Sitta, ninakupa ushauri wa bure! You talk too much! Kificho ameweka standard mpya ya Spika (Mwenyekiti), so be careful, kazi yako ya nyuma inaweza kuingia mchanga. Biblia inasema katika MITHALI 10:19,"Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili." Kificho yuko makini, hasemi maneno mengi, na ni mwangalifu sana katika kuchagua maneno ya kuzungumza. Mind you, kwa kila jambo sasa utapimwa katika mizani na kulinganishwa na Mwenyekiti wa muda, Kificho, na wala siyo Makinda! Mwenyekiti wa kudumu anatarajiwa na wengi, awe na uwezo na hekima zaidi, kuliko Mwenyekiti wa muda! Kumbuka kwamba kuanzia sasa, kila neno lako moja, lina tafsiri elfu moja, kwa maadui zako, na marafiki zako wa zamani! Neema ya Mungu ikufunike!