Yanayoendelea kwenye kambi ya Singida Big Stars jijini Arusha (Pre-season Camp)

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Watu wa Soka,

Timu yetu Singida Big Stars imeweka kambi hapa Njiro jijini Arusha kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23.

Tulichagua kuweka kambi (Pre season camp) hapa Arusha kutokana na sababu kadhaa ikiwemo hali ya hewa nzuri na mazingira yenye utulivu katika mitaa hii ya Njiro. Pia kukimbizana na muda na kuwa na maandalizi ya uhakika ikizingatiwa tumefanya usajili wa wachezaji wapya ambao wanahitaji muda wa kutosha kuweza kuunganika na wachezaji wetu waliomo kikosini tangu msimu wa Championship. Hakika ulikuwa ni uamuzi sahihi!

Wapenzi na mashabiki wetu na wadau wote wa soka kwa ujumla, kupitia uzi huu mtapata kufahamu mambo yanayoendelea na updates zote muhimu kuhusu timu katika kipindi chote tutakachokuwepo hapa kambini jijini Arusha.
 
DAY 1

Siku ya kwanza kambini timu ilipata wasaa wa kufika kwenye uwanja wa mazoezi na kuanza ratiba bila kuchelewa.
 

Attachments

  • IMG_6202.jpg
    2.2 MB · Views: 8
  • IMG_6196.jpg
    2.3 MB · Views: 8
  • IMG_6204.jpg
    1.7 MB · Views: 7
DAY 1

Siku ya kwanza kambini timu ilipata wasaa wa kufika kwenye uwanja wa mazoezi na kuanza ratiba bila kuchelewa.

Kama kuna mwamba umemuona unayemkubali mtaje na useme neno moja kwake, atasoma hapa!
 

Attachments

  • IMG_6186.jpg
    2.1 MB · Views: 6
  • IMG_6190.jpg
    2 MB · Views: 5
  • IMG_6192.jpg
    2.3 MB · Views: 6
  • IMG_6205.jpg
    1.9 MB · Views: 6
  • IMG_6211.jpg
    2.3 MB · Views: 5
  • IMG_6224.jpg
    2.4 MB · Views: 6
Mbona wana furaha sana! Mnawapa nini wachezaji wenu? Hongereni sana.
 
Kufanya vizuri kwenye ligi kuu na michuano yote tutakayoshiriki mkuu. More specifically tunatarget top 4 kwenye Ligi na inshaallah tutafanikiwa.
Kufanya vizuri kwa maana ipi? KUTARGET TOP 4 SIO KAZI RAHISI, MMEFANYA MIKAKATI IPI KUHAKIKISHA MNAIPATA TOP 4?
 
Baada ya Kyomo kuwakimbia mmemchukua striker gani kama mbadala wa kuziba hilo pengo lake
 
Kufanya vizuri kwa maana ipi? KUTARGET TOP 4 SIO KAZI RAHISI, MMEFANYA MIKAKATI IPI KUHAKIKISHA MNAIPATA TOP 4?

Mikakati ni usajili na maboresho yanayoendelea kwenye klabu. Tunafahamu kuna ushindani kwenye ligi, ndio maana tuko kambini kujiandaa vizuri na panapo majaliwa tutafikia malengo.
 
Mikakati ni usajili na maboresho yanayoendelea kwenye klabu. Tunafahamu kuna ushindani kwenye ligi, ndio maana tuko kambini kujiandaa vizuri na panapo majaliwa tutafikia malengo.
Je, usajili wa masalia una manufaa kwenu? Yaani wachezaji walikuwa wanasugua benchi timu walizoachwa ndio mje kuwatumia kupata ubingwa?
 
Baada ya Kyomo kuwakimbia mmemchukua striker gani kama mbadala wa kuziba hilo pengo lake

Asante mkuu. Labda nifafanue hivi:

1. Kyombo hajatukimbia, ametumia haki yake kwa mujibu wa mkataba. Hatuna tatizo nae.
2. Kyombo hakuwa chaguo pekee, tumefanya usajili madhubuti kwenye safu ya ushambuliaji. Wapo wengi wazuri zaidi na tutawatambulisha kabla dirisha la usajili halijafungwa.
 
Welldone mkuu, kwangu it make sense kabisa kuwa na kambi ndani ya nchi, why ukafanye mazoezi ughaibuni na kesho mnakuja kucheza game kwenye uwanja kama mkwakwani au majimaji au sokoine (viwanja vyote hivi vinafaa to train horses sio kucheza mpira wa miguu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…