Yanayojiri Bungeni Dodoma: Leo Jumatano, Tarehe 26 Novemba, 2014

Status
Not open for further replies.
Nahisi wabunge watakaopewa nafasi ya kuchangia leo watakuwa ni wale walioandaliwa mahusudi ili kudhoofisha mjadala
 
Asipotoka nduki mtu Bungeni leo basi tegemeeni Mipasho.

Mimi nipo pamoja nanyi kufuatilia mjadala huu, full charge na nina kagenerator kadogo hapa basi mambo Muruuuaaaa
 
Wanabodi,

Kwa mliongalia bungeni leo kupitia Star TV, Jee baada ya ile amri ya Mahakama jana kulizua Bunge kujadili hoja ya Escrow, jee kuna yeyote aliyeona hati zilizowasilishwa mezani asubuhi hii leo?!, Jee Ripoti ya CAG ya Ukaguzi Account ya Tegeta Escrow, na Maoni ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC imewasilishwa mezani?!.

Kama zimewasilishwa, hii inamaanisha Bunge letu tukufu, litakuwa limeidharau amri halali ya mahakama!. Amri yoyote halali ya mahakama ni enforceable by law, hivyo amri hii inapopuuzwa, arrest warrant hutolewa kuwatia mbaroni waliopuuza amri hii!, Bunge likiipuuza amri hii, jee baada ya mahakama kupuuzwa, will it enforce it?!, Jee Spika Makinda na Katibu wa Bunge Dr. Kashilila, watatiwa mbaroni leo?!.

Endelea kufuatilia.

Pasco.
 
Mkuu Pasco ni nani kakuambia kuwa BUNGE limekaidi amri ?
Bunge ni muhimili unaojitegemea wenye kanuni, taratibu na sheria zake za uendeshaji. Hivyo kinachofanyika hapo na bunge ni kulinda hadhi na madaraka yake kama BUNGE , na sio kupelekeshwa pelekeshwa na muhimili mwingine.
Mambo ya bunge ni ya bunge , na ya mahakama ni ya mahakama. Mbona hiyo mahakama haikumzuia CAG kuchunguza na kuwasilisha taarifa yake, eti leo inajitia kimbele mbele kuja kuzuia Bunge. Jaji mkuu ajitathmini ili "tusije mtoa nyota " mapema.
Moto usha washwa hakuna wa kuuzima ...Tunahitaji safisha hiki kichaka Tanzaniaili tuweze pata nchi safi na yenye maendeleo .
 
Last edited by a moderator:
Mhhh.......naogopa kua na higher expectation jamani maana hili li nchi halitabiliki kabisa.
 
Skype Mkuu naangalia kupitia TV Kuhusu masafa yao ya FM ngoja utajuzwa hapa hpa
 
Last edited by a moderator:
Kabla ya hapo nilidhani (I was wrong) kuwa mahakama itakuwa na nguvu ya kulisimamisha bunge kujadili lakini nimeona kuwa haliwezi kikatiba. Unless, yule aliyeleta kifungu hiki cha katiba awe kachakachuwa:

Ibara ya 100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika
Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema
au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo
 
Hashikwi mtu mbunge anakinga kwa jambo lolote alifanyalo bungeni. Ni bunge lenyewe tu ndio laweza kumuadhibu. Kwani Mahakama haiwezi subiria bunge limalize kazi yake ndio iendelee na hiyo kesi?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…