LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Halafu baadaye israel akiendelea kuwaangamiza wapalestina mnakuja hapa kulia lia.
Sasa ulitaka Hamas wakae tu ili wanajeshi wa Israel wawauwe?
Israel anacho ambiwa ni afuate sheria za vita na sio kupiga piga hovyo kama ni kupambana apambane na hamas awaangamize kama anavyo sema na sio kuuwa raia.
 
Ewe Mwenyezi Mungu uliyeumba Mbingu na Nchi na Ulimwengu Mzima.
Ingilia kati kumaliza Mgogoro wa Israeli na Palestina.
Watoto wako wasio na hatia wanaangamia kwa kukosa Maarifa Kama ulivyo sema katika
Hosea 4:6.

Hosea (Hos) 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

Wajaalie Rehema Zako zisizo na Kikomo.
Walikumbuke Neno lako na kupata ufahamu na kupona.

Amen [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Aliyekua anachekelea vifo vya watoto huko Gaza, kuweka vibonzo na kukejeli na kushangilia vifo vya watoto huko Gaza kifo cha Gafla

Jamaa mmoja maarufu mitandao hususan huko X na mfuasi kindakindaki wa Israel wa mtandaoni aliyejipatia umaarufu kwa kuwacheka na kuwakejeli watoto wa Gaza na vifo vya wapalestina amefariki ghafla kwa Shambulizi la Moyo

Ni majuzi tu alitoka kupost mtoto wa Kipalestina aliyejeruhiwa vibaya kwa vita na kuandika maneno ya kejeli na kumuedit kwenye Tangazo la vipodozi huku akitia kejeli

Hili tukio lilisababisha hasira sana miongoni mwa maelfu huko hususan huko X akilaaniwa na kila mtu.

Amefariki kwa shambulizi la Ghafla la Moyo hii ndo inaitwa Karma kweli Mungu hachezewi, yuko wapi sasa?

Tujifunze sana kupitia hili.

 
Sasa ulitaka Hamas wakae tu ili wanajeshi wa Israel wawauwe?
Israel anacho ambiwa ni afuate sheria za vita na sio kupiga piga hovyo kama ni kupambana apambane na hamas awaangamize kama anavyo sema na sio kuuwa raia.
Nilishasema sana huku ila kwa kuwamnaongozwa na ushabiki siyo uhalisia, ndiyo maana mnaona vita ni kama kuchota maji mtungini na kunywa na kisha kumwaga yaliyobaki.
Vifo na majeruhi na kutekwa ni matokeo ya vita hasa vita ya kuvizia.
Vita ambayo adui yupo chini ya ardhi, anatoka tu pale anapotaka kutekeleza shambulizi.
Na kwa sasa ni hatari sana kwa Israel,kwa kuwa wapo katikati ya adui.
Ila mwisho wa siku lazima wa kushindwa awepo. Tulipogigana na adui anaeonekana juu ya ardhi lakini ndani ya ardhi yake tulishinda ila kwa hasara kubwa .
Hii vita Israel ataishida ila kwa hasara kubwa ,vifo vingi na majeruhi wengi.
Kuendelea kuvunja majumba ni kujaribu kuharibu maficho ya adui, mwisho wa siku adui ataonekana waziwazi na hapo ndipo atakaposhindwa.
Israel haishambulii watoto na wanawake kama mnavyodai kwa kutaka,ndiyo maana waliambiwa waondoke , lakini Hamasi kwa kujua ,kuondoka kwa raia katika maeneo hayo kuna athari kubwa kwao wakawazuia wasiondoke.matokeo yake ni hayo ya kufa.
Vita si nzuri hata kidogo.
 
Jeneral wa Jeshi la Urusi Bwana Andrei Gorolyov ambaye pia ni afisa mwandamizi huko Urusi amekiri kuwa kwa taarifa zake rasmi ni kuwa wanajeshi zaidi ya 500 wa Israel washaangamizwa hadi sasa!!

Jenerali wa Urusi Andrei Gorolyov [emoji635]: "Kulingana na taarifa zangu, idadi ya wanajeshi wa Israel waliouawa ni takriban 500." "Ufadhili wa Hamas unatoka Uturuki na Qatar, hiyo ni kweli.

Kwa sababu fulani, kila mtu anazungumza juu ya Irani, kwa hivyo lengo ni Iran? Wanataka kuiingiza Iran kwenye mzozo na kuishinda ili kulishinda taifa hilo?

. Katika miongo kadhaa iliyopita, Iran imepata maendeleo makubwa katika uzalishaji wa silaha za kisasa, na ndio maana hata aircraft carrier za kubebea ndege ya Marekani hawafurukuti lakini Wamarekani hawajali hasara na uharibifu utakaotokea.

Bali wanataka Israel kupigana na kila mtu, kwa hivyo tuko vitani na America na amani haitakuja.

BREAKING[emoji599][emoji599]: Russian General Andrei Gorolyov [emoji635]: “According to my information, the number of Israeli army personnel killed is about 500.” “Hamas’ funding comes from Türkiye and Qatar, that’s true.
For some reason, everyone is talking about Iran, so the target is Iran? They want to drag Iran into the conflict and defeat this republic.
Over the past decades, Iran has made serious progress in the production of modern weapons, and that is why the American aircraft carrier groups do not approach, but the Americans do not care about the losses and destruction that will occur.
Rather, they want Israel to fight everyone, so we are at war with the United States, and peace will not come. On Earth, there is only a multipolar world and the departure of the hegemonic power.”
 
UPDATE: Unconfirmed report.......Hii habari bado sijajiridhisha,nilikua na haraka sana kuipost, huwa najitahidi sana kuleta habari za kweli humu na huwa nahakikisha naleta habari za uhakika kabisa!!Na hii habari niliitoa kwenye source ya uhakika kabisa lakini mleta habari amesema binafsi kuwa anaifanyia uchunguzi kwanza na akaifuta!!....Hii ni hadi nijiridhishe kwanza nilikua fasta sana kupost hii habari humu, so hadi nijiridhishe....Mimi sio kama kina MK254 ambaye habari zake 95% anazoleta humu ni za uongo!!..........
 
Ufadhili wa nini?

Qatar anatoa posho tu kwa civilian wa Gaza

Silaha anatoa nani kwa millitary wing ya Hamas.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…