Mkuu, nakushukuru sana kwa taarifa hii. Tayari nilirekebisha jina lake maana nilikuwa nimeandika jinsi nilivyokuwa nalisikia kutoka kwa Mwenyekiti na mwenyekiti wa KamatiNaam mkuu nimerejea baada ya kuzipata rejea zangu, jina lake anaitwa Dr. Tulia Ackson (si kama ulivyoandika), anafanya kazi chuo Chuo Kikuu cha Dar es salaam kama Mhadhiri mwandamizi (Senior Lecturer) kitivo cha sheria (Faculty of Law), pia ni Associate Dean, University of Dar es Salaam School of Law.
Twendeni tatayibu jamani hapa sio jukwaa la siasa ni katiba mpya! chondechonde!.
hizi habari za kula ya wazi sitaki kabisa kuzisikia wakuu sijui kwanini ccm wanai ng'ania hii kitu ya kura ya wazi
Pongezi za kipekee ziende kwa Mkuu Skype ​ambaye alikuwa nami sambamba kuwaletea updates za semina hii.
Pamoja sana mkuuPamoja sana mkuu bila kumsahau MaishaPesa na wengineo nisiowatambua, sasa ngoja nihamie majukwaa mengine kwa uchambuzi wa hoja za leo.
Mkuu Skype,
Si wewe pekee mwwenye maumivu ukiyafikiria hayo, ni kila karibu kila mtu mpenda mabadiliko wa nchi hii. Piga hesabu hivi, wabunge wote wa bunge la katiba na watumishi wengine muhimu kwa bunge hili wawe tu jumla ya watu 650. zidisha hiyo 650 x per day tsh 300,000/= utapata jibu kuwa tsh 195,000, 000/= zinatumika kwa siku moja Kisha jumlisha matumizi mengine ya siku kama umeme, maji, makaratasi na mengineyo. Bila shaka itapita zaidi ya milioni 200 kwa siku
Ukitaka upate presha sasa zidisha hiyo zaidi ya 200 mills kwa siku zilizokwishapita hatafu jumlisha na siku 70 zilikusudiwa. Utakuta ni zaidi tsh 22,400, 000, 000/=. Uuuuuuuwiiiiii.