Yanayoendelea Jijini Mbeya uzinduzi wa Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini ya Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
8,586
Reaction score
11,227
Ikiwa ni Mwisho wa mgogoro kati ya pande mbili zinazohitalifiana. Leo Jijini Mbeya wafuasi wa Askofu Mwaikali wanafurahia kujiunga na mwamvuli wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki wakitokea K.K.K.T.

Ni huzuni kubwa kujitenga na kanisa hilo kongwe lililoasisiwa mwaka 1963 baada ya kuunganisha dayosisi saba za wakati huo, lakini hakuna namna zaidi ya kufanya hivyo kwani wakubwa wa kanisa ndio waliotufikisha hapa.
 
Video inagoma kuatach
 
Mmeamua kuhama na jina kabisa? Kazi ya Mungu iendelee.
 
Wakubwa wamezuia kupiga picha? Na lipo sehemu gani ya jiji?
 
Hilo jina limepata usajili hapa??

Kwa maana huwezi ukaanzisha kanisa jipya kwa jina ambalo tayari lipo.

Ni kuwachanganya waumini.

Kwanini kwa busara tu msitafute jina jingine??

Maana huko ni kuendeleza migogoro wakati lengo ni kutoa huduma ya kiroho.
 
Kanisa kongwe mwaka 1963??? [emoji3]
 
Hilo jina halipo ndio jipya,jina lililopo ni Dayosisi ya Konde.
 
Sijakuelewa mkuu, walutheri wanajiunga na walutheri?
 
Haya anzeni kuwapelekea sadaka
Sasa

Ova
 
Ni tofauti mkuu. Kuna kanisa la kiinjili la kirutheri Tanzania, kuna kanisa la kirutheri la Africa mashariki yote yalikuwepo Tanzania
 
Siku hizi madhehebu karibu yote duniani viongozi wake wakianza kugombea fedha na mali zilizopatikana ndani ya madhehebu hayo hutokea mafarakano. Hekima inayotumika ni kugawanyika vipandevipande, mifano ipo mingi. Any way wote wanabaki kuwa wakristo na kazi ya kumhubiri Yesu kristo inaendelea kupitia mitafarakano hiyo. Ni kawaida kutawanyika kuliko kurundikana mahala pamoja kwa mafundisho yaleyale miaka nenda rudi.
 
Msizunguke saana lengo la hilo kanisa n kukusanya SADAKA

WATUMISHI WA MAKANISA MTAJI WAO N MDOMO.TU BAAASI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…