Yanga: A case Study

Mario Kejob

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2020
Posts
441
Reaction score
536
Maamuzi waliyochukua Yanga yatakuja kuwagharimu siku za usoni ya kuwataka TFF kufuata kanuni kwa asilimia mia moja. Ipo siku Yanga watakuwa na dharura ya kweli kwa mfano kupata puncture au flat tire wakati wanakwenda uwanjani na hivyo kuwapigia simu TFF kusogeza mchezo mbele kutokana na dharura hiyo, hapo ndipo Yanga watajua what goes around comes around.

Maamuzi haya yatakuwa kama boomerang na kuwapiga wao wenyewe pale TFF itakapo wajibu kwamba kanuni hairuhusu na wanahitaji masaa 24 kufanya hivyo.

Delay na postponement ni vitu viwili tofauti. Si amini kuwa delay ya game inahitaji notice ya masaa 24 ila postponement ndiyo inahitaji. Je? Mchezaji wa Yanga akipata ajali na kufariki siku ya mechi, Yanga watawajibika kucheza mechi siku hiyo? Si wataomba mchezo uahirishwe!

Hapo masaa 24 watayatoa wapi? Na hiyo timu pinzani ikifanya kama walivyofanywa Yanga, si tutakuwa tunaliua soka letu! Na kwa mantiko hiyo basi; Yanga hawakutaka TFF itii agizo la serikali ili mchezo uendelee katika muda awali?

Masikini washabiki na wapenda soka wa nchi hii waliojazana uwanjani kwa maelfu, gharama zao na muda wao nani atawalipa?
Upo uwezekano wa CAF na FIFA kuingilia kati suala hili, nani atajibu hoja zao? Na kama kutakuwa na penalties, nani atalipa?
Jamani tuwe tunachukua maamuzi ya busara kwa faida ya maendeleo ya soka letu na nchi yetu kwa ujumla.

Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu, hili litakuwa ni " tukio rejea" la matukio kama haya yakayofuata siku za usoni. Hivyo, maamuzi yoyote yatakayotolewa yazingatie haki, sheria na kanuni ili tusije ku-set a bad precedent kwa timu nyingine kufanya hivyo baadae ikizingatiwa kuwa timu zote zina haki sawa.
 
Shida pale yanga viongozi wamefeli, walichofanya Jana ni very unprofessional, na ni kwa sababu tu ni yanga ila ingekua ihefu ingeshapokonywa points na kushushwa daraja. Hakuna timu iliyo juu ya chama cha soka. Soka letu tunalidumaza wenyewe kwa kuruhusu viongozi waliokosa weledi kuongoza timu zetu
 
Kwani wewe ulitaka je, usipende kuishi kwa kubembeleza, fuata kanuni na sheria mda wote.
No kubebwa.
 
Nianze na wewe mleta uzi, tulio wengi tunalilia utawala wa sheria na haki, ukianza kuwazakutumia busara kwa sheria ili ipindishwe,tutaendelea kulia maana watakwambia wanatumia busara. Utaratibu mda mwingine unachelewesha,lakini ndivo inatakiwa.
Fuata sheria na kanuni.
 
Hata yule kwenye uzi wake aliesema alikunya juu ya kitanda lodge ni shabiki wa yanga
 
JIBU KWANZA KWANINI MIKIA WALIKIMBIA MECHI WAKAINGIZA TIMU SAA 12.30 JION KWENDA KUFANYA NINI
 
Hujui kitu...an analysis which is biased to the core
 
Ni kweli what goes around comes around.Kuna siku yanga watapata dharura mfano ya kufiwa,au chochote kile,sasa kama kanuni inasema kusogeza mbele muda ni kuahirisha,timu pinzani ipewe haki yake.

Nawashangaa wachambuzi taka taka wanavyoi support yanga kwa ujinga waliofanya
 
Mkuu umezungumzia dharura ambazo umezitaja kabisa,hivi juzi kipi kilifanya mechi isogezwe mbele?dharura gani has a hebu itaje kama ulivyotaja hapo kwa Yanga kufiwa n.k
 
Watanzania fuateni sheria na taratibu zilizowekwa rasmi mtakuwa salama wakati wote.
 
Acheni upumbavu na ushabiki usiokuwa na maana,kwa hiyo siku ya mechi Simba alipata ajali au alifiwa?

Fikilia leo Simba ilitakiwa kucheza,
lakini kwa sababu ligi inaendeshwa kisiasa mechi imeahilishwa,

Mfano Man City alikuwa anashiliki vikombe vinne kwa wakati mmoja,mpaka Sasa Hana kipolo hata kimoja , Man City ndiyo amezipita mchezo mmoja timu ambazo hazina maahindano mengi

Timu ya Yanga miaka ya nyuma ilikuwa na vipolo 8 eti sababu inashiriki mashindano ya kimataifa, ligi gani Duniani ilishaona timu inavipolo 5 Kama siyo Tanzania peke yake?

Na Yanga haitakiwi kupeleka timu uwanjani,labda Simba na TFF wapeleke timu zao,alafu tuone nini kitatokea?

Waziri mkuu anasimama Jana na kutoa maelekezo kwa Wizara ya michezo ,lakini hasemi sababu ya kuahilishwa kwa mchezo,
Anashindwa kutofautisha Serikali na mpira ni vitu viwili tofauti,Ndiyo maana mambo ya mpira Yana mahakama zake.
 
Yanga ni brand kubwa kuliko TFF
 
Mfano Man City alikuwa anashiliki vikombe vinne kwa wakati mmoja,mpaka Sasa Hana kipolo hata kimoja , Man City ndiyo amezipita mchezo mmoja timu ambazo hazina maahindano mengi
Hata Simba isingekuwa na kiporo kama nchi nzima miji inakochezwa ligi kuu kungekuwa na viwanja vya ndege, na pia timu zinazokuja kucheza na Simba hapa Dar zingekuwa na uwezo wa kupanda ndege. Fikiria labda Jumapili Prisons ya Sumbawanga icheze mechi na Kagera Sugar hapo mjini Sumbawanga. Je, ina uwezo wa kupanda ndege kuja Dar kucheza na Simba siku ya Jumatano? Kwa kuzingatia uchumi wa timu za ligi ya Bongo, kwa vyovyote lazima uweke gap la kutosha kuruhusu timu kusafiri walau kwa bus, kwa hiyo viporo vya Simba usilinganishe na vya Man City, kule Uingereza na Ulaya kwa ujumla kila mji una airport na kila timu inamudu kutumia usafiri wa anga
 
Dharura ilikuwa maelekezo ya serikali
Mkuu umezungumzia dharura ambazo umezitaja kabisa,hivi juzi kipi kilifanya mechi isogezwe mbele?dharura gani has a hebu itaje kama ulivyotaja hapo kwa Yanga kufiwa n.k
 
Huu ndy upumbavu tusioupenda,
Kanuni zimetungwa na tff vilabu na wadau, Sasa kwanini zisifuatwe.
Kwanini hamtaki kuongozwa na sheria?
 
Huu ndy upumbavu tusioupenda,
Kanuni zimetungwa na tff vilabu na wadau, Sasa kwanini zisifuatwe.
Kwanini hamtaki kuongozwa na sheria?
Nakubaliana na wewe kwamba kanuni zinapaswa kifatwa, lakini hupaswi kuwa rigid kwenye vifungu kwa sababu kuna dharura, hasara iliyosababishwa na maamuzi ya viongozi wa Yanga ni kubwa mno. Narudia tena soka letu linaharibiwa kwa vilabu vyetu kuendeshwa na watu waliokosa weledi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…