Usiwe na akili ya kukariri, Monastir ambaye ndiye anayeongoza kundi la Yanga na ambaye ndiye timu iliyomtoa bingwa mtetezi (Berkane) katika mashindano, imeshindwa kumfunga Bamako nje ndani. Monastir walitanguliwa ila wakaja kuchomoa goli na mechi kuisha sare.
Kitu cha pili ni kwamba Yanga hakuwa na utamaduni wa kufanya vizuri akiwa nyumbani, huo utamaduni alikuwa nao Simba wa kutegemea kuwa utakuja nawewe kwetu utaona. Yanga walimtoa Club African nyumbani kwake huko huko. Bamako kaponea chupu chupu kufungwa kwake kasawazisha dakiks za mwisho.
Kama unafatilia mpira utaona kuna kitu kinaenda kutokea mbeleni, endapo hakutakuwa na mvurugano wa kuondoka wachezaji muhimu na benchi la ufundi la Yanga na kufanya maingizo machache tu, Yanga inaenda kutengeneza ufalme wake katika michuano ya kimataifa. Timu zinachozeza na Yanga zinacheza kwa nidhamu kubwa na kuwa wanyonge na kusubiria counter attack hata wakiwa majumbani kwao. Ni wakati tu wa Yanga kujiimarisha katika mapungufu machache waliokuwa nayo. Kwenye performance ipo vizuri ni swala la kujiimarisha katika umakini tu (ushambuliaji na ulindaji)