Yanayonikuta London, Uingereza - Part 2

Yanayonikuta London, Uingereza - Part 2

Rudi home utibiwe mkuu ushapigwa jini baya sana.....

Wazungu hawana ubaguz huo sema wew ndo upo na shida mkuu may be Black magic inakusumbua.......
Atakuwa anamatatizo huyu ya maradhi ya akili yanamuanza. Upweka nao alionao ni mtihani mwengine,rudi nyumba bro hutahitaji kwenda kwa daktari,mkusanyiko wa watu ni dawa tosha + ukipata mke.
 
Niliwahi kuandika hapa: Yanayonikuta London (UK) mwaka mwishoni mwa 2023. Baada ya hapo niliamua kukaa kimya na kuendelea kupambana yanayonikabili.

Lakini mambo yameendelea kuwa mabaya kwa upende wangu hapa London. I feel very bullied, tortured, mistreated by health care professionals na ndio kilichonisukuma kuandika hapa leo. Hii imekuwa inaniwia vigumu kumwelezea mtu ambaye hanijuwi akanielewa kwa sababu UK wanaoneka wanafanya mambo yao kwa kuzingatia human rights.

HISTORIA YA NYUMA:
Kutoa historia yangu fupi kwa wale ambao awatakuwa na muda wa kusoma thread yangu ya nyuma. Mimi nimeishi London kwa miaka mingi sasa. Mwaka 2016 nikiwa ninafanya kazi National Healthcare Services(NHS) nilianza ku experience bullying ambayo chanzo chake kilikuwa ni incorrect beliefs lakini kipindi hicho mitaani nilikuwa sijihisi kunyanyaswa. Katika ya mwaka 2022 nikaamua niache kazi NHS nitafute kazi nje ya sector ya afya. Lakini nilipoacha kazi baada ya muda mfupi bullying ikaanza mitaani sehemu ambazo nilikuwa nimeshaishi kwa miaka mingi bila tatizo.

Hapa nilijiona kama kuna watu ambao wamekuwa wakinifuatilia kichini chini na ku-organise na ku-encourage watu wafanye mambo ambayo yatajenga picha ya mimi kuoneka kama wao wanavyotaka. Na vile vile kuni break down kidogo kidogo. Hii walifanikiwa sana kwa monitor mawasiliano yangu yote, ku share locations zangu na pia nina hisi kusikiliza live conversations kupitia simu.

Mwaka 2023, nyumba niliyokuwa nina ishi nilianza kupata kama electrical shock na pia wakati mwingine kama sharp needle pain au zote kwa pamoja. Kwa kipindi hicho hii ilikuwa inatokea mara nyingi nikiwa kitandani nina jaribu kulala. Nika ripoti Polisi mara kadhaa na vile vile nikawa nina lala hotelini na hosteli kabla sija hama.
Fast foward, kwa sasa hivi hizi kama electrical shock and sharp needle pain, the intensity and frequency of ocurrencies have increased. Hasa kama nikiwa ninafanya baadhi ya vitu kama kuandika barua ya malalamiko zinakuwa more intense. Nina amini hisi ni wavelengths ambazo zinatumwa na baadhi ya kikundi cha watu.

KILICHONISUKUMA KUANDIKA HAPA LEO:
Tarehe 5 September 24, ninapoishi sasa hivi mfanyakazi alitaatifu kwamba kuna madaktari wawili wapo reception na kama nilikuwa nina taka waje chumbani au niongee nao kwenye ofisini downstairs. Nikamwambia nitakuja downstairs mazungumzo yafanyike ofisini. Lakini nilipofika reception doctor akanishawishi yafanyike chumbani kwangu ambacho nilikubali.

Hii ilikuwa ni assessment. Doctor ambaye alikuwa anaongoza hiyo assessment alikuwa anauliza haraka haraka na pia kuchanganya changanya. Maswali yake hayakuwa kwenye staili ya mtiririko wa topic moja baada ya nyingine. Na wala mazungumzo hayaku chukuwa muda mrefu. Lakini kwa sababu walikuwa very friendly sikuhisi chochote kibaya kwa wakati huo.

Tarehe 10 September 24. Nikapata ripoti ya hayo mazungumzo. Ilinistua kwa sababu ilikuwa kuna mambo mengi ambayo yalikuwa sio niliyosema.

For Instance, he asked if I believed in black magic. I responded that I do not believe in black magic and I think it is full of bushit. Na ilikuwa nikwa kifupi hivyo.

LAKINI, kwenye report yake yeye aliandika hivi "He spoke about other residents in the previous placements and how they might have place black magic on him." sijasema kitu kama iko na kilichonitia hasira zaidi miezi ya nyuma kuna watu walikuwa wanajaribu kunilisha maneno kihaina nikawaambia kwamba hayo mambo mimi sihamini kwa sababu ninaamini ni uongo.

Pia imetinia hasira kwa sababu wakati nina fanya NHS walianza kuni buli kuhusiana na haya mambo ya imani mpaka mimi kuacha kazi na baadae kukimbia nyumba nilikuwa nimeishi kwa miaka mingi kutokana na harassments. Hii ilinidhirishia nilichokuwa nina hisi kwamba baadhi ya wanao organise haya mambo dhidi yangu watakuwa wana nguvu fulani na reputation ya kuweza kuwafanya watu wafanye mambo yanayokihuka haki za binadamu na sheria.

Nimesha andika barua ya malalamiko kwnye Trust ya huyo doctor aliyekuwa anaongoza assessment na aliyeandika report lakini bado hawaja jibu.

Hii imenifanya nihisi maisha yangu yapo hatarini sana kama mpaka doctor ameandika mambo ya uongo ili kualalisha mambo fulani na pia ku cover bullying ninayopitia

Ninachohisi hawa watu walioko nyuma ya huu mpango wametumia mda mrefu, resources na pia pesa kutengeneza mambo ya uongo kwa hiyo hawawezi ku back down now. Wataendelea kusigini mpaka wanimalize.

Mkuu komaa hivyo hivyo wataaalamu wataitimisha una ugonjwa wa akili. Hivyo utakaa nyumbani na kulipiwa nyumba na matumizi yako yote. Wakikupa madawa yatupe chooni. Piga kazi pembeni, save money, rudi nyumbani.

Ulaya inahitaji kichwa kigumu kupambana na kutoboa kwenye taasisi, kazi yoyote.
 
NHS kuna mabaya yake lakini watu wanaogopa kuwa attack. Na pia mengi yanafukiwa bila kufika public. Mafano ile ya lucy Letby malalamiko yalianzia mda mrefu lakini yalikuwa yanafukiwa kwa chin . Mum of baby girl murdered by Lucy Letby thought nurse was an 'odd loner'

Pia Kuna hizi:

Yapo sana mkuu na tunayasikia kila leo
Dr Harold Shipman unamkumbuka alieuwa kijiji zaidi ya wazee 200
Sikatai haya na kila mahali yapo kuna watu wana roho za kishetani wao wanauwa mpaka vichanga kila leo na kulikuwa na kashfa kubwa ya watoto kutolewa viungo kabla ya kupewa wazazi
Ilikuwa kashfa kubwa sana iliyoivua nguo NHS
Ila hii ya hapa ni tofauti
 
Mkuu ilipa shida kufikia uhamuzi wa kirudi nyumbani kwa sababu hapa nimeishi zaidi ya nusu ya umri wangu.
Lakini sasa hivi nina subiri ubalozi wa issue emergency travel document
Kwani hauna british passport mpaka leo?
Kama umejibu hili acha nitulie tu sasa
 
Nyumbani pagumu hapo juu kuna sehemu amesema ½ ya umri wake ameishi London so kama ana 50 25 yote hajawahi kukaa hapa labda kutembea tu hivyo unaweza ukaona jinsi ilivyo ngumu kurudi kichwa kichwa.

Hii huwasumbua wengi sana waliosoma wakaondoka nje muda mrefu maana kuondoka halafu arudi kuanza from scratch bongo mtu anapagawa akili.
Kwa kuwa hana hata hati ya kusafiria huoni hapo kuna tatizo pia
Mtu kakaa 🇬🇧 nusu ya umri na leo anatafuta Lascia passare arudi home
 
Paranoid! hamna mtu anakuhaunt kiongozi, nani anawekeza kwnye mambo ya namna hiyo? Pick your mind and look what's wrong au nenda kwa wazee wako kakanyage ardhi ya baba na mama huenda umekaa nje sana ukasahau ulipotoka! I know what I am saying, nimehudumia watu wa namna yako wengi t
Na doctor kuandika mambo y uongo kwenye report yake paranoid?!
 
Rudi nyumbani jomba!

Umri umeenda na huoni future akili inakataa kuamini, lazima udate. We hujalogwa wala nini jomba, we una 'slesi'! Kwa lugha nyepesi umedata! Moja haikai mbili haikai. Ukiangalia wana uliowaacha bongo wa umri wako life limesonga wana familia nzuri, wamejenga, wana kazi stable, wanasukuma mandinga makali, mabata kama yote

Njoo tufuge nguruwe kerege huku.
Mambo ya kudai fulani kaniloga ndio nina pinga. Nina amini uchawi au uganga ni ujinga wa mwafrica na pia yanachangia sisi kuwa nyuma kimaendeleo.

Na ni hapo lipoandika kwamba doctor ameandika vitu vya uongo kwenye report yake.
 
Pole sana mkuu jaribu kurudi bongo kama inawezekana.
au kama haiwezekani hama jiji hilo.
lakini pia inaonekana unaishi mwenywe.

ila maelezo yako ni kama persecutory delusions, isijekuwa ni schzophrenic disorders
Ni hiyo doctor kuandika uongo kwenye repoti pia ni schzophrenic disorders!
 
Nyumbani pagumu hapo juu kuna sehemu amesema ½ ya umri wake ameishi London so kama ana 50 25 yote hajawahi kukaa hapa labda kutembea tu hivyo unaweza ukaona jinsi ilivyo ngumu kurudi kichwa kichwa.

Hii huwasumbua wengi sana waliosoma wakaondoka nje muda mrefu maana kuondoka halafu arudi kuanza from scratch bongo mtu anapagawa akili.
Ni kweli lakini lazima nirudi. Yanayondelea ni ukihukaji wa haki za binadamu. Doctor kuandika uongo ili ku maintain narrative hakuna kitu kibaya kama iko
 
Kwani hauna british passport mpaka leo?
Kama umejibu hili acha nitulie tu sasa
Mimi kutochukua passport ya hapa. Nikiangalia kwa jinsi mambo yalivyo naona ina msaada mkubwa sana kwangu. Ningekuwa raia wa hapa wange ninyanyasa ki sawa sawa. Lakini kuna mambo hawawezi bila kuihusisha Tanzania na pia wanajua saa yoyote ninaweza kuondoka kirahisi.
 
Hakuna cha bullying wewe una matatizo ya akili,Trustme nina ndugu yangu unayoandika hapa ni kama namsoma yeye,nenda katibiwe afya ya akili
 
Mkuu kuna siku nitaandika kwa undani yote. Kifanya hivyo sasa hivi kuna mambo mengine watu wanaweza kuona ni matatizo ya akili.
Hii kupata kama electrical shocks au sharp needle pain ni rahisi watu wengi kudikiria ni matatizo ya afya ya akili au kama ilo ulilosema hapo juu. Lakini kwangu mimi hii inahuhusiano na bullying. Ila kwa sasa hivi siwezi kusema zaidi ya hapo.
Incorrect beliefs - Hii wanaamini una dark spirit ambayo ina cause mambo kutokea. Hii miaka ya nyuma hapa UK walio kuwa wanaamini ni Wa Congo, Central na West Africa. Lakini wazungu ambao ni wabaguzi wameona ndio sehemu ya kututwanga na kututupia lawama lakini hawaweki wazi. Lakini nina uhakika miaka ijayo wataongea hazarani.
Hapo kweye bullying ndio ninaposhindwa kukuelewa ...nani anakufanyia bullying na kwa sababu gani? Na kuna uhusiano gani wa kufanyiwa hyo bullying na mwili wako kupata hayo maumivu? Haya ndiyo maswali yamekosa majibu ndio maana watu wengi wanakuona km una matatizo ya akili.
 
Mkuu pole kwa changamoto, je unahisi ni sababu ipi inapelekea watumie nguvu kubwa sana kukufuatilia maisha yako?
Kuna mambo mengi kwa hapa sina majibu yake ya uhakika. Na hihi imechangiwa na kufuatiliwa sana. Labda nikiwa nje ya UK ndio ninaweza kupata majibu.
 
Back
Top Bottom