Yanga aibu gani hii: Naona imefungua akaunti ya kuomba michango kwa mshabiki

Alafu wewe bwana, timu ina mashabiki milions alafu unafikilia michango? Man united ina mashabiki bilion hawajafikilia hayo. Akili zetu za kiTanzania ni mzigo. Kama Yanga hawana biashara yoyote inayoweza kuwalipa kwa mtaji wa hao mashabiki milioni sita basi ni wakupuuzwa
 
how was MANU in 1840something, usiione MANU ya leo ukafikiri ilianza ikiwa hivyohivyo tu. Mazingira yetu ya soka na uchumi kiujumla hayaruhusu mambo kufanyika kama England au Europe kwa ujumla wenzetu viwanja vinaingiza watu elf70 na kwa kiingilio cha paundi40 ambacho ni karibu TZS120,000/= na viwanja vinajaa, hapa wakiweka kiingilio cha TZS20,000/= sisi haohao ukiwemo wewe tutapiga kelele sana, Investors kwenye soka hawapo nchi zetu hizi kulingana na biashara zao haziwaruhusu kutapanya mapesa mpaka huko kwani haitawalipa. leo tunafurahia sana chanel za bure, hatutaki kulipia kuangalia matangazo ya TV,sasa AZAM atailipa timu kiasi gani ili apewe haki za kuonyesha mechi za timu husika?. Angalia klabu zenye mafanikio kama TP mazembe haziendeshwi kiuchumi kama MANU klabu inategemea tajiri mmoja tu!!. Kwa hiyo ndugu yangu kuendesha timu nchi hii ni ngumu sanasana, ukifananisha na MANU sio timu tu na viongozi wake ndio wabadilike ni jamii yote inahitaji kubadilika!!!!
 
kwa mfano biashara nyingi sasa hivi inaenda online, he vilabu vya Tanzania vimeshafikiria kitu kama drop shipping ambapo kwa washabiki wengi hao wa Yanga ingeweza kuwafikishia bidhaa zao kirahisi sana!!
 
Kumbuka hapa pia tunaiongelea yanga ambayo ipo tangu miaka 1930, usisahau hiyo. Unaiongelea yanga as if ni timu iliyoanza miaka ya 2000, tatizo lipo hapo. Sasa kama unaamini hao mashabiki wanaweza kutoa michango kwa nini usifikilie hiyo pesa unayoihitaji kwa michango usiipate kwa njia ya biashara? Yaani mnafika hatua mnashindwa kutumia media kuhamasisha watu wanunue brands za timu yenu then mnatumia same platform kuwahamasisha michango. Jibu ni moja tu, vionhozi wa hovyo, wanajua kabisa runing business inahitaji skills na hawataki kuangahika na hilo. Kukusanya michango hata machokolaa wa posta wanaweza, i doesnt need any skills na ndicho viongozi wenu wanaweza, ukizingatia sio rahisi kukagua matumizi.
 
unaongea fact mzee baba, wanaibisha sana wachezaji wanapowachoresha kwenye TV wakiombaomba
 
Yaani tuchangie sisi mashabiki na wanachama wa yanga alafu aibu uone wewe mbumbumbu,

ona kwanza aibu kwa timu yako iliyopigwa goli 10 katika mechi 2
 
Ndugu yangu nimesema yanga kama yanga ama simba haitaweza kufurukuta katika uchumi kama jamii(Society) haitaweza nayo kubadilika hata kama wajerumani wakiwasaidia kuprint hizo jezi at zero cost. kwani timu zetu hazijawahi kufanya hivyo?!?, kila siku unawasikia wanalalamika kuhusu kubumbwa kwa jezi zao, halafu kumbuka purchasing power ya mashabiki wa timu zetu,je wanauwezo wa kununua jezi hata kwa elf50? nani wangapi watakuwa na uwezo huo?, kwa nini usiwaombe mchango wa elfu mojamoja ambayo wana uwezo nayo kuliko kuwategemea kwenye kitu ambacho hawataweza?. Labda nikubaliane kwamba kuna udhaifu kwenye promotion. tukiwekeza kwenye kuziingiza klabu zetu kwenye mioyo ya mashabiki wao wakahamasika kuchangia YANGA na SIMBA zinaweza kubadilika kabisa.angalia tu mapato yatokanayo na mechi, utawalamu viongozi bure lakini watu hawana uwezo wa kulipa fee ya kuingilia viwanjani tena ukiweka kubwa ndio balaa.Hivi hata wewe nikuulize unaweza kwenda kununua jezi ya timu yoyote hapa TZ kwa USD150?, kwa sababu to cover the cost kwa brand zuri lazima bei ianzie mahali fulani sasa ni wangapi wenye uwezo huo?!?.Mimi naona Yanga wako kwenye right truck isipokuwa wainvest kwenye kuipeleka timu mioyoni mwa mashabiki wao. Hata kwa sasa timu inaendeshwa hivyo na mafanikio unayaona,ukilinganisha na timu inayopata billions kutoka kwa investor, bado yanga wana deserve pongezi. Wajameni kama tunapenda maendeleo ya soka nchi hii na wewe hapo ulipo timiza jukumu lako, si kulaumu viongozi tu.
 
Bosi mimi naongelea by experience, kwa kuwa unahisi hicho kitu hakiwezekani, na viongozi wanahisi hivyo vitu haviwezekani but kuna watu wanaingiza mamilioni mengi kupitia brands za hao, wale washabiki wa yanga na simba wanaovaa jezi za yanga na simba wanazinunua wapi? Inawapa faida gani? Unakumbuka mbeya city? Ilifanya uhamasishaji kununua jezi zao, walitengeneza wenyewe jezi za kutosha na ziliuzwa kama njugu na waliingiza pesa, sasa unaongelea simba na yanga? Wewe unafikili Mo anaigombania simba akiamini atapata hasara? Unaongelea purchasing power? Ya wapi unayoijua wewe, yaani sasa hivi washabiki wa yanga wananunua jersey za al haly tena og ili akaishangilie agaisnt simba, really? Ndio huyo unayemwona kama hana purchasing power? Tatizo tunaviongozi waliofeli, hawana vision.
 
Hawezi kukuelewa huyo, unapoteza muda wako buree.
 
Mfumo rasim wa kuendesha klabu kama vile mfumo wa kampuni huwa hakuna mianya ya upigaji ndio maana hawataki Yanga iwe kampuni

Wanaendelea na mfumo huo wa kuomba omba ili waendele kula pesa za wajinga

Mimi Yanga lakini hata shilingi kumi sichangii maana hakuna cha maana kitacho fanyika
Sent using Jamii Forums mobile app
 


Yanga = Watoto wa Mze Malecela, wagogo wa Jangwani (hili ndilo jina lao kwa siku hizi).
 
enyimba inaendeshwa kwa michango ya wanachama na ni bonge la timu africa, al ahly iliyowapiga hamsa inaendeshwa na wanachama, asec mimosas, canon younde, al hilal sudan zote hizo ni timu za wanachama...

yanga ni timu ya wanachama.. na imeanzishwa na wanachama.. so inapofata misingi yake.. iheshimiwe..

dewji anaibia watanzania.. anajimilikisha mashamba anakopea... nchi itauzwa hii.. analipa watanzania mshahara laki moja kwa mwezi kwenye kampuni zake...nyinyi mikia mna muona Mungu mtu... ngoja siku aje akopeee na simba iwekwe bondi iuzwe na bank... ndipo mtajua muhindi sio ndugu yako...





 
Manji atarudi tu.Wapiga magoti wanaumia lakini ukisimama tu msaliti.Lazima upige magoti mpaka yatoke damu.
Ujinga uliopitiliza timu ina udhamini wa bilioni 1 wa Sports Pesa lakini mapopoma wanashindwa hata kulipa wachezaji mishahara. Hakuna mwenye akili hata ya kujiuliza!
 
Kuna mjinga anadai muhindi sio ndugu yako!
Hivi Manji msambaa?
Ujinga mwingine hauna mipaka. Kuropoka tu.
Mnayempigia magoti ni nani?
 
Tembea ukiona kikapu kinapitishwa tupia mchango wako.
Wasiliana na wenzako ili kuchangia timu yenu lakini usiulize bilioni moja ya udhamini wa Sports Pesa zinakwenda wapi?
 
Ngoja waendelee kuibiwa OMBAOMBA zao
 
Reactions: Tui
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…