Yanayojiri kwenye Sakata la Mwalimu kumchapa kikatili Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wilayani Kyerwa, Kagera

Yanayojiri kwenye Sakata la Mwalimu kumchapa kikatili Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wilayani Kyerwa, Kagera

Hutu tu clip twa simu tutafukuzisha staff wengi sana wa serikali, Mungu tena!

Mmoja anachapa kishenzi, staff mwingine yupo pembeni anafotoa kinyama na kurusha
!
Tukiachana na stori za ukiukwaji wa haki za binadamu, hili limekaaje hili!
 
Kuna sababu nyingi za serikali kutowathamini walimu.

Asilimia kubwa ni wakatili sana japo ndio wanaofundisha watoto wetu, hivi ingekua ndio mtoto wake anaona anavyochapwa hivyo angejiskiaje?

Waalimu wa namna hii ni mafakeni tu hawana maana
 
Alafu unamchapa mtoto kwenye sehemu sensitive na delicate namna hiyo miguu una mishipa karibu yote ya fahamu za mwili wa mwanadamu adhabu ilishawekewa vigezo msichana atachapwa mikononi na mvulala atachapwa matakoni hayo mengine wizara na wajinga wake wakaangalie hao wajinga kabisa wanachukuliwaje hatua
 
Wazazi wanatakiwa walipe visasi kwa walimu au watu wanaowafanyia unyanyasaji watoto wao.

Iruhusiwe kisheria.
Yaani ndio mwanangu anarudi ananiambia amefanyiwa hiko kitendo aloo hata kama mwalimu anasingiziwa mahakama itakua ndogo kesi kubwa huu ni ukatili uliopitiliza
 
Sasa mtoto kama huyo atakuwa amefanya kosa gani mpaka anapewa adhabu kama hiyo kisa kapata 1/10 au
Na pembeni kule wamekaa wengine wanacheka tu kama ni jambo la kawaida linalotendeka [emoji706] kuna watu ni matakataka
Mambumbumbu hayo DIVISHENI FOO.

Hakika ningekuwa na mamlaka ningewashughulikia kwa mapana na marefu.
 
Kuna matoto yamekubuhu kweli kweli, yametoka kwenye familia za malezi ya hovyo hovyo, yamejifunza mambo tofauti na umri wao, wanasumbua na huharibu wenzao waliotoka kwenye familia Bora. Wakiachwa Taifa litaangamia. Mwalimu lazima saa nyingine ajivike mabomu kwa maslahi mapana ya nchi
Fundisha rudi nyumbani.

Mengine hayakuhusu
 
Kuna matoto yamekubuhu kweli kweli, yametoka kwenye familia za malezi ya hovyo hovyo, yamejifunza mambo tofauti na umri wao, wanasumbua na huharibu wenzao waliotoka kwenye familia Bora. Wakiachwa Taifa litaangamia. Mwalimu lazima saa nyingine ajivike mabomu kwa maslahi mapana ya nchi
Acha ukichaa kabisaa
 
Kwani kamuua, kuna vitu vya msingi vya kushadadia na sio hizo mambo za maskuli mnapigwa kodi zenu na viongozi wa juu mpo kimya ila upuuzi ndo mnaupazia sauti
Kama mwanao nilisugu wakwetu hawawezi kupigwa ivyo adhabu zipo na sheri mahali pakuchapa panajulikana kwaiyo ww unaona anapo chapa ni sahihi??????
 
Hv Mwalimu ukikausha ukawa unafundisha zako ukimaliza unaendelea na mishe zako utapungua nini?
Kuwa mwalimu Kama hiko kitu kinawezekana uone, mwalimu ana wajibu wa kitaaluma na nidhamu pia hio ni wajibi na lazima Hapo kwenye nidhamu Sasa nakwambia jaribu kuomba nafasi ya kuwa mwalimu hata kwa miezi mitatu then uwone sawa na useme wewe una wajibu wa nidhamu ya watoto wako eti huwezii wakiza tu watoto mpaka wanakua bila hata kuwafanya chochote impossible impossible
 
Daaah ni kweli mkuu. Ila mara nyingi haya mambo yanafanyika shule ambazo zipo ndani ndani kidogo. sijawahi sikia dar matukio kama haya mkuu au yapo?
Yapo kote mpk Dar sema Sio kiwango kikubwa ,walimu wengi tuna shida na tunapenda sana sifa tunadhani kuchapa ndo kufunza
Vijijini Huko Hali ni mbaya sana kwanza wakuu wa Shule wanajiona wao exceptional hawaguswi wanaanzisha masheria ya hovyo mashulenu watoto wanafukuzwa Shule kirahisi TU
Hapa Dodoma Shule Fulani siku ya mtihani wa darasa la 7 mkuu wa Shule kafukuza watoto wasifanye necta kisa hawajaja Shule wiki Moja TU,mpk wanafuni wenzao wakawa wanalalamika yaani wiki Moja mwl mkuu kafukuza wasifanye mtihani na anajua wazazi au walezi hawana uwezo wa kufatilia ipasavyo kutafuta hakiza watoto wao

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hayo mamlaka mkuu wa shule anayatoa wapi? Tatizo ni kupewa vyeo kwa kuhonga ila kichwani hamna kitu.

Sent from my CPH2239 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom