LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Endeleeni kuchinjana sisi tuna post tuu huku tukila porpcorn 😂😂
 
Nipo nasoma comments kidogo kidogo katika huu uzi kila napopata muda. Ila kiukweli mpaka sasa kwa muda mfupi ninaosoma huu uzi nakutana na baadhi ya vitu vya kushangaza sana.

Hivi haya maneno mnayatoa wapi?
Nabii Wa Allah Dawud (Amani iwe juu yake) yuko mbali na aliyosingiziwa na mashetani yaliyoandika maneno machafu kuwa alicheza mpaka akavua nguo. Matusi mabaya yaliyotungwa na watu waovu kuwasingizia Mitume wa Allah sio ya kweli. Na Allah atawalipa wanachostahiki mashetani wote waliotunga uongo na kumsingizia Mtume wake na Mitume wengine waliosingiziwa vitendo vichafu kama kulala na binti zao wa kuwazaa na kuzaa nao watoto au kulewa mpaka wakakaa uchi.

Na Waislam tuko mbali na haya unayojaribu kutusingizia. Mitume wa Allah na Manabii wake walikuwa ni watu bora kabisa na wasafi walioepushwa na machafu. Na wanayosingiziwa katika maandishi yaliyoko mikononi mwa watu wa kitabu ni katika maneno ya uongo yaliyoingizwa na watu waovu kabisa.

Na Qur'an imekuja kupambanua na kubainisha.

So huo uongo tena kuuhusisha na mawlid nimeshangaa. Hata hiyo Mawlid sijui kama unaelewa ni nini.
 
Jamani, maghorofa huko Ghaza yanapasuliwa na kuanguka kama kisu kinakata nyanya
 
Israel piga hao samaleko mpaka wamkubali Yesu kristo kuwa ni bwana na mwokozi wa maisha yao.
Nani alikwambia Waisraeli ni Wakristo

Wale wana dini yao ya Kiyahudi

Wakristo tusijipendekeze kwa hao Waisrael

Kwanza hawamwamini hata Kristo

Huwa nawashangaa sana Wakristo wenzangu ambao wanaona Israeli ni Wakrsito
 
Kuna video ilisambaa Jana ikiwaonyesha Hamas wakiuburuta kwenye gari mwili wa mwanamke binti mrembo kabisa ukiwa mtupu bila nguo wakidai ni mwanajeshi wa Israel kumbe yule dada ni raia mwema tu kutoka Ujeruman na alienda Israel kwenye music festival iliyokuwa inafanyika karibu na mpaka na Gaza..

Alafu Kuna watu wanatumia nguvu nyingi kuwatetea Hawa wajinga inashangaza sana.
 
Ratio huwa hivi - 400:2000.
Inasikitisha sana, wanapigana wakimalizika au wakipungua vya kutosha, wanakubali maridhiano, wanaanza kuzaliana upya wakifikia idadi ya kutosha wanaanzisha tena vita ili wapunguzwe tena, mtihani huu.
 
Wenyewe wanasema ni tukio baya zaidi kutokea kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita wewe mtwa mkulu unasema vikosi dhaifu vya kuvizia, watu wameingia border live kweupe wewe unazungumzia kama utani, situation ni ngumu huko.
Nitukio baya sana ila lilikuwa la maroketi. Kweli israeli hawajawahi kuuliwa kwa kiwango hicho hivyo ghadhabu itakayo wakuta mujehdini hawa watageuzwa majivu.
 
Nadhani jamaa alipandwa na mori wa kimisr akaona na yeye acontribute kidogo kwenye operation.
Ila wao jew akifa mmoja wanaona wamepoteza sana ila leo balaa kubwa limetokea mpaka big news Tatu zinatofautiana kwa takwimu sky news, BBC na Al Jazeera wanatoa takwimu tofauti tofauti
Ila Habari zingine ziko sawa kwa takwimu kama tetemeko la Afghanistan lililouwa watu 2053 kila news iko sawa

Huyo aliuwa kwa furaha zake tu zilizidi kifani akaona aongeze idadi na yeye
 
Najua ni ngumu kuweza kuamini, lakini nataka nikuhakikishie ya kuwa "Israel Presents Itself As Haven For Gay Community"

Ndilo taifa Mashariki ya Kati ambalo lilikuwa la kwanza kuhalisha mpaka mashoga jeshini mwaka 1989.

 
Huo ndo ukweli,jaribu kujisomea mzee. Jamaa ameelezea vizuri kabisa.
Kwamba Hitler ndio aliwatoa hao mayahudi katika ardhi ya Shaam? Kwamba Wapalestina hawakuwepo pale kabla ya kuanza vita kuu ya pili ya Dunia mwaka 1939?

Hao mayahudi wanatangatanga katika ardhi na miji huyo Hitler hajazaliwa na wala sio mwenye kutajika.
 
Msemo kama huo ilionekana ni kama ndoto ukiwalinganisha wapiganaji wa Hamas na jeshi linalosifika duniani la Israel.
Kwa sasa huo ndio ukweli ulivyo kwani zaidi ya masaa 24 bado wapalestina wakiongozwa na Hamas wameyashikilia maeneo ya kusini ya Israel wakiendelea kuyatetea yasirudi mikononi mwa taifa hilo kwa mara nyengine.
 
Ukraine kavamiwa ila hateki vibibi/vibabu vya kirusi, hateki vijana/mabinti wadogo wasiohusika na vita, haingii nyumba kwa nyumba kuua raia wasiokuwa na hatia bali anapambana na vikosi vya kirusi na miundombinu Yao, huoni utofauti?
Israel hua inafanya targeted killings Palestina na casualty hua inagusa mpaka bystanders
 
Hali ni mbaya sana huko aisee hao Hamas inaonekana walijiandaa na hii vita hizi mambo mara parachuti mara wameteka Waisrael sio ishu ndogo hii...hao jamaa ni watata sana aisee...
Kiuhalisia wamefanya surprise kubwa sana mpaka nashangaa nini kimetokea, halafu wao wana ile spirit ya ndani hawaogopi kufa na wamezoea kuona ndugu zao wakiteswa na kuuwawa, morali ya hapo sio ya nchi hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…