Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,251
- 22,929
Kwa mara nyingine tena Marekani imetuma wajumbe wa Baraza la Congress kwa ndege ya kijeshi hadi Taiwan tarehe 14 Agosti 2022.
Kwa kitendo hiki,Marekani inafanya uchokozi wa wazi kwa China. Ujumbe huu mwingine wa Bunge la Congress ulikwenda Taiwan kwa kutumia ndege ya kijeshi, moja kwa moja hadi Taiwan.
Wajumbe walio-kuwepo kwenye ujumbe huo ni Seneta Ed Markey (D-MA), Mwakilishi John Garamendi (D-CA), Mwakilishi Alan Lowenthal (D-CA), Mwakilishi Don Beyer (D-VA), Territorial Delegate Amata (R- American Samoa) .Wawakilishi hao walisafiri kwa ndege ya kijeshi hadi Taiwan kwa ndege ya Jeshi la Anga la U.S. Boeing C-40C. Ndege hiyo ilitua saa 8:04 asubuhi saa za Taiwan Jumapili.
Naibu Waziri Mkuu wa Taiwan Yui,alitoa makaribisho mazuri na ya kufana kwa rafiki wa muda mrefu wa Taiwan Sen. Markey na ujumbe wake wa vyama mbalimbali uliojumuisha Rep. Garamendi, Rep. Lowenthal, Rep. Don Beyer & na Rep. Amata."
Naibu Waziri Mkuu huyo wa Taiwan aliendelea kusema, "tunaishukuru Marekani kwa Wabunge hawa wenye nia moja na sisi kuizuru Taiwan.Tunashukuru sana pia kwa misaada isiyo yumba ya Marekani kwetu."
Hata hivyo bado haijajulikani kwa nini wajumbe hawa wa Congress wamechagua kwenda Taiwan wakati huu, hasa kwa vile suala hilo ni nyeti kwa Beijing. Ikumbukwe kwamba ni hivi majuzi tu Speaker wa Bunge la Congress Nancy Pelosi alizuru Taiwan, kitendo ambacho kilileta msuguano mkubwa kati ya Marekani na China.
Hizi inaelekea ni jitihada za makusudi kabisa za Marekani kuipinga Beijing kwa makusudi ya kuanzisha vita baina ya nchi hizo mbili, na hatimaye kui-ingiza Dunia katika sintofahamu nyingine tofauti na ile ya Russia na Ukraine.