Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Watu wa Soka,
Timu yetu Singida Big Stars imeweka kambi hapa Njiro jijini Arusha kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23.
Tulichagua kuweka kambi (Pre season camp) hapa Arusha kutokana na sababu kadhaa ikiwemo hali ya hewa nzuri na mazingira yenye utulivu katika mitaa hii ya Njiro. Pia kukimbizana na muda na kuwa na maandalizi ya uhakika ikizingatiwa tumefanya usajili wa wachezaji wapya ambao wanahitaji muda wa kutosha kuweza kuunganika na wachezaji wetu waliomo kikosini tangu msimu wa Championship. Hakika ulikuwa ni uamuzi sahihi!
Wapenzi na mashabiki wetu na wadau wote wa soka kwa ujumla, kupitia uzi huu mtapata kufahamu mambo yanayoendelea na updates zote muhimu kuhusu timu katika kipindi chote tutakachokuwepo hapa kambini jijini Arusha.