensa wapewe ambao ni watumishi ili kudhibiti uzembe utakaojitokeza na wengine wanadai wapewe ambao hawana ajira ili walau wapate mitaji.

Makundi yote ukiwasoma katikati ya mstari wana hoja zenye mashiko lakini kuna sehemu nakubaliana kutokukubaliana.

Kundi la kwanza ambao wanadai watumishi waangaliwe zaidi wamesahau Jambo moja. Ajira hizi za sensa hazina uhusiano kabisa na ajira nyingine mtu aliyonayo, kwamba muajiriwa wa TRA aliyeomba nafasi za sensa za NBS aadhibiwe na TRA kwa uzembe atakaofanyia NBS? Hapa inakosekana logic kabisa

Ninachojua kila ajira kuna utaratibu wake wa kinidhamu na hivyo ajira za sensa zina utaratibu wake uliowekwa na NBS na mtu anapoonyesha utovu wa nidhabu ni NBS wanatakiwa kumuwajibisha pekee kwa kosa la ajira ya sensa na si nyingineyo aliyonayo kutoka mamlaka nyingine.

Tukija kwa kundi la pili, hawa wanadai wasio na ajira wafikiriwe kwanza. Kwa kundi hili Nina haya machache, ajira zinapotolewa zinaangalia uwezo wa mtu, katika walioomba sensa na wasio na ajira kuna watu Wana Elimu ya kidato Cha nne tu lakini kuna mwenye ajira na kaomba sensa ana Elimu ya chuo kikuu. Hawa ni watu wawili tofauti, wa kidato Cha nne reasoning yake ipo chini kuliko wa chuo kikuu. Elimu inasaidia kufikirisha ubongo na kutoa maamuzi yenye busara. Madhara ya kutumia vijana wa form 4 ni mengi na ushahidi ninao wa kilichotokea kwenye zoezi la ANUANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI kwenye Halmashauri fulani.

Maoni yangu

i) Kusiwepo na upendeleo wa aina yoyote ile kwenye kazi hii ya sensa, ama mtu ana vigezo vyote achukuliwe yeye bila kujali ni mtumishi au hana ajira. Upendeleo ndio hupelekea kupatikana wasio na sifa wakafanya vituko.

ii) Wote watakaofanikiwa kupata ajira wale viapo vya uaminifu na uadilifu kwa zoezi zima na viapo hivyo viwe vinaweza kumshtaki mtu na kumtia hatiani.

iii) Yawepo makubaliano maalumu kwamba muombaji alipwe baada ya kazi kukamilika na baada ya uhakiki wa kazi ya mtu. Kwa Sababu ni zoezi la kidigitali naamini uhakiki utakuwa wa haraka na yakibainika makosa yoyote akatwe sehemu fulani ya malipo yake. Hii itadhibiti kufanya kazi hovyo. Na pia naamini kunaweza kufanywa hujuma ili kulipa pungufu na hela kupigwa.

iv) Kwa sababu zoezi hili litakuwa na wasimamizi kigezo Cha kusema watumishi wa eneo husika wanayajua maeneo yao ndio wapewe sio sawa. Usimamizi na ufuatiliaji ukiwepo mzuri hata mtu akiletwa kutoka Burundi ahesabu watu wa manzese hatoshindwa. Kigezo Cha kujua eneo kwa kuishi eneo sio sawa kwa Sababu kuna wengi Sana wapo eneo hilohilo kwa miaka 15 lakini hajui mipaka ya mtaa wake.

Mwisho,

Kuna kikundi Cha watu kinataka kuhalalisha umuhimu wako kwa zoezi hili ili wengine wasipewe, kikundi hicho ni hatari Sana. Sifa na vigezo Kama mtu anavyo apewe.
Mtazamo wako kwenye kipengere cha Ushauri si mbaya ila elimu ya chuo kikuu haitoshi katika "judging and reasoning" inategemea na mtu mwenyewe ana utashi kiasi gani, ndiyo maana elimu ya chuo kikuu inahitaji neno uzoefu ili kuleta weledi zaidi.
 
Sasa anwani nyumba na makazi walizingatia vigezo au ilikuwa ni mchongo ule ? Viongozi walichukua ndugu zao ndo wakawekwa kwenye vitengo.

Ushauri wangu wasio na ajira wapewe kipaumbele .

Ninachoisihi serikali kwenye usaili ihakikishe mhusika anadahiliwa kweli kweli .
 
Mwalimu mwenye F ya hesabu anayefundisha Kichakoro primary school na ana mwaka wa 10 hapo akitokea mkoa mwingine, anamzidi graduate wa takwimu ambae ni mzawa asiye na ajira?
 
Sasa anwani nyumba na makazi walizingatia vigezo au ilikuwa ni mchongo ule ? Viongozi walichukua ndugu zao ndo wakawekwa kwenye vitengo.

Ushauri wangu wasio na ajira wapewe kipaumbele .

Ninachoisihu serikali kwenye usaili ihakikishe mhusika anadahiliwa kweli kweli .

Ubaya ni kwamba kuna wenye ajira wameandika hawana ajira [emoji23][emoji23]Tz bhana
 
Connection Imerasimishwa siku hizi mkuu,Anaweza kuchukuliwa hata std7...Muhimu uwe na mjomba tu huko.
 
Swala hili linafikirisha. Ukimpa asiye na ajira ni huwezi kumwajibisha baadae hata akiboronga tofauti na kada zenye kuheshimu utawala kama kada ya ualimu
Naheshimu mawazo yako lakini sidhani kama yapo sahihi uwajibishwaji wa mfanyakazi unatokana na Sheria na taratibu za kimkataba baina ya pande mbili sababu huwezi wajibishwa kwa kosa ambalo limefanyika katika sehemu nyingine Sheria ya kazi haipo hiyo jaribu kupitia labor laws act ya mwaka 2004 utapata madini mengi
 
Back
Top Bottom