Yanayotokea katika ulevi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
INAVYOTOKEA WAKATI WA UNYWAJI WA BIA

Chupa ya bia 🍾 ya kwanza huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo... Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

Chupa ya bia 🍾🍾ya pili, kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi....
Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Chupa ya bia 🍾🍾🍾ya tatu, huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana.... Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza.....

Chupa ya bia 🍾🍾🍾🍾ya nne, huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia..... bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Chupa ya bia 🍾🍾🍾🍾🍾ya tano, ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu......na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’
Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia chupa bia🍾🍾🍾🍾🍾🍾🍻 ya sita, na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. ....... ...Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.
Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika.......











 
Nimecheka sana [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huwa nawaza hivi siku nitakayoonja pombe itakuwaje?!

Ibilisi apite mbali, hiyo kitu nisijewaza kuilamba!
Jaribu tu, si mbaya kuiona kwanza namna ilivyo na kisha ufanye maamuzi ya ama kuendelea au kuacha kabisa. ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…