Yanayojiri Azam VS El Mereikh

Yanayojiri Azam VS El Mereikh

yeah inaonekana vizuri

attachment.php

Basi Net yangu huenda ikawa ndo mgogoro.
 
daah matokeo wadau au ndo kusema mnakula bia muda huu? wengine hatupendi tv bana hebu leteni habari hapa!
 
Kwa matokeo haya Azam anatakiwa atangulie kutafuta goli moja ugenini kabla ya kufungwa...

Waarabu hawa wa Sudan ni wazuri sana nyumbani...

Maadam wana hela, wanaweza kwenda na mikate yao, maji yao, na kulala kwenye hoteli waitakayo wao, fitna za nje ya uwanja wanaweza kuzidhibiti.

Ni tumaini yale mambo ya akina "Madeni ya Maharage" hayatarudiwa tena,ya kusafiri na kipanya mwendo wa masaa kadhaa, kuingizwa kwenye hoteli chafu usiku wa manane, na kuchezea kichapo cha magoli matatu ndani ya dakika kumi za mwanzo wa mchezo.

Huyu beki kisiki wa Ivory Coast aliyetokea El Mereikh atakuwa shamba darasa kwenye fitna za hao waarabu weusi.
 
Back
Top Bottom