Yanayonikuta London, Uingereza - Part 2

Rudi home utibiwe mkuu ushapigwa jini baya sana.....

Wazungu hawana ubaguz huo sema wew ndo upo na shida mkuu may be Black magic inakusumbua.......
Atakuwa anamatatizo huyu ya maradhi ya akili yanamuanza. Upweka nao alionao ni mtihani mwengine,rudi nyumba bro hutahitaji kwenda kwa daktari,mkusanyiko wa watu ni dawa tosha + ukipata mke.
 

Mkuu komaa hivyo hivyo wataaalamu wataitimisha una ugonjwa wa akili. Hivyo utakaa nyumbani na kulipiwa nyumba na matumizi yako yote. Wakikupa madawa yatupe chooni. Piga kazi pembeni, save money, rudi nyumbani.

Ulaya inahitaji kichwa kigumu kupambana na kutoboa kwenye taasisi, kazi yoyote.
 
Yapo sana mkuu na tunayasikia kila leo
Dr Harold Shipman unamkumbuka alieuwa kijiji zaidi ya wazee 200
Sikatai haya na kila mahali yapo kuna watu wana roho za kishetani wao wanauwa mpaka vichanga kila leo na kulikuwa na kashfa kubwa ya watoto kutolewa viungo kabla ya kupewa wazazi
Ilikuwa kashfa kubwa sana iliyoivua nguo NHS
Ila hii ya hapa ni tofauti
 
Mkuu ilipa shida kufikia uhamuzi wa kirudi nyumbani kwa sababu hapa nimeishi zaidi ya nusu ya umri wangu.
Lakini sasa hivi nina subiri ubalozi wa issue emergency travel document
Kwani hauna british passport mpaka leo?
Kama umejibu hili acha nitulie tu sasa
 
Kwa kuwa hana hata hati ya kusafiria huoni hapo kuna tatizo pia
Mtu kakaa 🇬🇧 nusu ya umri na leo anatafuta Lascia passare arudi home
 
Na doctor kuandika mambo y uongo kwenye report yake paranoid?!
 
Mambo ya kudai fulani kaniloga ndio nina pinga. Nina amini uchawi au uganga ni ujinga wa mwafrica na pia yanachangia sisi kuwa nyuma kimaendeleo.

Na ni hapo lipoandika kwamba doctor ameandika vitu vya uongo kwenye report yake.
 
Pole sana mkuu jaribu kurudi bongo kama inawezekana.
au kama haiwezekani hama jiji hilo.
lakini pia inaonekana unaishi mwenywe.

ila maelezo yako ni kama persecutory delusions, isijekuwa ni schzophrenic disorders
Ni hiyo doctor kuandika uongo kwenye repoti pia ni schzophrenic disorders!
 
Ni kweli lakini lazima nirudi. Yanayondelea ni ukihukaji wa haki za binadamu. Doctor kuandika uongo ili ku maintain narrative hakuna kitu kibaya kama iko
 
Kwani hauna british passport mpaka leo?
Kama umejibu hili acha nitulie tu sasa
Mimi kutochukua passport ya hapa. Nikiangalia kwa jinsi mambo yalivyo naona ina msaada mkubwa sana kwangu. Ningekuwa raia wa hapa wange ninyanyasa ki sawa sawa. Lakini kuna mambo hawawezi bila kuihusisha Tanzania na pia wanajua saa yoyote ninaweza kuondoka kirahisi.
 
Hakuna cha bullying wewe una matatizo ya akili,Trustme nina ndugu yangu unayoandika hapa ni kama namsoma yeye,nenda katibiwe afya ya akili
 
Hapo kweye bullying ndio ninaposhindwa kukuelewa ...nani anakufanyia bullying na kwa sababu gani? Na kuna uhusiano gani wa kufanyiwa hyo bullying na mwili wako kupata hayo maumivu? Haya ndiyo maswali yamekosa majibu ndio maana watu wengi wanakuona km una matatizo ya akili.
 
Mkuu pole kwa changamoto, je unahisi ni sababu ipi inapelekea watumie nguvu kubwa sana kukufuatilia maisha yako?
Kuna mambo mengi kwa hapa sina majibu yake ya uhakika. Na hihi imechangiwa na kufuatiliwa sana. Labda nikiwa nje ya UK ndio ninaweza kupata majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…