Yanayotokea bungeni Dodoma prof. Shivji alishayasema siku nyingi !

Yanayotokea bungeni Dodoma prof. Shivji alishayasema siku nyingi !

babayah67

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2008
Posts
493
Reaction score
79
Ndugu wana JamiiForum
Toka kuanza kwa vikao vya Bunge la katiba hadi leo hii tumeshuhudia yale yote aliyokuwa akiyasema Prof SHIVJI wakati nchi ikiwa kwenye maandalizi ya katiba mpyaa.

Katika Mhadhara wake wa kwanza juu ya masuala ya katiba mpyaa uliofanyika Nkhuruma Hall hapo Mlimani, Prof Shivji alipinga saana dhana ya wabunge waliopo bungeni sasa kuingia katika bunge la katiba kwa nyadhifa zao. Haya yanayotokea sasa ndio hayo tuliyoelezwa, lakini kwa upofu wa viongozi wetu wakapuuza ushauri wa nguli huyu wa Sheria.

Kinachotokea ndio matunda ya ubishi. Mabishano tulokwisha yaona hadi sasa katika kupitisha tu rasimu ya kanuni za kuendesha bunge sote tumeyashuhudia, sijui hali itakuwaje huko Mbele Rasimu ya Katiba itakapoanza kujadiliwa??? Ni dhahiri tutashuhudia mengi!!!!!

TUJIFUNZE KUKUBALIANA NA USHAURI WA WASOMI WETU, ITATUEPUSHIE MIGOGORO ISOKUWA NA LAZIMA!!!
HONGERA PROF SHIVJI, NAONA HUKO ULIPO UNAPOSHUHUDIA YANAYOTOKEA DODOMA UNATABASAMU KWA FURAHA
 
Ndiyo maana hata Prof. Lipumba alisema nchi kama France zilipoandika katiba yao waliweka masharti ya kuwa mjumbe wa bunge la kutunga katiba asiruhusiwe kugombea uongozi!! Hiyo kitu maCCM hawataki kusikia kabisa ............... ni bunge la kiini macho kwa ajili ya maslahi yao. Ni bora tukatangaza kuwa sisi ni sehemu ya North Korea ili tuelewe mmoja!!
 
Nakubaliana naye 100%. Maana kama ndio hawahawa tunategemea waje washike nafasi za uongozi ili kuitekeleza katiba hii wanayoitunga basi sio ajabu kuona leo waking'ang'ana kuweka vifungu ambavyo watakapokuwa madarakani visiweze kuwabana. Eeeh Allah hebu tunusuru wajawako na hii dhahma nzito.
 
mbona tumesha kosea tangu mwanzo et katiba upuuz mtupu katiba ya wanasiasa
 
Ndugu wana JamiiForum
Toka kuanza kwa vikao vya Bunge la katiba hadi leo hii tumeshuhudia yale yote aliyokuwa akiyasema Prof SHIVJI wakati nchi ikiwa kwenye maandalizi ya katiba mpyaa.

Katika Mhadhara wake wa kwanza juu ya masuala ya katiba mpyaa uliofanyika Nkhuruma Hall hapo Mlimani, Prof Shivji alipinga saana dhana ya wabunge waliopo bungeni sasa kuingia katika bunge la katiba kwa nyadhifa zao. Haya yanayotokea sasa ndio hayo tuliyoelezwa, lakini kwa upofu wa viongozi wetu wakapuuza ushauri wa nguli huyu wa Sheria.

Kinachotokea ndio matunda ya ubishi. Mabishano tulokwisha yaona hadi sasa katika kupitisha tu rasimu ya kanuni za kuendesha bunge sote tumeyashuhudia, sijui hali itakuwaje huko Mbele Rasimu ya Katiba itakapoanza kujadiliwa??? Ni dhahiri tutashuhudia mengi!!!!!

TUJIFUNZE KUKUBALIANA NA USHAURI WA WASOMI WETU, ITATUEPUSHIE MIGOGORO ISOKUWA NA LAZIMA!!!
HONGERA PROF SHIVJI, NAONA HUKO ULIPO UNAPOSHUHUDIA YANAYOTOKEA DODOMA UNATABASAMU KWA FURAHA

Ni kweli kabisa. Mabishano yanayoendelea ndani ya Bunge la Katiba hayana msingi na yanaegemea Vyama.
 
Kama mimi ningekuwa rais, ningelivunja bunge hili na kuitisha uchaguzi wa wajumbe wa bunge, harafu ningetunga sheria ambayo tume ya rais ya katiba iingie katika bunge hili kusimama upande wa serikali kujibu hoja za wajumbe kuhusu ibara mbalimbali. Lakini kwa unafiki wa wabunge maccm, walipendekeza tume ya warioba ivunjwe na kujipendekeza wabunge na wawakilishi kuwa wajumbe, na kupunguza idadi ya wajumbe wengine wa kuteuliwa, ni ubinafsi tu wa maccm na chama kinachowatuma
 
Kama jana jioni, Tundu Lisu akaamua kupasua live msimamo nadhani wa chama kuhusu hoja kinzani hapohapo Mbowe, Mdee wakasimama hadi Kificho akawaomba wakae chini na akaahirisha kikao. Hivi vyama na katiba ni sawa na kirusi.
 
Kwa kweli kwa hali inavyoonekani watanzania tupo ktk wakati mgumu sana katika mchakato wa kupata katiba iliyo bora' hizi hoja za kuanza kujadili kura ya wazi na siri kwa takriban wiki mbili kweli huu mchakato wa kujadili hii rasimu ya katiba itawagharimu miaka mingi xana. Wajadili yaliyo ya msingi kwanza ndipo yenye malumbano waunde tume huru kuyajadili kwa undani!!!
 
Back
Top Bottom