Yanayojiri leo katika maaadhimisho ya siku ya Walimu Duniani: Bukombe 2024

Yanayojiri leo katika maaadhimisho ya siku ya Walimu Duniani: Bukombe 2024

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Leo tarehe 11/10/2024 ikiwa ni siku pekee ya maadhimisho ya siku ya Mwalimu Duniani yanayofanyikia katika Wilaya ya Bukombe yakibebwa na kauli mbiu " WALIMU NI NYOTA INAYOANGAZA" yameanza muda huu huku kukiwa na kila aina ya shamrashamra za furaha.

Hakika, aina za "t- shirt" na rangi zake zimependezesha sana madhari hii ya ya shule ya Sekondari Ushirombo katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Mabango makubwa yaliyobeba picha ya Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ,Waziri Mkuu pamoja na Naibu Waziri Mkuu yamepamba sana jukwaa.

Mwitikio wa walimu ni mkubwa sana katika eneo hili huku wadhamini wakubwa CRDB na NSSF wakiacha alama zao katika maeneo tofauti tofauti. Walimu wana hamasa kubwa kusikia ujumbe utakaoletwa na viongozi huku wakitazama kauli mbiu Kwa dhati "WALIMU NI NYOTA INAYOANGAZA"

Muda siyo mrefu mgeni rasmi atapita kukagua mabada ya maonesho ya CRDB, LAKE ENERGY na ASAS. Mshereheshaji anaonekana kuiandaa hadhira vizuri kabisa kupokea ugeni huu adhimu.

Naam, Mheshimiwa mgeni rasmi Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa tayari ameshawasili ikiwa ni saa nne na dakika ishirini na Moja Asubuhi( 10:21 am).

Upekee wa Maadhimisho haya ni kuwa yameweza pia kuwakutanisha Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu katika hafla moja. Naibu Waziri Mkuu anakiri kupewa ushirikiano mkubwa sana pamoja na maelekezo kutoka kwa viongozi waliopo juu yake na pale anapokoseakosea ni yeye tu kushindwa kuelewa.
 
Back
Top Bottom