LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Hali unazidi kuwa mbaya Ukanda wa Gaza na sasa eneo hilo liko Gizani huku mapigano yakiendelea

Netanyahu asema atatumia silaha zake zote kuhakikisha anawaangamiza Hamas
Awaita Wapinzani kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa dharura

Israel yaita Jeshi lake la akiba kukaa Mguu Sawa

Source: Al jazeera news
 
Israel ana wanajeshi palestina ana magaidi kweli ukitakata kumuua paka mpe jina!
 
Hhhhh tukubali tu leo Israel kapokea kichapo, na kama sio air supremacy, wakelambwa wengi sana.
Sasa mzee unachagua silaha za kutumia 😁. Eti kama sio air supremacy, sasa si ndio maana ya jeshi lenyewe. Au ulitaka wapigane kizamani? Au ulitaka wakunje suruali na mashati wachapane makonde? Nadhani haujapata taarifa za hivi punde. Fungulia Al Jazeera uone vifusi huko Gaza
 
Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wetu Mpendwa Major General Ariel Sharon ( 1928 - 2014 ) alituachia Waisraeli huu Msemo wake wa Kishujaa usemao..."OUR DOCTRINE IS THAT THERE'S NO MISSION WE CAN'T ACCOMPLISH"... ambao ndiyo umekuwa Silaha yetu na Morali toshelezi Kwetu dhidi ya Wahuni na Wachokozi kama hawa Hamas wa Palestina, Iran na Lebanon.

Tumeshalipua tayari Ghorofa Kubwa lenye Wapalestina wengi na tumeshakamilisha Umafia wa Kuwakatia Umeme na sasa tunamalizia Kuiteka Rada yao ya Anga na Baharini ili kisitoke na kisijngie Kitu na baada ya hapo tunataka tutoe Funzo Tukuka kwa Wapalestina, Waarabu, Dunia na Wachokozi wote kuwa kama ambavyo ukiwa hapa JamiiForums hupashwi Kucheza na GENTAMYCINE basi hata hapa duniani pia hupashwi Kucheza na Taifa Teule la Mwenyezi Mungu la Israel.

Premier Netanyahu iteketeze Palestine.
 
Hawa ni watu wazima, waachwe wapigane mpaka waheshimiane. Wasiingiliwe wasiamuliwe, na hakuna kupumua. Atakayepigwa atamuheshimu mwenzake daima.
Lakini kila siku kuwaamua inatuchosha wengine. Makamera yoote yaangalizwe hapo alafu watwangane mpaka kieleweke.
 
Kila la heri kwenu
 
Toka ameondoka Mossad na baadae kufariki Meir Dagan kuna kujisahau kwingi sana pale Mossad.
Netanyahu asipokula kichwa cha Mossad Spy Chief wa sasa nitashangaa sana.

Huwezi kusema ni failure ya mossad moja kwa moja, pengine ni uhodari wa Hamas maana hawatumii tena simu ma device yyte ama text kwa mawasiliano yao. Wanawatumia watu wao kupeleka habari kutoka sehem moja hadi ingine bila ya wanao badilisha taarifa kuwa wanafahamiana.

Tangu Israel ijiindoe Gaza 2005, kumekuwa hamna ama ni wachache intel operative Kwenye hilo eneo kutoka mashirka mengi ya kijasusi duniani waliwepo Mossad.

Bado nakubalina na wewe kuna intelligence failure
 
Hivi hii ni vita kati ya Israel na Palestina au Israel na Hamas?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…