Yanayo tufanya tuwe waswahili...

Yanayo tufanya tuwe waswahili...

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
YANAYO TUFANYA TUWE WASWAHILI...

1.Unawasalimia watu usiowajuwa na kutaka

urafiki na kila anayetaka kuzungumza na wewe,

halafu unaanza kumwita mtu huyo(usiyemjuwa

undani wake wala tabia zake)aunt au anco!.



2.Asilimia 90 ya CD pamoja na cassete za

muziki ulizonazo nyumbani ni feki (sio original

copies).



3.Stoo yako imejaa vitu (makorokoro) kwa

kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku

utayahitaji kwa mfano karpet ukilitoa hulitupi n.k.



4.Una machupa ya maji matupu na ya shampoo,

chupa za perfume pamoja na vipodozi vingine

umeweka tuu kwenye rafu au meza yako wala

huna shughuli navyo.



5. Watoto wako wote wana majina ya utani

mfano babu ali,chidi,mamu, dida, kibabu, n.k.



6. Hakuna mtu katika familia yako anayetoa

taarifa kwako anapo kuja kukutembelea,

wanajileta tu, hata hawatazami idadi ya watu

wanaokuja wala kufikiria watalala wapi!




7.Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya

kusafishia meno,tissue n.k ulivyochukua

sehemu kama vile mgahawani (Restaurant).



8. Mama yako anamigogoro na ndugu na

hawazungumzi kwa muda wa siku 10 au zaidi.



9.Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao

gharama za kupiga ni nafuu(mfano usiku sana

)na mara nyingi huwa una beep tu hutaki kujitia

hasara hata kama wewe ndiye uliye na haja

hiyo.



10.Ulipokua mdogo nguo unazonunuliwa pamoja

na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa

muda mrefu zaidi.



11.Wakati ukisafiri na ndege unabeba mzigo wa

uzito mkubwa kuliko inavyoruhusiwa, kwa kuwa

unataka kumridhisha kila mtu kwa zawadi huko

unakokwenda.


12.Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi

utakuwa unapita na huku unasema kama sio

mimi asingekuwa vile yule.


13. Wale tunaowasaidia wengi wanakosa

shukurani na badala yake wanasema, eti

kaniletea kijisimu hiki, si hata hapa ningeweza

kukipata? Ndio, zawadi ya Ulaya hii?! Halafu

wanacheka!


14. Hatuvai nguo nzuri au mpya na kujipamba

tunapokuwa majumbani mwetu isipokuwa

tunapokwenda maharusini, khitma au kwenye

mialiko ya futari au pale tunapoalikwa vyakula

na marafiki!


NOTE: Basi wapelekee waswahili wengine ili

wajuwe ni kitu gani kinawafanya wao wawe

Waswahili... ......... ......... ..... kama mimi na wewe


,
lakini si wakati umefika wa kubadilisha khulka

hizi, zilizopitiwa na wakati? (out dated

traditions and customs)!!?....mmh?



Cheers



|
.
serv
 
mambo yo ya kwanza mpaka ya mwish ni vichekesho vyote.. hahahahaahha lol... mzizi mkavu....
 
Back
Top Bottom