Chama cha Mapinduzi
Member
- Aug 8, 2013
- 10
- 33
Magufuli akiwa Arusha
Amesema ameguswa sana kutokana na mapokezi ya aina yake tangu alipokuwa akiingia mjini Arusha ameona majani ya masale yameinuliwa juu na hata hapo mkutanoni yapo, amesema anawapenda na ataendelea kuwapenda, na kwa sababu hiyo mapokezi hayo yatabaki na deni kubwa moyoni mwake la kuwafanyia kazi wana Arusha
Atakapochaguliwa kuwa Rais kwa awamu nyingine ameahidi kuwa atakuwa rais wa watu wote, wa watanzania wote, bila kuwabagua kutokana na vyama vyao, dini zao wala makabila yao.
Amesema mara yake ya kwanza kufika kwenye Jiji hilo la Arusha ilikuwa mwaka 1984, alikuwa kaenda kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, Kambi ya Makuyuni, na jambo moja analolikumbuka sana aliona maji mengi yakitiririka kila mahali na miti mingi ilikuwa imepambwa kwa rangi ya kijani na hiyo ilidhihirisha kuwa Arusha kuna maisha na leo nimekuta rangi hiyo hiyo ya kijani. Na kutokana na mapokezi aliyopata amesema inaonesha wana Arusha wamechoka kuchagua watu wenye Porojo.
Amesema mwaka 2015 alipofika hapo Arusha alikwenda kuwaomba kura akiwa kashatumika kwenye uwaziri kwa miaka 20 na walimpa kura za kumuwezesha kuwa rais lakini hawakuchagua wabunge na madiwani wa Kutoka CCM na hiyo alijua ni msalaba mkubwa sana na alipata shida sana na alijiuliza atafanyaje kupata "connection" ya kutatua kero za watu wa Arusha.
Amedai kuwa ili kuwezesha kazi zake ilibidi amteue Gambo kuw amkuu wa wilaya na kuwa mkuu wa mkoa ili kuwezeshesha shughuli za maendeleo ya wana Arusha.
Gambo alianza kumweleza matatizo ya wana Arusha na alimwambia akafanye kazi kama mkuu wa mkoa wa Arusha na pia kama mbunge wa Arusha pia na alifanya kazi.
Amesema Arusha hata wakati wa Utalii wazungu wanakaa hapo, Arusha hata vijana wanakaa, wakina mama na wakina baba wanakaa hapo, Arusha ni mji wa watu wanaopenda kujishughulisha.
Arusha ni watu wanaopenda maendeleo, Arusha ni watu wanaopenda maendeleo ndio maana akawaletea Gambo.
Amedai kuwa wana Arusha ni mashahidi kwa jinsi alivyokuwa akipambana na mbunge aliepita aliekuwa hapo akitekeleza miradi ya maendelo na mbunge aliepita alikuwa akipinga kwa sababu kazi ya wapinzani wakati mwingine ni kupinga kila kitu hata maendeleo ya watu waliowachagua.
Amesema Gambo hakumfukuza Ukuu wa mkoa wala aliekuwa mkuu wa wilaya hakuwafukuza, ila walitoka kwenye nafasi zao kwa kuwa walikwenda kugombea ubunge. Na kwa sababu chama cha Mapinduzi kinapenda haki akawaambia waachie nafasi zao. Hiyo alifanya kwa wakurugenzi, wakuu wa mikoa, na wakuu wa wilaya wote, na kwa bahati nzuri Gambo alimuomba na yeye akamjibu aende na Mungu amtangulie.
Amesema anashangaa kuna watu wanasema hampendi Gambo " Ningekuwa simpendi Gambo ningemrudisha jina lake hapa kuja kugombea?" Amesema wana Arusha kama wanataka maendeleo ya kweli "Kama mnataka maendeleo na mabadiliko ya kweli nileteeni Gambo aje Agambolile Arusha na maendeleo ya kweli".
Nataka niwatolee mfano, Arusha imetengenezwa kwenye mahali ambapo hakuna mito, Arusha kupata maji ni shida. Tulipopata fedha za kutekeleza miradi ya maji, wametengeneza miradi 1443 nchi nzima na mradi mkubwa wa kwanza ni wakutoa maji ziwa Viktoria kupeleka maji miko aya Tabora, tulipeleka Wilaya ya Nzega na Igunga, ambao umetumia zaidi ya trilion 1 point.
Na mradi wa pili ambao ni mkubwa wa maji katika nchi hii amabo unagharimu bilion 520 ni mradi wa Arusha, na alieuchokonoa na kumsumbua ni Gambo na atawashangaa sana wana Arusha kwa mtu aliewatetea malipo yao yatakuwa ni kumyima kura na atawashangaa sana wana Arusha na Ataishangaa Dunia.
Gambo amemsumbua mambo mengi hata kwenye barabara hiyo ya kilimita 14 ya njia nne barabara ambayo hakuna alietegemea itajengwa Arusha kwa watu waliomnyima kura ingeweza hata hiyo barabara wakaipeleka mkoa mwingine, Mji wa Arusha sasa unapendeza una mpaka taa za barabarani. Aliekuwa anamtuma kufanya hayo yote ni Gambo na amempeleka Arusha hategemei wamkatae.
Amewaomba wana Arusha kuwa maendeleo hayana chama na ndio maana alipeleka fedha kwa ajili ya mradi wa maji na anataka mwezi wa 12 maji yaanze kutoka hapo Arusha na kwa kuwa bado ni Rais anataka mkandaras aanze kufanya kazi usiku na mcna mwezi wa 12 maji yaanze kutoka.
Amewaasa wana Arusha kwa kuwaambi kuwa wamechelewa sana sababu wanatakiwa kuwa na watu wenye uchungu na nchi na wala wasiweke mambo ya Ukabila kwa kuwa ukabila haujengi na ameambiwa kuwa kampeni za Arusha zimeazna kuzaa ukabila. Kuingia kwenye ukabila itakuwa ni dhambi kubwa sana na kwa sababu baba wa Taifa aliliacha taifa bila ukabila.
Magufuli amesema ana mawazo mazuri na Arusha na anataka Arusha iwe ndio Calfonia ya Tanzania. Ameongeza kuwa hilo halishindikani na ndio maana maisha yake yoe amekuwa akihubiri amani na anawashukuru viongozi wote wa dini kwa kuhubiri amani na anataka waongeze watalii na watalii hawawezi kwenda kwenye nchi ambayo hakuna amani.
Katika kipindi cha miaka mitano wamefanya mambo yafuatayo, Kwenye huduma za jamii kwenye sekta ya afya wamepeleka xray mpya ya kisasa katika hospital ya Mount Meru, wamejenga hospatali za wilaya nne, Longido, Arusha jiji Karatu na Ngorongoro pamoja na kujenga vituo vya afya 4 na kukarabati nyingine 8. Miaka mitano ijayo watajenga hospitali zahanati na vituo vya afya na kuongeza watumishi, kujenga shule, elimu bure, Kuongeza ajira, kutoa bima za afya kutekeleza miradi ya maji.
Magufuli amemaliza kwa kuwaomba kura watu wote, wa vyama vote dini zote, kabila zote pia amemuomba kura mbunge aliemaliza muda wake Ngugu Godbless Lema wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.