KOLOKOLONI
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 2,476
- 2,371
Bunge ni kama "limevunjika". Sitta anasema ameliahirisha hadi baadae. Wajumbe hawakuruhusu Warioba kuongea hata neno moja ingawa alisimama kwenye podium.Mkuu nini kinaendelea huko, naona utabiri wako unatimia kuwa inawezekana leo kukatokea mgawanyiko mkubwa.!
Kuna tetesi nambiwa hapa eti Warioba ameshindwa kuwasilisha Rasimu baada ya Wajumbe baadhi kuzomea....na Bunge limeahirishwa !.
hEBU TUPENI HABARI ,WENGI BADO TUPO OFISINI
Ni kweli mkuu makelele yalikuwa mengi mno!hadi imemlazimu mwenyekiti kuhairisha kikao hadi itatakapotangazwa tena.Kuna tetesi nambiwa hapa eti Warioba ameshindwa kuwasilisha Rasimu baada ya Wajumbe baadhi kuzomea....na Bunge limeahirishwa !.
hEBU TUPENI HABARI ,WENGI BADO TUPO OFISINI
Mwenyekiti amelazimika kusitisha shughuli za bunge leo jioni baada ya wabunge kukataa kusikiliza hotuba ya mwenyekiti hii inaonesha pia Warioba ameamua kugoma kusoma kwani wazo la Sita lilikua isomwe tu.
Bunge limehairishwa kwa muda.
star tv nao bure kabisa siku hizi ka nokia ya tochihivi kuna live coverage ambayo nnaweza cheki online kuhusu bunge la katiba, maana star tv leo michosho hawapatikani
Ndivyo alivyo fanyiwa, baadhi ya wabunge wakiongozwa na Mtikila wamesimama na kuanza kupiga meza huku wakionesha hali ya kutokukubali Jaji Sinde hasisome rasimu bungeni.Kuna tetesi nambiwa hapa eti Warioba ameshindwa kuwasilisha Rasimu baada ya Wajumbe baadhi kuzomea....na Bunge limeahirishwa !.
hEBU TUPENI HABARI ,WENGI BADO TUPO OFISINI
Wajumbe wamesikika wakimtaka mwenyekiti afuate kanuni vinginevyo hakuna kitakachoendelea!Punde nimefungua TBC Tv channel nilichokishuhudia ni wajumbe kumshangilia jaji Warioba mfululizo kwa kugonga meza bira kikomo mpaka speaker akaamua kuvuja kikao. nini kilitokea?// naomba mnijuze wana jamvi