Ndugu yangu nimesema yanga kama yanga ama simba haitaweza kufurukuta katika uchumi kama jamii(Society) haitaweza nayo kubadilika hata kama wajerumani wakiwasaidia kuprint hizo jezi at zero cost. kwani timu zetu hazijawahi kufanya hivyo?!?, kila siku unawasikia wanalalamika kuhusu kubumbwa kwa jezi zao, halafu kumbuka purchasing power ya mashabiki wa timu zetu,je wanauwezo wa kununua jezi hata kwa elf50? nani wangapi watakuwa na uwezo huo?, kwa nini usiwaombe mchango wa elfu mojamoja ambayo wana uwezo nayo kuliko kuwategemea kwenye kitu ambacho hawataweza?. Labda nikubaliane kwamba kuna udhaifu kwenye promotion. tukiwekeza kwenye kuziingiza klabu zetu kwenye mioyo ya mashabiki wao wakahamasika kuchangia YANGA na SIMBA zinaweza kubadilika kabisa.angalia tu mapato yatokanayo na mechi, utawalamu viongozi bure lakini watu hawana uwezo wa kulipa fee ya kuingilia viwanjani tena ukiweka kubwa ndio balaa.Hivi hata wewe nikuulize unaweza kwenda kununua jezi ya timu yoyote hapa TZ kwa USD150?, kwa sababu to cover the cost kwa brand zuri lazima bei ianzie mahali fulani sasa ni wangapi wenye uwezo huo?!?.Mimi naona Yanga wako kwenye right truck isipokuwa wainvest kwenye kuipeleka timu mioyoni mwa mashabiki wao. Hata kwa sasa timu inaendeshwa hivyo na mafanikio unayaona,ukilinganisha na timu inayopata billions kutoka kwa investor, bado yanga wana deserve pongezi. Wajameni kama tunapenda maendeleo ya soka nchi hii na wewe hapo ulipo timiza jukumu lako, si kulaumu viongozi tu.