Yanga acheni tabia za kuwaza ushirikina kila mnapobanwa mbavu!

Yanga acheni tabia za kuwaza ushirikina kila mnapobanwa mbavu!

Mkuu itakuwa wewe ni mshirikina. Kwa nn utoe hitimisho kuwa kwa kitendo hicho cha wachezaji wa Yanga kutikisa nyavu wanaamini ushirikina.
Baada ya hapo wakaenda kuchukua taulo la golikipa,nalo pia wakalikung'uta kama wanatafuta kitu kwenye hilo taulo!
Kwenye mchezo wa soka labda tuseme walikuwa wanatafuta nini?Filimbi ya mwamuzi au mpira ulipotelea kwenye taulo?
 
Leo nimeshangaa sana Kaseke na mwenzake kwenda goli la mpinzani kuanza kutikisa nyavu kama wanatafuta kitu hivi kwa chini,baadaye wakaenda hadi kwenye taulo la golikipa na kulikung'uta!Nilipigwa na butwaa kuona hivyo!Wakati huo Matokeo yakiwa Prison 1-0 Yanga na Yanga walikuwa wakishambulia sana!
Hii tabia si nzuri hasa kwa timu inayoshiriki ligi kuu na Club kubwa kama Yanga!Mnatia aibu kwakweli na hii sio mara ya kwanza ninyi kufanya hivyo!
Prison mnalingana nguvu maana kwenye mechi ya kwanza mlitoka sare tena kwenu!Sasa mnachoshangaa ni nini wao kuongoza kwa goli moja na ninyi mkiwa mnakosakosa?
Aibu kwenye michezo,mechi zinaonekana mpaka nje ya nchi halafu mnafanya ujinga!Shwain kabisa!

Siku nyingine mkagoma kuingilia lango la kuingia uwanjani,ninyi watu gani?Mbona mnaupa sana promo ushirikina?

Nawatakia kheri ya mwaka mpya!
Timu ya kishirikina, wachezaji washirikina na mashabiki washirikina. A.K.A VIGAGULA

Sent from my SM-N910F using JamiiForums mobile app
 
hivi na ile tabia ya golikipa kuushika mpira uliotengwa kwa ajiri ya kupigwa penati inamaanisha nn. Au ni ushirikina pia.
 
Timu ya kishirikina, wachezaji washirikina na mashabiki washirikina. A.K.A VIGAGULA

Sent from my SM-N910F using JamiiForums mobile app
Halafu kuna jamaa anashupaza shingo hapa eti ni jambo la kawaida!
Hawa jamaa wakienda kwa waarabu wakapigwa 5-0 watavumilia kweli kama kamoja tu wakaanza kutafuta hirizi?
Bora wabaki hapa hapa aisee!
 
makanjanja ya utopolo redioni na mwanaspoti gazeti hutakaa usikie yameongelea hili ila ingekuwa simba mama yangu weeeeeeee
 
upo lakini siamini kama unafanya kazi kwenye soka. Coz kama ungekuwa unasaidia maybe Africa kuna nchi ingekuwa imewahi miliki kombe la dunia.
Ok, ndio maana tuko hapa tunakemea kwa sababu na sisi tunaamini kama wewe unavyoamini kuwa haufanyi kazi. Ila kaseke anaamini kuwa goli linaweza lisiingie sababu ya vitu kufukiwa langoni au kuvilingishwa kwenye taulo, na uthibitisho wa haya ni kwa sababu alionesha kutokuwa na imani na taulo na posts baada ya kosa kosa ya goli.
 
Nasikia Kuna mchezaji mmoja mechi ya Yanga vs Simba ya 2-2 alikamatwa na hirizi uwanjani, sijui Nani yule nimemsahau kidogo jina...
 
Nasikia Kuna mchezaji mmoja mechi ya Yanga vs Simba ya 2-2 alikamatwa na hirizi uwanjani, sijui Nani yule nimemsahau kidogo jina...
Acha unazi usio na maana,kuvaa vitu hatarishi huwa hairuhusiwi!Sasa unaenda umevaa cheni au bangili ambazo sio plastic ukionekana lazima uzuiwe!Hizo kawaida hata ulaya tunaona,ila hii ni kali zaidi!Au ile hutaki kuingia uwanjani kupitia lango kuu,unapitia kwenye vichochoro,khaaaaah!
 
Leo nimeshangaa sana Kaseke na mwenzake kwenda goli la mpinzani kuanza kutikisa nyavu kama wanatafuta kitu hivi kwa chini,baadaye wakaenda hadi kwenye taulo la golikipa na kulikung'uta!Nilipigwa na butwaa kuona hivyo!Wakati huo Matokeo yakiwa Prison 1-0 Yanga na Yanga walikuwa wakishambulia sana!
Hii tabia si nzuri hasa kwa timu inayoshiriki ligi kuu na Club kubwa kama Yanga!Mnatia aibu kwakweli na hii sio mara ya kwanza ninyi kufanya hivyo!
Prison mnalingana nguvu maana kwenye mechi ya kwanza mlitoka sare tena kwenu!Sasa mnachoshangaa ni nini wao kuongoza kwa goli moja na ninyi mkiwa mnakosakosa?
Aibu kwenye michezo,mechi zinaonekana mpaka nje ya nchi halafu mnafanya ujinga!Shwain kabisa!

Siku nyingine mkagoma kuingilia lango la kuingia uwanjani,ninyi watu gani?Mbona mnaupa sana promo ushirikina?

Nawatakia kheri ya mwaka mpya!
Kutingisha nyavu ndio uchawi? Au wewe ndio mchawi mkuu ?
 
Kitu kafanya kaseke, sasa unahusishaje Yanga yote?
Mbona Kaseke alikuwa akifunga goli mnasema Yanga imepata goli. Mfano mechi na Azam alifunga Kaseke na goli pekee mkasema Yanga imeshinda. Utopolo bana. Kitu kinapofanywa na mchezaji au shabiki au kiongozi tena amevaa nembo ya timu hiyo ni timu imefanya na si vinginevyo.
 
watu mnapofeli ni kujifanya hamuamini ushirikina mbele za watu ilhali juma ya pazia ni wachawi wakubwa...
 
Back
Top Bottom