Yanasemwa mengi juu ya ajira za Sensa, nami niseme machache

Kikitumika kigezo hiki cha hesabu, wataenguliwa wengi sana kwenye hii kitu maana wengi walikimbia na alerg na hesabu/takwimu [emoji3]
Kkkkk kweli yaani MTU ana 'F' ya hesabu halafu anaomba KAZI ya takwimu??!! Huyo hayupo serious.
 
Kuna Mambo matano mtumishi wa umma ukiyafanyia mchezo yanaathiri moja kwa moja utumishi wako na yapo kwenye sheria ambayo ni mitihani ya Taifa,Sensa,uchaguzi mkuu,mwenge na msafara wa Rais
 
Mtazamo wako kwenye kipengere cha Ushauri si mbaya ila elimu ya chuo kikuu haitoshi katika "judging and reasoning" inategemea na mtu mwenyewe ana utashi kiasi gani, ndiyo maana elimu ya chuo kikuu inahitaji neno uzoefu ili kuleta weledi zaidi.
 
Sasa anwani nyumba na makazi walizingatia vigezo au ilikuwa ni mchongo ule ? Viongozi walichukua ndugu zao ndo wakawekwa kwenye vitengo.

Ushauri wangu wasio na ajira wapewe kipaumbele .

Ninachoisihi serikali kwenye usaili ihakikishe mhusika anadahiliwa kweli kweli .
 
Mwalimu mwenye F ya hesabu anayefundisha Kichakoro primary school na ana mwaka wa 10 hapo akitokea mkoa mwingine, anamzidi graduate wa takwimu ambae ni mzawa asiye na ajira?
 

Ubaya ni kwamba kuna wenye ajira wameandika hawana ajira [emoji23][emoji23]Tz bhana
 
Connection Imerasimishwa siku hizi mkuu,Anaweza kuchukuliwa hata std7...Muhimu uwe na mjomba tu huko.
 
Swala hili linafikirisha. Ukimpa asiye na ajira ni huwezi kumwajibisha baadae hata akiboronga tofauti na kada zenye kuheshimu utawala kama kada ya ualimu
Naheshimu mawazo yako lakini sidhani kama yapo sahihi uwajibishwaji wa mfanyakazi unatokana na Sheria na taratibu za kimkataba baina ya pande mbili sababu huwezi wajibishwa kwa kosa ambalo limefanyika katika sehemu nyingine Sheria ya kazi haipo hiyo jaribu kupitia labor laws act ya mwaka 2004 utapata madini mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…