Yanayofanyika Chato yanafanyika kote Nchini Tanzania

Yanayofanyika Chato yanafanyika kote Nchini Tanzania

Unalinganisha kijiji cha chatu na miji mikubwa kama Dar, mbeya, Mwanza, Arusha nk, rudi ukafanye homework yako vizuri....
Hivi una ufahamu wa kuweza kutofautisha jiji na kijiji/tarafa?
 
Hivi una ufahamu wa kuweza kutofautisha jiji na kijiji/tarafa?
Hadhi ya chato ilinganishwe na vijiji vingine, siyo miji mikubwa na majiji....ndo maana butiama haijawahi kulinganishwa hadhi hata na Musoma hadi kujengwe makao makuu ya kanda na hospitali ya rufaa.
 
Bado mradi gani mpya ambao unahisi unatakiwa kuwepo Chato?
 
Mkuu,

Umejaribu kuelezea uwiano wa maendeleo vitu nchini Tanzania kwa sasa kwamba kinachofanyika wilayani Chato mkoani Geita ndicho kinachofanyika maeneo mengine Tanzania kwa sawiia lakini maelezo hajathibitisho kwa kuonesha angalu kwa mikoa kumi na tano tu 0ambayo haiko karibu karibu kwamba hicho unachotaka kuaminisha jukwaa hili ni kweli

1. Enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Burito alipokuwa mapumzikoni Butiama au Msasani mara kadhaa shughuli za serikali alizifanyia ikulu ndogo ya Mwanza (Capri point Mwanza), Musoma mjini na nyumbani kwao Mwitongo, Butiama;
2. Enzi Mwalimu Ali Hassan Mwinyi mapumzikoni alionekana ama Unguja Zanzibar, Jijiji Dar Es Salaam, Mikocheni au Temeke lakini shughuli za serikali alizifanyia ikulu ya Magogoni Dar Es Salaam;
3. Enzi za mwanadiplomasia na mwanahabari Benjamini William Mkapa alipokuwa mapumzikoni alionekana ama Moshi, Lushoto,Tanga na Lupaso, Masasi Mtwara na kufanyia shughuli za serikali ikulu ya Magogoni, Dar Es Salaam;
4. Enzi za Kanali mstaafu na mwanadiplomasia Jakaya Mrisho Halfan Kikwete alionekana ama nchi za nje, Jijijini Dar Es Salaam na Msoga na kufanyia shughuli zake za serikali katika ikulu ya Magogoni Dar Es Salaam au nchi yoyote huko ughaibuni inategemeana na alivyopanga;
5. Enzi za Mwalimu na Mkemia Dk John Pombe Magufuli anapokuwa mapumziko siku zote anaonekana Kijijini Rubambangwe na mjini Chato na kutekeleza majukumu yake ya Urais akiwa hapo Chato;

TANBIHI: Kwa hiyo ikulu sio jengo maalumu la kiofisi kwa utekelezaji wa majukumu ya kiuRas. Mahali Rais alipo hasubiri kurejea kwenye ikulu kuu ya Magogoni au Chamwino kutekeleza majukumu yake ya Urais, mahali popote alipo taasisi zote zinazounda mamlaka ya taswira ya Rais wa nchi zinafanyika kwa ufanisi ule ule.

Hakuna hata mwandishi au mwanasiasa yeyote wa sasa ambaye alishawahi kuelezea kwa kina makazi ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete yaliyoko huko Msoga, Chalinze zaidi ya kushiriki hafla mbalimbali ambazo mhusika anapokuwa na nafasi ya kuwashirikisha kuujulisha umma hasa shughuli za kilimo na ufagaji, lakini yeye mwenyewe alishawahi kusikika akisema ni kweli ana makazi huko Msoga lakini hawezi kuishi huko.

Kauli hii ilitakiwa ifuatiliwe na ifafanuliwe vyema kwa manufaa ya jamii. Hospitali iliyopo hapo Msoga enzi akiwa madarakani ilikuwa imechangamka sana na majengo yalikuwa ni angavu lakini kwa sasa tayari yamechakaa na sijui kama kuna mpango wowote wa kuyahuisha kurudi katika ubora.

Hakuna shughuli za kiuchumi zilizowekezwa kuzunguka kijiji hicho ambacho inaonekana kina rutuba na hali ya hewa nzuri kwa kilimo, ufugaji na masoko ya mazao kama Nanasi, Mahindi, Papai, Machungwa na matikiti maji. Kabla hajamaliza muda wa uongozi wake ilipangwa kujengwa bandari ya nchi kavu kati ya Chalinze na Msoga lakini mpaka sasa hakuna chochote.

Kijiji kimezungukwa na misitu yenye uwanda mpana unaoweza kutengwa kwa ajili ya hifadhi na utalii. Lakini pia ndio eneo maarufu kwa sasa ambako ndipo yanapatikana mali asili madini mawe meusi ambayo yanatumika sana kwenye ujenzi wa miundo mbinu imara kama mchanganyiko wa lami, zege kwenye miundo mbinu ya ujenzi wa SGR, Stiglers Gorge dam, barabara, hata kwenye viwanda vya simenti kwa kuwa mawe hayo ni magumu sana.
 
We kweli bwege unalinganisha Dar na huo uchafu Chato?Dar inachangia asilimia 80 ya pato la Taifa,kwa kila shilingi 100 zinazokusanywa Kama mapato na TRA,shilingi 80,zinatoka Dar,hapo ni lazima Dar uipe kipaumbele,hata mtoto wa Darasa la Saba anajua Hili,sasa Chato Kuna nini?

Weka mifano sio kusema jiwe kajenga sehemu nyingi,
 
Chato ina mapato gani iliyokua inatengeneza mpaka ipewe kipaombele hivyo. Angalia mikoa yenye kuingiza mapato makubwa serekalini kama Arusha,Dar,Iringa(Mufindi),Kilimanjaro,Shinyanga haijapewa kipaombele kama ilivyo chato....Chato ilikua kijiji hakina mapato yoyote. Chato ndo ya kupewa
Hosptal ya rufaa
Mahakama ya kisasa
Uwanja wa kisasa wa mpira
(National zoo) chato burigi
Internationa Airport
Chuo cha utumishi wa uma
chuo cha VETA
Ndani ya miaka 5 tuu
Huu ni ubinafsi kiwango cha lami haufai kufumbia macho hata kidogo
 
Mtoa mada unayashabikia haya kesho si ajabu akatunga sheria Kama utoki chattling ni marufuku kupata ajira serikalini ndipo utaikana post yako.Central Afrika, Rwanda na Burundi, nigeria yaliyaanza kidogo kidogo Kama haya ukabila,udini,ukanda kustukiza hakuna anaepumua
 
Ili tukuamini unachokisema weka miradi hiyo hapa kwa uwiano wathamani na uwiano wa mgawanyo wa kieneo na kikanda,kushindwa kufanya hivyo ni porojo na uimbaji wa mapambio unaloligharimu taifa hili.Ukweli ,na haki huinua taifa.
 
Kaka nilikua nakuheshimu sana kumbe kichwan bora kibuyu kabisa
Sema tu BAVICHA mna roho za ubinafsi sana, roho zimejikunja. Pingapinga, tu toka Taifa lipataje uhuru nyie ni kupinga pinga,
 
Yanayofanyika Chato; Yanafanyika Kote Nchini Tanzania

Na: Mzalendo wa kweli (ellyskywilly)

Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikifanya kila liwezekanalo katika kuhakikisha Tanzania nzima inakuwa na maendeleo ya vitu na watu, hivi sasa kila ukipita kwenye maeneo mengi nchini utakutana na ama miradi imekamilika au inaendelea na ujenzi au ipo katika hatua za mwisho za kumalizika kwa miradi mbalimbali.

Ukianzia Jijini Dar es Salaam tunashuhudia miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, hospitali na huduma nyingi sana za Kijamii, ukija Mkoa wa Pwani halikadhalika utakutana na ujenzi wa miundombinu mingi.

Ujenzi huo pia unafanyika kwenye maeneo mengi nchini.

Kinachofanyika Wilayani Chato ndicho kinachofanyika kwenye maeneo mengi nchini Tanzania, ninasema hivi kwa sababu wasioitakia mema nchi yetu mara nyingi wanahoji eti kwa nini maendeleo yanafanyika Chato! Wananchi wa Chato ni Watanzania kama ilivyokuwa kwenye maeneo mengine nchini ambayo maendeleo ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo unafanyika.

Swali la kujiuliza ni kwamba, hivi Chato ipo nchi gani? hivi Wananchi wa Wilaya hiyo hawahitaji hospitali? hawahitaji barabara? Hawahitaji huduma za kijamii kama ilivyo Dar es Salaam na Mikoa mingine? Wanaoeneza habari hizi za uzandiki bila shaka ni walewachumia tumbo ambao wanadhani huu ni muda wa propaganda

Wanahoji ujio wa hivi karibuni wa baadhi ya Viongozi wakuu wa nchi waliotembelea Chato eti kama dhifa za kitaifa na magwaride ya heshima kwa ajili ya Wakuu hao yamefanyika Chato, walitaka vifanyike wapi? Dar es Salaam? Dodoma? Au Kilimanjaro? Wamekosa hoja.

Kufanyika kwa mapokezi hayo Chato ni sawa sawa kabisa kwa sababu tukumbuke Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli anatokea Chato, kama ilivyo kawaida mahali anapotoka Rais ni lazima kuwe na Ikulu ndogo ambayo shughuli zote za Rais zinafanyika, tumeshuhudia Butiama kwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, tumeshuhudia kwa Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, awamu ya tatu, ya nne na ya sasa ya Dkt. Magufuli.

Chato kama ilivyokuwa maeneo mengi nchini inahitaji miundombinu ya usafirishaji kama inavyofanyika sasa ya ujenzi wa uwanja wa ndege wenye uwezo wa kutua na kurusha ndege kubwa sawa na viwanja vya ndege vya Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Mwanza na Mbeya.

Chato inahitaji kuwa miongoni mwa Wilaya za kisasa kwa kuwa na miundombinu bora ya barabara na taa za kuongozea magari barabarani, hata ikiwa ni Wilaya pekee yenye miundombinu bora nchini ni Sawa kabisa kwani kwa miaka mingi tumeshuhudia miji ya Dar es Salaam ikiwa na miundombinu bora, mbona Chato hawakupiga kelele?

Wilaya ya Chato ni ya kipekee kwa vivutio vya Utalii ikiwepo hifadhi ya Taifa ya Burigi na hivyo kuwepo kwa ongezeko la Watalii ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakiliingizia Taifa fedha za kigeni hivyo kuna kila sababu ya kuiendeleza Wilaya hii.

Chato kama ilivyo kwa Wilaya na Mikoa mingine Nchini Tanzania ipo katika program za kuanzisha na kuendeleza michezo program ambazo zinaenda sambamba na ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu pamoja na Michezo mingine mingi.

Kutokana na umuhimu wa Wilaya ya Chato kibiashara sasa Mabenki ya kibiashara na taasisi nyingine zimeona fursa na kuamua kuwekeza kwenye Wilaya hiyo inayokuja juu kibiashara.

Wilaya ya Chato kijiografia ipo katika Mkoa wa Geita Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania, Chato ni mojawapo ya Wilaya tano za Mkoa wa Geita na kiuchumi Wilaya hii inafanya shughuli za kilimo cha kibiashara, uvuvi na shughuli nyingine za kiuchumi.

Kwa upande wa Sekta ya utalii, ni kwamba Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo katika Ziwa Victoria ipo nje kidogo ya Wilaya ya Chato. Hifadhi hiyo ilianzishwa mwaka 1965 na, kwa mujibu wa takwimu zilizopo sasa, hifadhi hiyo inatembelewa na wageni wengi sana kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Wilaya ya Chato ilianzishwa mwaka 2005 kutoka iliyokuwa Wilaya ya Biharamulo, Mkoa wa Kagera. Mwaka 2012, Wilaya hiyo ilihamishiwa kwenye Mkoa mpya wa Geita.

Wilaya hii imekuwa maarufu zaidi Kutokana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyechaguliwa kama Rais wa Tanzania mwaka 2015, alizaliwa Chato mwaka 1959.

Hivyo basi kwa wanaobeza maendeleo ya Chato hawana hoja kwa sababu Wananchi wa Chato wanahitaji maendeleo pia, sio dhambi Rais kupeleka maendeleo na nyumbani kwao kama anavyofanya nyumbani kwa watanzania wengi kwenye Mikoa yote Nchini.

Hivi kuna dhambi mtu akajenga kwao, namaanisha yaani unafanya kazi alafu usijenge angalau nyumba ya chumba na sebule nyumbani kwako? Yaani utachekwa hadi na sisimizi, Magufuli anapaswa kuendeleza Chato kama anavyoendeleza Kilimanjaro, Arusha, Mbeya na kwingineko.

Sio vibaya nyumbani kwa Rais wa nchi kuwa na maendeleo au mambo mazuri, na wala sio sifa nyumbani kwa Mkuu wa Nchi kuwa pa hovyo hovyo au duni kimaendeleo, hili naomba Watanzania mlielewe.

Vipaumbele vya Watanzania ni maendeleo na ndio dhana ambayo inafanywa Rais Magufuli Nchini kote ikiwepo Wilayani Chato.

Ni ukweli usiopingika kwamba mambo mengi na mazuri yanayofanywa Chato hayatokani na uhusiano wake na Rais Magufuli bali uhusiano wa Wananchi wa Chato na fursa za kiuchumi katika Wilaya hiyo.

Watu wengi wanafurahia kuona Wilaya zilizopo pembezoni mwa Tanzania zikibaki kuwa maskini katika uendelezaji wa miundombinu yake hali ambayo Rais Magufuli ameiondoa kwenye akili za watu, Rais Magufuli anaiambia Dunia kuwa hata katika Wilaya hizo kunahitajika kuwepo kwa miundombinu bora.

Ikumbukwe kuwa Rais Magufuli amefanya mambo mengi makubwa ndani ya muhula wake wa kwanza, kwa maneno mengine, hata kabla ya kufikisha miaka minne kati ya mitano ya muhula wake wa kwanza, Rais Magufuli amefanya mambo makubwa nyumbani Tanzania nzima kuliko walivyofanya Marais wa Tanzania waliomtangulia katika miaka 54 waliyokuwa madarakani.

Rais Magufuli amefanya yote haya katika mazingira ya kikatiba, kisheria na kisiasa ambayo ni magumu zaidi kuliko ya watangulizi wake wote kwani tangu tuwe Jamhuri mwaka 1962.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli mwaka 2015 amekuwa na rekodi ya kipekee ya kuweza kufanya mambo makubwa nyumbani Nchini pengine Wananchi wanajiuliza amewezaje kufanya mambo haya makubwa!? Jibu rahisi sana, utayari na uchungu wa maisha ya Watanzania wenzake.

Aliyoyafanya Rais Magufuli nchini Tanzania kwa kipindi kifupi tu na ambayo hayajawahi kufanyika tangu Uhuru wa Taifa letu yanamuweka katika kundi la kipekee hata katika Bara zima la Afrika. Bara letu limekuwa na Marais wa aina hii wachache sana na huenda wasiwepo.

Ni Rais Magufuli ndie aliyerudisha nidhamu kwa Viongozi na wafanyakazi wa Serikali, ni Rais Magufuli ndie aliyekabiliana na rushwa na ufisadi, ni Rais Magufuli ndie anaependwa na mataifa mengi Duniani kwa namna anavyoiendesha nchi na kufikia hatua ya kukabiliana na majanga mbalimbali likiwepo janga la Corona linaloikumba Dunia kwa sasa.

Huu ndio upekee wa Magufuli katika Tanzania, katika Bara la Afrika na Duniani, ni upekee wa kujivunia sana.
Chato, chato, chato= I am the state
 
Back
Top Bottom