Yanayojiri Bungeni Dodoma leo March 08, 2014

Yanayojiri Bungeni Dodoma leo March 08, 2014

Naam mkuu nimerejea baada ya kuzipata rejea zangu, jina lake anaitwa Dr. Tulia Ackson (si kama ulivyoandika), anafanya kazi chuo Chuo Kikuu cha Dar es salaam kama Mhadhiri mwandamizi (Senior Lecturer) kitivo cha sheria (Faculty of Law), pia ni Associate Dean, University of Dar es Salaam School of Law.
Mkuu, nakushukuru sana kwa taarifa hii. Tayari nilirekebisha jina lake maana nilikuwa nimeandika jinsi nilivyokuwa nalisikia kutoka kwa Mwenyekiti na mwenyekiti wa Kamati
 
Kanuni zote kuanzia za 32 hadi 43 zimepitishwa isipokuwa kanuni ya 37 na 38 ambazo maelezo yake tumeyatoa. Sasa Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni anapewa nafasi ya kueleza kazi waliyopewa kuhusu Nyongeza na Kanuni. Mwenyekiti anasema kuwa nyongeza ya kanuni imekamilika na Mwenyekiti anawahoji wabunge kama waendelee kujadili au la. Baadhi ya wabunge wanasema kuwa kikao kiahirishwe hadi Jumatatu. Wabunge wanaafiki suala hilona kikao kinaahirishwa hadi jumatatu ijayo
 
Nawashukuru sana wote walioshiriki kwenye mjadala huu na Mungu akitujaalia tukutane siku ya Jumatatu kwa ajili ya kumalizia viporo vya vilivyobaki na probably uchaguzi wa Mwenyekiti. Stay Connected
 
Kuna mjumbe anajiita daktari nani sijui... Yeye naona kakariri. Anasema "There is Always Next Time". Akimaanisha muda umepita sana watafanya kazi hata jumatatu. Nadhani huo msemo si wa kutumia kila sehemu.
 
Mwenyekiti anatoa ufafanuzi kuwa kila kilichojadiliwa kimepitishwa na kazi iliyobaki ni ya kuandaa final draft ya kanuni kwa ajili ya kupitishwa.
 
Pongezi za kipekee ziende kwa Mkuu Skype ​ambaye alikuwa nami sambamba kuwaletea updates za semina hii.
 
Asante sana mkuu. Tunakutarajia tena kukuona jimatatu mumu humu jamvini.
 
Pongezi za kipekee ziende kwa Mkuu Skype ​ambaye alikuwa nami sambamba kuwaletea updates za semina hii.

Pamoja sana mkuu bila kumsahau MaishaPesa na wengineo nisiowatambua, sasa ngoja nihamie majukwaa mengine kwa uchambuzi wa hoja za leo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Skype,
Si wewe pekee mwwenye maumivu ukiyafikiria hayo, ni kila karibu kila mtu mpenda mabadiliko wa nchi hii. Piga hesabu hivi, wabunge wote wa bunge la katiba na watumishi wengine muhimu kwa bunge hili wawe tu jumla ya watu 650. zidisha hiyo 650 x per day tsh 300,000/= utapata jibu kuwa tsh 195,000, 000/= zinatumika kwa siku moja Kisha jumlisha matumizi mengine ya siku kama umeme, maji, makaratasi na mengineyo. Bila shaka itapita zaidi ya milioni 200 kwa siku

Ukitaka upate presha sasa zidisha hiyo zaidi ya 200 mills kwa siku zilizokwishapita hatafu jumlisha na siku 70 zilikusudiwa. Utakuta ni zaidi tsh 22,400, 000, 000/=. Uuuuuuuwiiiiii.

Baaasi mkuu, usizidi kuniongezea presha, yani umenikumbusha mabilioni tuliyokua tunawalipa dowans, epa na madudu mengine yanayofanana na hayo. Aise uwe na siku njema.
 
Back
Top Bottom