Pre GE2025 Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Pre GE2025 Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ni Mbowe au Lissu

  • Mbowe

    Votes: 179 14.7%
  • Lissu

    Votes: 1,038 85.3%

  • Total voters
    1,217
  • Poll closed .

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Leo mbali na kuwa ni Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA pia wanasherekea Miaka 32 ya CHADEMA kupata Usajili wa Kudumu, ambapo ulipatikana Januari 21, 1993.

Mbivu na mbichi kujulikana leo, tumeona mengi na kusikia mengi kila upande ukitetea kwake. Je, nani ataibuka kidedea? Nani atatolewa kimasomaso na wajumbe?

Katika uchaguzi huu wajumbe watachagua Mwenyekiti Taifa pamoja na Makamu Mwenyekiti kwa Bara na Zanzibar, ambako ushindani mkubwa upo kati ya Mbowe na Lissu kwa nafasi ya Uenyekiti, na Wenje na Heche kwa nafasi ya Umakamu Uenyekiti.

1737406128366.jpeg

Je, ni Mbowe au Lissu? Ni Heche au Wenje?

Orodha ya Wagombea wote ni;

Mwenyekiti Taifa
  • Freeman Mbowe
  • Odero Odero
  • Tundu Lissu
Makamu Mwenyekiti Bara
  • Ezekia Wenye
  • John Heche
  • Mathayo Gekul
Makamu Mwenyekiti Zanzibar
  • Hafidh Saleh
  • Said Issa Mohammed
  • Said Mzee Said
  • Suleiman Makame Issa

Snapinst_app_474332647_18345511765194590_2423259377445939677_n_1080.jpg

Wagombea Wanatoa Salamu kwa Wageni Waalikwa na Wapiga Kura

Tundu Lissu

Lissu amshukuru Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe kwa kufanya nae kazi kwa kipindi cha miaka 20, licha ya kutofautiana kimitazamo lakini amekiri hawajawahi kugombana.

"Nimekaa pembeni ya Mwenyekiti wetu wa Chama mfululizo kwa miaka zaidi ya 20 na katika kipindi chote hicho hatajawahi kugombana, hatujawahi kupigana mimi na yeye binafsi. Ndio tumetofautiana kimsimamo lakini hatujawahi kugombani"

"Vyovyote itakavyokuwa leo, tutakuwa pamoja katika kukijenga chama chetu (Chadema)"

Freeman Mbowe

"Hiki chama tunawajibu wote wa kibinadamu na Wakimungu wakukilinda kwa gharama yoyote ile, na chama hiki hatutakiruhusu kwa gharama yoyote eti kwasababu pengine kura za mbowe hazikutosha au kura za Mhe. Lissu hazikutosha ama za Mhe. Odero yule mzee wetu wa kesho kuna mwanga kwamba kura hazijatosha".

"Uchaguzi huu usiwe vita unapashwa kuwa furaha ya ujenzi wa demokrasia"

"Wako watabiri wengi sana wamesema kuhusu uchaguzi wa CHADEMA, Mhe. Mbowe unaenda kukipasua chama, Mhe. Mbowe inakuaje, hawa ni wanademokrasia, wote kama mnavyowaona. Tofauti zetu kwenye mitazamo hii naamini tunakwenda kuizika mwisho wa kikao hiki tunanelea mbele stronger together"

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, ametoa taarifa kwa ufupi kuhusiana na hali halisi ya Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Urais wa mwaka 2020.

Mnyika asoma maazimio ya kamati kuu kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa (2024), ambapo yatapelekwa Mkutano Mkuu kwaajili ya kupendekezwa kupitishwa kama maadhimio ya mkutano mkuu wa chama.

Mnyika amehitimisha kwa kuwasilisha mapendekezo ya maazimio ya Mkutano Mkuu

Zoezi la uhakiki wa Wajumbe

Shughuli za uhakiki wa wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zinaendelea katika ukumbi wa Mlimani City.

Uhakiki huo unaongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na kukamilika kwake kutaashiria kuanza kwa uchaguzi wa nafasi za uenyekiti na makamu wa chama hicho Taifa.

Wajumbe 996 wathibitishwa ni halali, zoezi la kura kuanza.

Update

IMG_20250122_082953_937.jpg

Matokeo ya Uchaguzi Mkuu CHADEMA nafasi ya Mwenyekiti Taifa na Makamu Mwenyekiti

Awamu ya 1 nafasi ya Makamu Mweyekiti Zanzibar
Suleiman Issa alipata kura 67 sawa na 7%
Hafidhi Salehe alipata kura 241 sawa na 24%
Said Mzee Said alipata kura 301 sawa 30%
Said Isaa Mohamed alipata kura 388 39%

Wapiga kura waliojisajili 1014
Kura zilizopigwa - 1003
Kura halali 997, Habikika 6

Awamu ya Pili
Wagombea wawili baada ya mmoja kujitoa
Said Mzee Said
Kura zilizopigwa 706
Halali 700
Zilizoharibika 6
Za ndio 625 sawa na 89%
Hapana 75 sawa na 11%

Makamu Mwenyekiti Bara
Wapiga kura 1014
Kura zilizpogwa 1005
Halali 998
Haribika 7

Mathayo Gepgkul
Kura 49 5%

Ezekia Wenje
Kura 372 37%

John Heche
Kura 577 57%

Nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa
Wapiga kura jisajili 1014
Kura zilipigwa 999
Halali 996
Zilizoharibika 3

Odero Odero
Kura 1 0.1%
Freeman Mbowe
Kura 482 48.3%

Tundu Lissu
Kura 513 51.5%

Updates za Matukio
 
Wakuu,

Mbivu na mbichi kujulikana leo, tumeona mengi na kusikia mengi kila upande ukitetea kwake. Je, nani ataibuka kidedea? Nani atatolewa kimasomaso na wajumbe?

Katika uchaguzi huu wajumbe watachagua Mwenyekiti Taifa pamoja na Makamu, ambako ushindani mkubwa upo kati ya Mbowe na Lissu kwa nafasi ya Uenyekiti, na Wenje na Heche kwa nafasi ya Umakamu Uenyekiti.

Je, ni Mbowe au Lissu? Ni Heche au Wenje?

Duh!!!! Usiku wote huu hawajalala???
Kwani uchaguzi unafanyika usiku mnene kama vilinge vya wachawi????
 
Wakuu,

Mbivu na mbichi kujulikana leo, tumeona mengi na kusikia mengi kila upande ukitetea kwake. Je, nani ataibuka kidedea? Nani atatolewa kimasomaso na wajumbe?

Katika uchaguzi huu wajumbe watachagua Mwenyekiti Taifa pamoja na Makamu, ambako ushindani mkubwa upo kati ya Mbowe na Lissu kwa nafasi ya Uenyekiti, na Wenje na Heche kwa nafasi ya Umakamu Uenyekiti.

Je, ni Mbowe au Lissu? Ni Heche au Wenje?

Mbona mhombea mmojawapo hujamuweka nae ni Odero Odero?!
Mimi kama mjumbe naenda ODERO.
 
Wakuu,

Mbivu na mbichi kujulikana leo, tumeona mengi na kusikia mengi kila upande ukitetea kwake. Je, nani ataibuka kidedea? Nani atatolewa kimasomaso na wajumbe?

Katika uchaguzi huu wajumbe watachagua Mwenyekiti Taifa pamoja na Makamu, ambako ushindani mkubwa upo kati ya Mbowe na Lissu kwa nafasi ya Uenyekiti, na Wenje na Heche kwa nafasi ya Umakamu Uenyekiti.

Je, ni Mbowe au Lissu? Ni Heche au Wenje?

Tusubiri kukuche tufahamu mbichi na mbivu
 
Sote ni mashuhuda kwamba Freeman Aikaeli Mbowe anaungwa mkono na wajumbe wa mkutano mkuu wengi zaidi ya mgombea uenyekiti mwingine yeyote wa chadema, na kwahivyo anakwenda kushinda uchaguzi huu kwa kishindo.

Tayari visingizio kutoka kwa wapambe wa wagombea wanaowafungia wajumbe wao kwenye nyumba za kulala wageni, huku wakikosa kujua ratiba na kinachoendelea kwenye ukumbi wa uchaguzi, wameanza kupiga mayowe ya kushindwa, kanakwamba kuna rafu za uchaguzi hali ya kua wanajitakia wenyewe. Ni vichekesho na makusudi ya kujitakia tu, eti mpaka sasa kuna wajumbe hawajasajiliwa na hawana vitambulisho, wamefungiwa ndani tu.

Prof. Kitila Mkumbo amebainisha wazi kwa umma kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwmba, Freeman Aikaeli Mbowe hawezi kugombea nafasi ya uongozi ambayo hatashinda.

Ni muhimu sana wadau wa JF na wanachadema kwa ujumla, kuzingatia kauli hii ya kitaalamu kutoka kwa mwanafalsafa huyu wa siasa za Tanzania.

Kila la kheri wajumbe,
Kila la kheri Mbowe na Asanti Lisu kwa kushiriki uchaguzi wa chadema ngazi ya taifa.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom