Yanga 2-0 Mbeya City | Ligi kuu NBC | Benjamin Mkapa

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Tukiendelea na hekaheka za kombe la dunia pia Ligi kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwenye dimba la Benjamin Mkapa ambapo Yanga anaikaribisha Mbeya City.

24' ⚽ Yanga inatangulia kwa goli lililofungwa na Fiston Mayele.

33' Moloko anajaribu lakini beki wa Mbeya City anaweka mguu na mpira unabadili mwelekeo. Yanga wanapata kona isiyoleta matokeo.

37' 🟡 Kayoko anamlambisha kadi ya njano Joseph kwa kumshusha chini Kibwana Shomari

38' Tuisila Kisinda anawekaaa mpira nyavuni, refa anapuliza kipenga kuashiria sio goli.

44' Mbeya city wanaingiza krosi maridadi na kumpita Diarra lakini shuti linapaa juuuu

45+2' Mapumziko

49' Mpira umerejea kutoka mapumziko na unachezwa zamu kwa zamu

78' ⚽ Mayeleeeeee, anamalizia krosi maridadi kutoka kwa Moloko. Yanga 2-0 Mbeya City

90' Mpira unatamatika dimba la Benjamin Mkapa. Keki yenye namba 49 inatawala uwanjani
 
Wakati Simba wakinufaika na goli la offside Juzi, Leo Yanga wananyishwa goli halali kabisa hapa refa anadai ni offside..

Paka hapo ushajua nani anagawa bahasha

Bongo hata Yanga anagawa bahasha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…