Wewe nawe acha kudanganya watu kha! Maiti zinazokotwa kama ni wa Ethiopia ni aje wameshindwa kutambulika kwa utaifa wao sasa ndugu watoke Ethiopia kuja kuwatambua? Balozi ya Ethiopia ipo wamepewa hiyo taarifa?
Ben Saanane Chadema wamelizungumza hili jambo hadharani serikali ipo kimya Lissu ni vile alidhulumiwa hadharani mchana
Usiwadhihaki Wakenya wakati ukijua hata Tz Hali si shwari. Kenya Mungu awasimamie awaepushe na kikombe hiki! Tunawaombea!
Acha maneno yasiyokuwa na msingi, maiti zinazopatikana zinakuwa katika hali mbaya ya kutotambulika kwa sura, ndiyo sababu serikali inasema kama kuna watu wamepotelewa na ndugu zao waende wakatoe mate ili wapime vinasaba, ndiyo njia pekee ya kuweza kulinganisha na kuzitambua, nimekuambia dalili zinaonyesha kwamba si watanzania ni waethiopia kwa kuzingatia mambo mawili
1)Hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyejitokeza kupotelewa na ndugu au jamaa yake
2)Zile maiti za waethiopia zilizokuwa zikiokotwa kwa wingi porini, siku hizi hazipo tena huko porini, je zipo wapi na wakati biashara ya kuwavusha inaendelea?
Hii miili ilipokuwa ikiokotwa porini ilikuwa ikitambulika kwa sura zao, ila si rahisi hii ya baharini kwa sababu inakuwa imeharibika sana, hivyo sio rahisi kusema moja kwa moja ni wahabeshi wala watanzania.
Kuhusu Ben Sanane , Lisu na Roma, huko ni ukweli kuna kila sababu na ushahidi wa kimazingira kwamba serikali imehusika, kama ambavyo kuna kila sababu na ushahidi wa kimazingira vinavyoonyesha kwamba hii miili inayookotwa sio watanzania