Yanayojiri kwenye Sakata la Mwalimu kumchapa kikatili Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wilayani Kyerwa, Kagera

Yanayojiri kwenye Sakata la Mwalimu kumchapa kikatili Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wilayani Kyerwa, Kagera

Nidhamu ya shule ikiwa mbovu wanasiasa watakuvamia tena.

Kimsingi walimu hawapui wakisimama nchale wakichuchuma nchale, wakikikimbia nchale, wakilala nchale.

Wanasiasa wakisikia tu mwalimu Fulani kazingua wako fasta kwenda chukua credit.
nidhamu ninawahusuje wanasiasa? labda ungesema wazazi
 
Sintoweza kuangalia video inayotia hasira wahuni kama hao adhabu zao zinatakiwa ziwe kubwa sana...ili iwe Fundisho kwa wahuni wengine wakatili kwa Watoto.
Hasira zao ,stress zao wanawahamishia wanafunzi

Wakati wetu tuko shule ujinga kama huu ukikutokea kungechimbika

Ova
 
Hii wiki nimekuwa nazurula kwenye mashule kwa michakato ya kazi zangu .Tunajaribu kuwafahamisha nini cha kufanya na nini wasifanye .Nimekutana na watu wazuri sana ,sijui wanakumbwa na vitu gani lakini wengi niliokutana nao watoto kwa walimu watu safi sana.Tuache ukatili kwa watoto mambo yakigeuka rangi zote utaziona vizuri.
Stress

Ova
 
Yap inaumiza sana kwa kweli dogo kupigwa kama ngoma..
Wakati nasoma sangu sec form 1
Nlikutana na kipondo hapo shule
Kuna sehemu shuleni wanapaita soweto, nlipelekwa pale nkalazwa chini kila mwalimu akipita ni bakora
Kuna mwalimu mmja alikuwa mkuda
Anaitwa kasebele na kabigi
Hao nkiwakariri
Nlikuja mtafuta mwalim nje ya shule
Nlichomfanya alijuta kunipiga
Nlafukuzwq shule hiyo
Nkaenda St Anton naye wakat wa bro masabo pale napo kuna mwalim alinizingua,nami nkaja mzingua nkafukuzwaaa tena
Primary school nko mbuyuni kuna mwalimu alikuwa anaitwa omary ah nishashikatana naye sana mashati
Mpk nikawa nampiga biti namwambia poa tutakutana mtaani
Mm suala la kuonewa kwangu huwa ni mwiko ilikuwa

Ova
 
Wakati nasoma sangu sec form 1
Nlikutana na kipondo hapo shule
Kuna sehemu shuleni wanapaita soweto, nlipelekwa pale nkalazwa chini kila mwalimu akipita ni bakora
Kuna mwalimu mmja alikuwa mkuda
Anaitwa kasebele na kabigi
Hao nkiwakariri
Nlikuja mtafuta mwalim nje ya shule
Nlichomfanya alijuta kunipiga
Nlafukuzwq shule hiyo
Nkaenda St Anton naye wakat wa bro masabo pale napo kuna mwalim alinizingua,nami nkaja mzingua nkafukuzwaaa tena
Primary school nko mbuyuni kuna mwalimu alikuwa anaitwa omary ah nishashikatana naye sana mashati
Mpk nikawa nampiga biti namwambia poa tutakutana mtaani
Mm suala la kuonewa kwangu huwa ni mwiko ilikuwa

Ova
Sangu nimepiga Advance kule Soweto nilipaona pana dogo mmoja mtukutu Kambasonic wa mtaani alikua anapaongelea sana hapo na wakija Club Mount Livingstone akipiga mkwara Tura yeyote anamwambia atamvizia Soweto...Sangu ilikua na watu sana nimepita pale enzi za Mwalimu Bukuku Mtaalamu wa Uchumi..baada ya Mwalimu Mwakyulu Marehemu...RIP
 
Hii wiki nimekuwa nazurula kwenye mashule kwa michakato ya kazi zangu .Tunajaribu kuwafahamisha nini cha kufanya na nini wasifanye .Nimekutana na watu wazuri sana ,sijui wanakumbwa na vitu gani lakini wengi niliokutana nao watoto kwa walimu watu safi sana.Tuache ukatili kwa watoto mambo yakigeuka rangi zote utaziona vizuri.
Hapo wameitikia tu nduguu yangu I know my fellow teachers kichapo kinaendelea kama kawa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: K11
Ninalea mtoto mtukutu mno wa ndugu yangu, mama yake ametoweka mwaka karibu wa nne hatujui alipo. Pamoja na utukutu wa mtoto sijawahi hata kufikiria kumpa adhabu ya kikatili namna hiyo. Huwa sielewi watu wanaofanya ukatili kwa watoto wanafikiria nini vichwani mwao
 
Tafadhali ni nani anayejua hii shule?

====

UPDATES: 1
Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalumu Dorothy Gwajima, Serikali imefanya ufuatiliaji wa kina na kubaini kuwa tukio hili lilitokea Januari 10, 2023 kwenye Shule moja ya Msingi iliyopo Wilayani Kyerwa, Kagera.

Akithibitisha hayo kupitia Akaunti yake rasmi ya Mtandao wa Instagram, Waziri Gwajima amesema kuwa hali ipo kwenye udhibiti mzuri (Situation is under control) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila atatoa taarifa inayohusu tukio hilo Januari 25, 2023.

Waziri Gwajima amelaani tukio hilo na amewaasa walimu kuzingatia utaratibu wa adhabu wanazotoa kwa wanafunzi, pia amewataka kuheshimu sheria kwani Hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaofanya aina hii ya ukatili.



View attachment 2494390

UPDATES: 2
Mwalimu aliyeonekana akimuadhibu mwanafunzi kinyume na taratibu, akimchapa kwenye nyayo za miguu, amesimamishwa na kutenguliwa Kwa nafasi yake kama Mwalimu mkuu. Pia, ameshaandikiwa Mashtaka kwa Mamlaka ya TSC ili akajibu tuhuma zinazomkabili.

Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda amesema hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.

UPDATES: 3

View attachment 2494822

Mtuhumiwa yupo ndani, Mkuu wa Mkoa ameshafika hospitalini kumuona mtoto na Jeshi la Polisi linaendelea na hatua zake.
Huyo mkuu wa mkoa aliwahi kuwalamba mboko wanafunzi kule mbeya akiwa mkuu wa mkoa huo. Kwa kuwa jinai haifi ni vizuri polisi wamweke ndani na kumfungulia mashitaka kama huyo mwalimu.
 
Corporal Punishment.

Educational psychology hakuizingatis mwalimu.

By the way Kuna mambo ya kuyaacha kama yalivyo sometime ukijifanga ngangari sijui kindakindaki unakutana na visanga na misala kama hio.

Ticha hatotoka salama wanasiasa watamfanya asusa.
Kuna SoMo la measurements & evaluation.....
Walimu hufundishwa tena Kuna Saga Moja ntaisimulia kidogo.....

Kuna baba mmoja alinunua gari mpya ya bei kali na gari Ile NDIO ilikua ya kwanza maishani mwake......kama tujuavyo kimuhe muhe Cha gari la kwanza...

Siku Moja baba alipak gari yake nje ya nyumba kama ilivyo kawaida yake........mtoto Ake mdogo akawa amechukua jiwe akawa kama ana scratch bodi ya gari....... mzee alipo Toka nje akamwona Kwa mbali mtoto Ake kama ana scratch bodi ya gari Ake....
Mzee akaja fasta fasta akamkamata mtoto akachukue praizi akaanza kumpiga nayo mtoto mkononi....... Kwa hasira several times kuja ku taamaki vidole vya mtoto vimepondeka pondeka na kuharibika vibaya.......

Ikabid amchukue kumpeleka hospital baba alipokua hospital dokta akamwita akamwambia mzee kua vidole vimeharibika sana inabid vikatwe....

Alipo Rudi kumwona mwanae mtoto anatabasam akawa ana muuliza baba Ake......baba vidole vyangu vitaota lini.....mzee kusikia vile roho ilimuuma sanaa.....

Mzee akarud nyumbani akaenda Moja Kwa Moja kwenye gari lake.....kuangalia pale mtoto alipo kua ana scratch mtoto alikua ameandika...... I LOVE YOU DADDY

Hichi kitu kili muumiza sana mzee yule....

So tunajifunza THINGS A TO BE VALUED & PEOPLE TO BE LOVED

Mzee ange Fanya measurements & evaluation Yale yote yasinge tokea......the same Kwa huyo mwalimu mkuu huko wilayani Kagera......

Wasalaam
 
walimu mnajipa kazi si zenu, unapiga mtoto wa watu unapata pesa zaidi? Kwa nn usifanye ujasiriamali upate pesa ukafurahi na wanao?
 
Yaani ukifikiria vizuri kama ni adhabu wapewe tu adhabu ya aina moja na kama ni zawadi pia hivo hivo,
 
Back
Top Bottom